Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,664
- 22,255
WanaCCM wanaoshabikia Sumaye kuukosa uongozi wa juu CHADEMA wamefadhaika lengo lao kukwama. Sumaye angetaka kuonesha uaminifu wake CHADEMA angetumia muda mrefu kuwa mshauri wa chama hicho ili ajijengee uaminifu usio na shaka.
Sumaye alipokuwa Waziri Mkuu alikula viapo Serikalini kuhusu kuhifadhi siri za Serikali na viapo hivyo ni vya kudumu mpaka mwisho wa uhai wake hivyo mchango wake kwa CHADEMA itakuwa wa kawaida na wenye mashaka kumpa nafasi ya juu kabisa ya chama.
Lazima tujue kuwa Sumaye muda wote yuko chini ya uangalizi maalum wa huko alikotoka kuhusu viapo vyake, (like strangers but do not trust them)
CCM walikosea sana kutumia juhudi nyingi sana kuhakikisha Sumaye anashika chama ili waweze kujipenyeza na kukiua chama, juhudi hizo ndizo zilizowaamsha wanachadema na kuwa na shaka isiyo na shaka.
Mwisho ningetegemea baada ya kuukosa uongozi wa juu kabisa yeye asingejitoa ili aweze kujijengea uaminifu wa ziada na kuonesha uhalali wa kuchgua na kuchaguliwa, angewauliza wale wanaoshabikia kuwa lazima ashinde nafasi ya juu ya CHADEMA walitaka nani asishinde na kama ni hivyo kwanini walifanya uchaguzi badala ya kuteuliana.
CCM mnapokuwa na projekti nyeti msijioneshe wazi mkaleta mashaka.