Anayeishi "condemned cell" anaweza kuishi salama na aliye uraiani akatwaliwa. Mungu huyu ni fundi!

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Familia ya Mbowe imethibitisha kupitia ukarasa wa tweeter kwamba baba yao amechanganywa na wafungwa wanaosubiri kunyongwa. Tunaamini waliofanya haya hawataweza kumnyonga ila wanaweza kumweka kigungoni milele. Lakini aishivyo Mwenyenzi Mungu alimweka huyu Condem pia anaweza akatwaliwa katika ulimwengu huu na mrithi wake akamtoa Mbowe.

Ila Jambo hili linakuwa gumu pale ambapo linafanywa na Watanzania wenzetu, waumini wenzetu wa dini na watu wanaolipwa mishahara na sisi kwa sababu tu wanaamini wao walizaliwa kututawala na iwavyo isivyo lazima tutawaliwe.

Haya yanafanyika katika Taifa ambalo linadai Lina viongozi wa dini lakini viongozi hao wa dini wameshindwa kabisa kufungu na kuomba ufunuo juu ya madhara ya uchungu unaosambazwa na watawala wetu.

Yanafanyika kipindi ambacho majirani zetu wanashangilia kuona na sisi tumegawanyika na wanajiandaa kututawala na kutwaa ardhi na rasilimali zetu Kama ilivyo Kongo. Naamini tunalo jukumu lakuwaamsha usingizini watu Hawa,viongozi wastaafu msione kama mpo salama Sana.

Mwisho niwaombe wenye Magereza wasikae kimya juu ya tuhuma hizi vinginevyo Kama ni za kweli na wao kwa utaratibu wao wanaamini hiki ndicho kinapaswa kufanyika.

Hatupo wamoja tena, nafsi zimeinama katika kila sekta. Naamini hata ndani ya nafsi za mawaziri na wakuu wa vyombo upo mgogoro mkubwa juu ya kesho ya watoto wao. Haiwezekani kila mtu alalamike, Kuna shida mahali na tunahijua japo atulazimishwi kuwalazimisha mfanye tuonavyo sisi.
 
Inaweza ikawa ni sehemu salama na pakistarabu kuliko angechanganywa na mahabusu wa kawaida.
 
na nyie na mbowe wenu hebu tupisheni kwanza tufanye mambo mengine ya kimaendeleo. 'Kutoka' tena kwa chama chenu kupitia njia hii au yeyote ile kwa sasa naona ni ngumu mno. Kiukweli huku mtaani (mnaweza kufanya utafiti wenyewe mkipenda (kama hamuamini hili)) watu hawana habari kabisaaa na suala la mbowe au chadema kwa ujumla.....yaaani wapo kimya kabisa wanajadili mambo mengine tu km tozo n.k Pita kwenye mabao, pita kwenye vijiwe vya kupiga kahawa au alkasusu, pita kwenye madraft, pita vijiwe vya bodaboda n.k hali ni hiyo.

Hali ni tofauti kabisa na ilivyokuwa chadema ya miaka ile ya 2010 kuja juu....jambo dogo tu kwa chadema lilivuma kila pembe. ukweli ni kuwa MMEPOTEA, huo ndo ukweli. Upoteaji huu, kwa mawazo yangu, umetokana na kutoeleweka kwa misimamo yenu (kuunga juhudi, kumpokea na kumpitishaa lowasa (mliyekesha kumsema), kuipindisha katiba yenu kwa manufaa ya mwenyekiti pekee n.k). Lkn kubwa zaidi ni dhambi inayowatafuna ya kutokubali kuyaona mapungufu yenu na kujisingizia nyie ni wachaMungu saaana na kwamba mpo sahihi kwa kila jambo. Katiba ya wengine mnakosoa vikali inapovurugwa; ajabu yenu ikivurugwa kwa manufaa tu ya mwenyekiti mnakesha mkitetea kwa nguvu zote....inachekesha sana!

Kwa sasa, hata gwajima anazungumzwa zaidi mtaani kuliko chadema na viongozi wake.....huo bdo ukweli mchungu 'makamanda'!

Km taifa hili limegawanyika au litagawanyika, kitu ambacho kwa sasa hakipo na Mungu Mkuu naamini hatokiruhusu, basi si kwa sababu ya chadema hivyo acha kulazimisha kisichokuwepo!
 
Watanzania tulikwisha gawanywa tangu alipoingia JPM na kusema mwanaccm asibugudhiwe.
 
Aisee km ni kweli wamekosea sana
Tunaweza tukaongea sana hapa kwa kuwa hatujui hizo cell zipoje lakini nikuambie tu..hao jamaa waliohukumiwa kunyongwa wanakuwa treated tofauti kabisa magerezani na ni sehemu salama kwa Mbowe...hata Hanje Nusrat aliwekwa huko wakati yupo ndani..ni bora kuwa huko kuliko kwenye kuchanganywa na wakawaida
 
Back
Top Bottom