Anayeingia kwa rushwa lakini Muungwana na anayeingia kwa huruma lakini Mnafiki nani mzuri?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Hivi mfano mgombea Urais wa Chuo Kikuu ambaye anajulikana kabisa kuwa anautaka Uongozi huo kwa kutoa rushwa lakini anajulikana pia kuwa ni Muungwana kwa wenzake na mpinzani wake ambaye ana sifa ya kuwa na Huruma kwa Wanyonge lakini ni Mnafiki na mbabe wa kichini chini unadhani ni yupi sisi Wanafunzi wa Chuo Kikuu tukimchangua tutafaidika nae ndani ya Uongozi wake wa Miaka mitano hapa Chuoni?

Nasubiri jibu lenu Wakuu kwani naingia muda mfupi kufanya Mtihani wangu wa Ethics na hilo swali tumetonywa kuwa lipo na Mimi GENTAMYCINE nataka kutusua na Distinction A kabisa ili niweze kufaulu na First Class.

Nitawashukuruni nyote na natanguliza sana Shukrani zangu kwenu wakati nikiyasubiri kwa hamu majibu yenu kwa swali Kuntu kabisa ambalo nimewaulizeni hapo juu.

Nawasilisha.
 
Huna haja ya kujiua ndugu yangu. Umefanya kazi iloyotukuka. Bora Lowassa angeingia madarakani.
 
Mh bora huyo anayeingia kwarushwa lakin anakuwa muungwana maana anakuwa kaonesha tabia yake ipoje, ila huyu mchini chini cbora kwasababu yawezekana hana hela ndiomaana hawez kutoa rushwa ila naamini angekuwa nazo angetoa nae rushwa
 
Nakumbuka miaka mi-i-ngi iliyopita kwenye essay ya English O Level swali lilikuwa:politics: a noble art or a dirty game? Ukiweza kusema ungekuwa wewe ungeandika nini utakuwa umepata jibu la swali lako
 
Back
Top Bottom