Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Sukari imefika 3200 na unga wa mahindi 2200, where are we going????? Masikini wanaendelea kuwa masikini zaidi, na washangiliaji nao wanajitahidi kumshangilia kwa kila jambo.
Mkuu unakaa wapi!? Mbona hiyo bei yako ya sukari kubwa sana!? Na unga umeshaanza kushuka bei..
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema "hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho ataamka amefikiria nini au ameshauriwa nini na mke wake". Kwa wakati ule kilionekana ni kijembe kwa mzee Mwinyi lakini leo kauli yake inaonyesha maana.

Hatujui mwelekeo wa nchi kiukweli hatujui kesho atafukuzwa na nani au ziara ya rais au waziri mkuu itakuwa wapi. Hatujui kama tutaamka tunafagia barabara au tutaingia ofisini kwetu kama kawaida.

Hatujui tunaanza na nini, kujenga viwanda au kuboresha miundombinu na kuimarisha kilimo ili tupate malighafi.

Hatujui tatizo la sukari kwa mfano linaondoka kwa kurekebisha viwanda vyetu na kuongeza uzalishaji wa miwa au kuruhusu sukari ya nje au tuvamie magodauni ya watu

Ukimuangalia usoni na ukasikia anachotamka unakiri ana nia kabisa ya kututoa hapa. Swali ni je? anajua jinsi ya kututoa?

Anajua anakotupeleka? Nimejitahidi kuangalia bunge ili nione labda mawaziri wake wanaweza kuonyesha mwelekeo, huko nikachanganyikiwa zaidi.

Mwanamtandao mmoja alisema unaweza kuwa na dereva mzuri anayefuata sheria zote za barabarani lakini hajui anaenda wapi!

Umepotea?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mkuu alituahidi hatotuangusha.mbona mimi naona tumeshaanguka tena tumeangukia pua na pumzi zinaenda kukata au ni ule msemo wa wahenga kwamba baada ya dhiki faraja?
 
Rais anatupeleka tunakopaswa kwenda, na anachojaribu kufanya ni kujenga msingi wa kitu kinaitwa the Development State Model. Kwa sasa anajaribu kusahihisha makosa tuliyoyafanya huko nyuma ili kujenga msingi imara. Hata mataifa yaliyoendelea yaliendelea kwa sababu yalithubutu kurekebisha makosa yao na kusonga mbele. Kila anachofanya rais ni katika kuhakikisha kuwa tunaweka mambo sawa ili tuwe na msingi wa maendeleo. Kwa mtu yeyote mwenye uelewa ataelewa ninachojaribu kusema. Na kama rais atapata ushirikiano wa kutosha nchi itasonga mbele. Tatizo la walio wengi tunapinga kila kitu kwa kujua au kutokujua.
 
Mbona siona hoja hapa ktk andiko lako . . ?!

Kujenga DEVELOPMENT STATE MODEL ndio kudhibiti uhuru wa vyama vingine vya siasa ?! Au ni kudhibiti Uhuru wa habari na vyombo vya habari . . ?!

Hebu toa definition ya hii DSM uliyotaja . .
 
Sema sielewi, usiseme huoni hoja. Nitajie nchi hata moja iliyoendelea kwa kukumbatia hicho unachoita demokrasia mwanzoni mwa mchakato wa maendeleo yake. Nchi zote duniani zimekuja kukumbatia demokrasia baada ya kupata maendeleo. Huwezi kuendelea huku umewaachia watu wafanye kila wanalotaka. Paul Kagame wa Rwanda alikuwa anapigiwa kelele hivyo hivyo. Leo wanamwelewa alichokuwa anafanya. Hii tendency ya kuwa brain washed kuwa vyama vinakandamizwa ni upuuzi wa Hali ya juu. Sasa wewe subiri utamwelewa rais baadae.
 
Mmenielewa? maana naona toka aanze kuchaji hainyeshi kupata hata kijiwe kimoja.

Jamani, katumbua majipu hatujaona usaha, sijui unabaki ndani?
Wafanyakazi Hewa kaokoa Shilingi ngapi, hajasema,
Wanafunzi Hewa kaokoa Shilingi ngapi hajasema,
Kazuia Siasa za upinzani, CCM wanafanya Siasa kasaidia kiasi gani CCM kupendwa hajasema,

Sijawahi kusikia toka nianze kujua tunaendeshwa kwa Bajeti kwamba bajeti imeferi kutekelezwa, sio kutekelezwa tu, kutokutekelezwa kwa asilimia 50. yaani 50% sijawahi.

CCM mwambieni awaamini watendaji wa Serikali, awaachie watumie akili zao, awatengenezee sheria za kuwabana sio kuwabana kwa mabavu.

Mwambieni msimwogope Simu bila Betri ni Sawa na kujipulizia Pafyumu bila kuoga.
 
Utawala wa Magufuli unasadifiana sana na biashara za Mzee mmoja pale Morogoro aliyejulikana kwa jina la Banzi. Mzee huyu alikuwa ni mfanyabiashara maarufu na mwenye kujituma sana. Jitihada zake zilimpelekea Mzee huyu kuwa na mafanikio makubwa sana kimaisha. Tatizo kubwa la Mzee huyu lilikuwa ni kutaka kufanya kila kitu peke yake (wazungu wangesema Ku-micronage) na zaidi ya yote kutowafundisha watoto wake misingi ya biashara yake. Bahati mbaya siku moja Mzee huyu alipatwa mshtuko wa moyo na kufariki. Watoto wake walijitahidi kuziendeleza shughuli za baba yao lakini walishindwa kwani walikuwa ni wageni na hawakujua kwa undani biashara zile.

Familia ya Mzee Banzi tunaweza kuifananisha na Tanzania ya Magufuli. Taifa letu haliongozwi kwa misingi ya katiba bali utashi wa Bwana Mkubwa. Tumeona Wapinzani wakiwekwa ndani bila ya sababu za msingi. Pili, tumeona manunuzi makubwa ya serikali yakifanywa bila ya kulihusisha bunge letu. Tatu, vyama vya upinzani vimezuiwa kufanya shughuli zao wakiambiwa wasubiri mpaka mwaka 2020. Nne, tumeona sheria zikipindishwa kuwalinda wale walio karibu na Mheshimiwa kama kina Bashite na mbaya zaidi watu hawa wamejiusisha na vitendo vya dhahiri vya ukiukwaji wa sheria na hawajafanywa lolote. Tano, pamoja na sifa nyingi alizopewa huyu Mheshimiwa ameshindwa kufanya kazi yake namba moja kama kiongozi ambayo ni usalama wa raia wake! Huko Kibiti watu wamekuwa wakiuwawa na serikali imeshindwa kueleza ni nini haswa kinachoendelea.

Vitu vyote vinaashiria uongozi uliopwaya. Na kusema ukweli utawala umegubikwa na matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Hakuna taifa hapa duniani lililopiga hatua bila ya kuwa na misingi mizuri yenye kuheshimu sheria walizojiwekea. Serikali inayojaribu kuwanyima wapinzani uwezo wao wa kufanya kazi ni serikali ya kuogopwa kwani inachojaribu kufanya ni kutotaka kukosolewa. Kitu hiki ni kibaya kwa ustawi wa taifa kwani kinauwa mfumo wa Check and Balances. Ni muhimu kwa viongozi wetu kutambua ya kuwa nafasi walizonazo sio za milele kwa hiyo watumie muda wao kujenga taasisi badala ya kujijengea sifa wao wenyewe. Tatizo kubwa la uongozi wa style ya Magufuli ni kuwa maendeleo yanayopatikana ni ya muda mfupi na mara nyingi yataendelea kuwepo kama tuu kiongozi fulani ataendelea kuwepo....
 
"mungu mdogo" - hahitaji sheria,katiba,bunge bajeti wala ushauri wa shetani au malaika kufanya atakalo ,kwani jeshi na polisi si wanafuta amri yake?
 
Teh..teh...Maimamu wa karibu misikiti yote Dar es salaam baada ya kupewa "FUTARI" na Bashite mawaidha yao mengi ni kumuunga mkono Magu na utawala wake.Inakumbushia zile milioni kumi kumi waluzopewa wabunge wa CCM.Maimamu wa Dar bei rahisi sana

Nasubiri siku Bashite awaite Pengo,Malasusa,Shoo,Gwajima,Kakobe Lusekelo nk..awagaie mchele na sukari ..
 
Hii ni dharau au kejeli
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom