Anayejua anisaidie namna ya kudhibiti Sisimizi

WANKIE

JF-Expert Member
Jan 25, 2013
984
313
Habari wana JF!

Katika nyumba yangu kuna tatizo la sisimizi.

Hivi sasa imekuwa ni kero mtindo mmoja. Kwa yeyote anayefahamu, naomba anijuze nitumie dawa gani ili wadudu hawa wapotee kabisa ndani ya nyumba yangu.
 
Tafuta dawa inaitwa SUPER 10 inauzwa na hawa watu wa GLND imenisaidia sana.Ni PM jtatu nitakuagizia wapi ukanunue na shs ngapi.
 
Akheri powder utasahau tatizo la sisimizi. Inauzwa buku 3. Nyunyiza kwenye kona za nyumba
 
mkuu nakushauri na usafi dawa haita saidia kama vyakula vinapikwa kwa kumwagwamwagwa. zingatia hili na dawa.
 
mbona mmekaa kimauaji tu?hebu wapeni haki yao ya kuishi! unaonaje ukiwawekea hivyo vyakula wanavyovifuata ndani sehemu kama bustanini au kwenye yard yako?kitu kingine sisimizi ni wadudu wa msimu ukiwaona ndani basi ujue wanakimbia 'mafuriko'nje wahurumie!mi hata mbu huwa nawategeshea mguu wavyonze waende zao halafu nalalaa bila bugudha!na nina chumba changu special kwa ajili ya kunguni , mende na mapanya!
 
Wadau habari za asubuhi?

Naomba kuuliza mwenye kujua dawa ya wadudu waitwao sisimizi,mchwa,siafu nk.Hao wadudu wamekuwa wakinisumbua mara kwa mara nyumbani kwangu,sijajua chanzo ni nini?

Nimejaribu kutafuta na kutumia dawa mbali mbali bila mafanikio,hivyo naomba msaada wenu kwa yeyote mwenye kujua dawa ya kumaliza tatizo hilo.

Asanteni wote.
 
fuatilia ile njia yao uone wanaanzia wapi then tafuta oil iliyotumika mwaga kuzunguka eneo lako kamwe hawatarudi tena
 
mbona mmekaa kimauaji tu?hebu wapeni haki yao ya kuishi! unaonaje ukiwawekea hivyo vyakula wanavyovifuata ndani sehemu kama bustanini au kwenye yard yako?kitu kingine sisimizi ni wadudu wa msimu ukiwaona ndani basi ujue wanakimbia 'mafuriko'nje wahurumie!mi hata mbu huwa nawategeshea mguu wavyonze waende zao halafu nalalaa bila bugudha!na nina chumba changu special kwa ajili ya kunguni , mende na mapanya!

???????????:-D
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom