Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Tuzidi kuwaombea viongozi wetu watuongoze kwa busara, hata ng,ombe akiswagwa hajui anapelekwa malishoni!
 
Akupeleke kwani wewe umekuwa zombie? Raisi Magufuli hayuko hapa kukupeleka wewe popote pale, bali wewe ndiyo unatakiwa ujipeleke mahali kwingine, wewe ndiyo unatakiwa ujitoe hapo ulipo na kwenda sehemu nyingine, wewe ndiyo unatakiwa ujifungue minyonyoro uliyofungwa na fisadi Lowasa, Mbowe & Co. na kuwa mtu huru Raisi Magufuli hawezi kulifanya hilo na wala siyo kazi yake!
mijitu bwanaaa...serikali ina wajibu wa kuendeleza watu wake Lumumba mnakosa exposure ...Ulaya unapewa mkopo ukiwa na proposal tu..50m kila kijiji ziko wapi
 
Kuongeza mishahara ya watumishi imekuwa ni danadana tu huku kukitolewa visingizio kadha wa kadha tangu awamu hii iingie madarakani.

Mbali na kukwepa kuongeza mishahara kwa visingizo mbalimbali kuanzia uhakiki na sasa tunakamilisha kwanza miradi mikubwa,teyari tumeshuhudia walimu wa masomo ya sanaa wakihamishwa kutoka shule za sekondari kwenda msingi kwa maelezo wamekuwa wengi kuliko mahitaji.

Vile vile tunashudia danadana za kuajiri.Kwa mfano zile nafaai zaidi ya 52,000 zilizowahi kutangazwa siku za nyuma sijui kama zote zimeshajazwa mimi sielwi.

Kwa trend hii naanza kujiuliza hivi huko mbeleni hakuna uwezekano wa kuja hata kupunguza baadhi ya watumishi wa umma kwa baadhi ya kada/sekta? za utumishi wa umma?

Kama wameweza kuwahamishia walimu wa sekondari na kuwapeleka katika shule za msingi,hii sio dalili kuna siku wanaweza kupunguza watumishi wa umma walioka katika baadhi ya kada za utumishi wa umma?

Nawaza mengi tu wajameni!!
 
Magufuli ni mbaguzi tena wa waziwazi kama anadiriki kuyasema haya hadharani je yasirini si yatakuwa yanatisha.

1. Serikali yangu lazina wawe wanatoka ndani ya ccm tu.

2. Sasa ni zamu ya kanda ya ziwa na kusini

3. Marufuku kuwabomolea wa mwanza ndio walio mpa kura

4. Hakuna bunge live, yeye kutwa yuko live

5. Aliyesoma private school hakuna mkopo, yeye aliyesoma seminary ilikuwa ni government?

6. Waliopata tetemeko yeye hakuleta tetemeko hela ya maafa ikaenda kujenga shule ya ccm na wahanga wakaisoma namba.
 
Wa kulaumiwa na JK na Mkapa!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Hatuwezi kuwa na Rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli, hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya Rais au Waziri Mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu.

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je, anajua jinsi ya kututoa?! Anajua anakotupeleka?

Nimejitahidi kuangalia Bunge ili nione labda Mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!
Huu uzi mpaka leo sijaelewa kwanini haujapewa sifa ya kuwa sticky
 
Kuongeza mishahara ya watumishi imekuwa ni danadana tu huku kukitolewa visingizio kadha wa kadha tangu awamu hii iingie madarakani.

Mbali na kukwepa kuongeza mishahara kwa visingizo mbalimbali kuanzia uhakiki na sasa tunakamilisha kwanza miradi mikubwa,teyari tumeshuhudia walimu wa masomo ya sanaa wakihamishwa kutoka shule za sekondari kwenda msingi kwa maelezo wamekuwa wengi kuliko mahitaji.

Vile vile tunashudia danadana za kuajiri.Kwa mfano zile nafaai zaidi ya 52,000 zilizowahi kutangazwa siku za nyuma sijui kama zote zimeshajazwa mimi sielwi.

Kwa trend hii naanza kujiuliza hivi huko mbeleni hakuna uwezekano wa kuja hata kupunguza baadhi ya watumishi wa umma kwa baadhi ya kada/sekta? za utumishi wa umma?

Kama wameweza kuwahamishia walimu wa sekondari na kuwapeleka katika shule za msingi,hii sio dalili kuna siku wanaweza kupunguza watumishi wa umma walioka katika baadhi ya kada za utumishi wa umma?

Nawaza mengi tu wajameni!!
Danadana maana yake hawana uwezo huo,hivo visingizio lzm viwe vingi, si ajabu wakajakopwa hata huko mbeleni.
 
kuna watu hata uwaambie hatari hiyo hawastuki mpaka iwakute ndio huanza ninge!! ukisikia mtu anasema ninge ujue alikua mbishi.

sasa nadhani kwa wale ambao mpaka wazame hatarini ndio hushituka kwa mbaali wanaona alarm ya hatari kwa huyu kipenzi wao kwamba sio.

akasema watoto waliomimbwa no school wakapiga makofi huku wakijiuliza maswali bila majibu.

sasa kasema kama uliweza kulipia lak tano au milion huna sababu ya kukopa tena. ww ni mwendo wa kulipa keshi tu hata kama ni million kumi. haijalishi hata kama ni mkopo.
haijalishi hapo awali ulikua na uwezo na sasa huna utajiju. haijalishi kuna watu walikusaidia hapo mwanzo ni lazma wakusaidie mpaka chuo kikubwa. utafikiri hela ni zake binafsi. kumbe hela ni zetu wote tunaosoma kwenye vumbi na kwenye viti.

hapa nadhani kidoogo hata wa kijani wamestuka. ila naawaambia bado kuna kubwa ataamuru tutii na litakua kubwa ndio wote tutaimba wimbo mmoja. naota siku moja atasema shule za watu wa kambo zifungwe wote tusome shule za kata . si mnajua ana wivu zile shule zinafundisha sana!! ndio mtajua hafai. sahiz endeleen kumvumilia.

mimi sinjamsema mtu ila siku akisema wote tuhamie dodoma kwa vile pale ndio mji mkubwa haitakiwi iwe na watu wachache ndio mtajua huyu mtu sio kabisa.
 
Habarini wadau.
Yaani hii nchi sijui ina matatizo gani. Kila mahali siasa inataka kuingizwa.
Walianzia sukari kutafuta kiki za kijana, sasa kila mtu anajua bei ya sukari ilipofika.
Wakaja kwenye mafuta ya kula nako ni hivyo hivyo, bei mtaani ni tatizo.
Kwenye shule binafsi nako wakaingilia kutaka kupandisha ada, elimu bure imewashinda wakaona watafute kiki shule binafsi, mara hamna kukariri darasa, hivi mtu kainvest mahela marefu bado unataka kumpangia namna ya kuendesha shule yake huku kichekesho kikiwa shule ya serikali kushika mikia kila mwaka, waboreshe shule zao ili wacompete na si kuleta siasa za kijinga.
Ila kikubwa kabisa na MD mpya ambao vodacom wanamtaka ila siasa nayo inataka kuingizwa na mwisho wa siku shirika life.
Vodacom kwani ni kampuni ya umma ama? Watu wameamua kumweka boss mpya kwa mitazamo yao serikali inataka kuleta siasa.
Yaani hii nchi bana, miezi sasa noah hazijaja huku tulitangaziwa matrilioni yanarudi. Tanzania ni taifa la ajabu na tuna viongozi wasio na maono bali kufikiria tumbo lao tu.
Nawasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom