Anayejua aina nzuri ya perfume

Habari, nimeulizia hiyo dark fever nimeambiwa ni 20,000/=

Kwa hiyo bei ya 12,000 wanauza wapi mkuu
Kuna duka nlinunua lipo mbande magenge nilichukua kwa bei hiyo 12, 000 ila kwasasa lina muda mrefu duka halijafunguliwa huenda jamaa kahama.
Jaribu kuja kuulizia mbagala zakhem pale itacheza bei ya 12 au elfu 10 kabisa
 
Kabla ya kununua perfume elewa tofauti ya deodorant na perfume.

Perfume (unyunyu): Hii huwa na manukato ya kudumu kwa muda mrefu (hapa ondoa zile perfume fake za buku tano tano), maranyingi watu hu-spray kwenye nguo au mwilini kidogo na huwa na bei zaidi ya deodorant/body spray.

Deodorant (aerosol/spray, roll-on, body mist n.k): maalum kwa mwilini kuzuia harufu lakini haidumu kwa muda mrefu na katika hizi deodorant zipo ambazo huondoa tatizo la kutoa harufu mbaya kwa muda mrefu mf: Anti-perspirant deodorants hii hupunguza kiwango cha bacteria kwenye ngozi yako na kuzuia jasho lisichanganyikane na bacteria, elewa jasho huwa halinuki ila likichanganyikana na bacteria wa kwenye ngozi ndio hutoa harufu (lakini kuwa makini kuna baadhi husema deodorant zinazozuia jasho mfano la kwapani sio nzuri sababu huziba tezi za jasho kwa muda mrefu).

Body spray huwa hazina bei sana kwa ufahamu wangu hizi tunazokutana nazo kwenye maduka yetu huwa kuanzia Tsh. 5,000 hadi 30,000 au zaidi (mf. product za forever) lakini perfume ukitaka nzuri angalau nunua ya kuanzia Tsh. 20,000 na kuendelea lakini zipo hadi za 200,000 na zaidi ya hapo.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom