Anayejua kuhusu malipo wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi serikali za mtaa

mimi nimesema hivi: wasimamizi wasaidizi walisimamia uandikishaji kwa siku 7--tangu jumamosi hadi ijumaa. so kwa rate ya tsh 10,000 walipaswa walipwe 70,000 kwa zoezi la uandikishaji tu. siku ya uchaguzi inatakiwa walipwe sh 10,000. ila wameambiwa watalipwa 50,000 (kwa siku 5 za uandikishaji badala ya siku 7!)--wameishalipwa 20,000 deni limebaki la 30,000--watamaliziwa lini haijulikani! unaona ufisadi huu? hapa pana harufu ya UFISADI!
mkuu hapo tayari mmeshaibiwa, dar walilipwa 70000 kwa siku 7, hawa wakurugenzi hawawezi kukulipa moja kwa moja kilichopangwa, lazima wachakachue, hiyo ndo jadi yao.
 
huku kwetu mkuranga hatukufanya semina, pili tuliambiwa kila siku ni tsh. 10,000/=, tatu eti leo ndio tumepigiwa simu na watendaji wetu kuwa fedha zimefika na kuwa tutakuwa na semina ijumaa ambapo tutakipwa 20,000/= na jumapili tutalipwa 30,000/=
haa haa, hii ndo tanzania ufisadi kila kona, watanzania tusipochukua hatua ya kuliondoa hilo dude la ccm mapema itakula kwetu.
 
Nchi yenyewe kila MTU mwizi tu. Ukamweke mtanzania mwenzio juwani siku nzima umlipe elfu kumi . ni dharau ya hali ya juu.

Miaka ya nyuma hizi kazi waliwapa waalim sijui sasa imekuwaje.
 
Nchi yenyewe kila MTU mwizi tu. Ukamweke mtanzania mwenzio juwani simu nzima umlipe elfu kumi . ni dharau ya hali ya juu.

Miaka ya nyuma hizi kazi waliwapa waalim sijui sasa imekuwaje.

Waalimu wameamka usingizini nao wanataka kulipwa pesa ndefu sasa alternative ni kusaka cheap labor... It really hurts hii nchi ni Kama haina viongozi tupo Kama hatupo
 
Nchi yenyewe kila MTU mwizi tu. Ukamweke mtanzania mwenzio juwani simu nzima umlipe elfu kumi . ni dharau ya hali ya juu.

Miaka ya nyuma hizi kazi waliwapa waalim sijui sasa imekuwaje.
Siku hizi hawataki Walimu wanasema Walimu wana chuki na Serikali.. Walimu wengi walio omba Hii kazi walipigwa chini. Ndo maana hata kuandikisha daftari la wapiga kura, watatumia wanajeshi..
Wanaogopa yaliyowakuta kwenye SENSA chezeya Walimu wewe!
 
hii nchi sijui tunaipeleka wa nimefanya kazi siku 30 nalipwa elfu 70..mbona wizi hii.
 
huku kwetu mkuranga hatukufanya semina, pili tuliambiwa kila siku ni tsh. 10,000/=, tatu eti leo ndio tumepigiwa simu na watendaji wetu kuwa fedha zimefika na kuwa tutakuwa na semina ijumaa ambapo tutakipwa 20,000/= na jumapili tutalipwa 30,000/=

Mkuu, hawa wakurugenzi ni MAJIZI wakubwa! Tayari hapa mmeliwa Tsh 50,000/=!!!!! Hii nchi bora mtu uwe jambazi au FISADI ndipo uta-enjoy maisha. MAJIZI yamejaa kila mahali!
 
Siku hizi hawataki Walimu wanasema Walimu wana chuki na Serikali.. Walimu wengi walio omba Hii kazi walipigwa chini. Ndo maana hata kuandikisha daftari la wapiga kura, watatumia wanajeshi..
Wanaogopa yaliyowakuta kwenye SENSA chezeya Walimu wewe!

hahahahahaha! walimu waliwakomesha kwenye sensa....hawana hamu nao tena!
 
wajumbe wa bunge la katiba walikuwa wanalipwa ngapi kweli kwa siku ? msimamizi wa uchaguzi alipwe 30000?!!! kweli mbombo ngafu.
 
Huku kwetu hawataki watu wenye uelewa, wanachukua std seven na watendaji Wa vijiji kusimamia. Kaaaz kwelkwel
 
Huku mbinga wamelipwa 35000 kwa siku 7, na pia watalipwa 15000 kwa ajili ya usimamizi. Kiujumla wakurugenzi wengi ni wezi na mafisadi wakubwa, yaani waziri mkuu pinda anaangalia tu jinsi mafisadi haya yanavyozidi kutamba mchana kweupe! Hapo watu wameshanunua viwanja na kujenga majumba kwa kodi za walala hoi.
 
Daftari la uandikishaji ukweli walitakiwa kupewa 120000 kwa siku saba pus semina. Huuwizi unapigwa na wakurugenzi , pamoja na watendaji wa kata na mitaa , vijiji na vitongoji.. Kwa sababu iweje watu wa tabora walipwe tofauti na watu wa iringa au mbeya. Ikiwa wote wanafanya kazi chini ya mamlaka moja ya TAMISEMI. Hii nchi imeoza kila sekta kuanzia mlinzi getini hadi boss mkubwa na anayepaswa kulaumiwa ni RAISI maana yeye hajawahi kuongelea swala lolote juu ya kumwajibisha fisadi au mwzi ndani ya serikali yetu hii.
 
Back
Top Bottom