Anayehusika na Kituo cha Paradise Center akamatwe

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
271
484
Kwa miaka zaidi ya mitatu nimekuwa nikikutana na kakikundi ka watoto wadogo kwenye maharusi na kumbi mbali mbali hapa Dar wakijitambulisha kama yatima na uanza kutumbuiza na kutuzwa.

Tatizo liko wapi? Hawa watoto inaonekana ndio shughuli yao angalau mala 2 kwa wiki, yaani send off alhamisi/ijumaa na weddings Jumamosi, je wanapata wapi muda wa kusoma na kupumzika? Nani anawaandaa nakuwaleta kwenye hizi kumbi? Kwanini wawe ndio wahudumiaji wa kituo tena kwa kutumikishwa usiku mrefu? Nina imani mwenye kituo anapata misaada kutoka sehemu mbalimbali kwa mgongo wa hawa watoto.
 
Unanipa walakini mkuu maana kichwa na mada kama vimepishana vle, au ndio umewasitiri watu fulani au bado hauna uhakika?

Fafanua japo kidogo mkuu
 
Nimewahi kuona hili zaidi ya mara moja lkn swali langu..

Je, hawa wote wanatoka ktk kituo hicho hicho kimoja? Au kuna vituo vingi vinavyojihusisha na hili?.

Ingependeza zaidi ukisema ahojiwe na sio kukamatwa.
 
Mkuu taarifa yako haijakaa kischool. Inaweza isipendeze kufanyia kazi.
 
Kumkamata tu inatosha kubadili hali ya maisha ya hao watoto? Ungechukua wakwako pia mtaani uwalee kisha uwatumie kama unaona ni mradi! Hujui kwamba wanachopata kinawasaidia kwenye kuendeza maisha ya kila siku?
 
Ndugu, nadhani huelewi kinachoendelea, haiwezekani watoto waanze kuzunguka kumbi baada ya kumbi usiku kutumbuiza kila wiki na bado nina uhakika wanachopata kinaishia mfukoni kwa mtu, hivi vituo vingi vinawatumia hawa watoto vibaya, ila kama kwako ni sahihi basi nategemea na wakwako watakuwa katika shughuli hizo.
 
Mimi nadhani kwa ulichoandika heading ilitakiwa wenye kuandaa harusi wakamatwe!
Au moderator wasaidie hilo.
 
Ikiwa wewe ni mtu mwema na kwamba unachofanya ni kuwanusuru hawa watoto ungaliweza kutoa suluhisho ambalo halitawakwamisha hawa vijana badala ya kutoa hukumu ya moja kwa moja ambayo hutolewa tu na watu wenye roho ya husda!
 
Nimekuelewa mkuu. Unadhani ningewekaje heading maana kusema kweli mimi binafsi nachukizwa na hii tabia.
 
Mimi nadhani kwa ulichoandika heading ilitakiwa wenye kuandaa harusi wakamatwe!
Au moderator wasaidie hilo.
Hawa watoto uwa hawaalikwi. Wanaibukaga nakuomba watumbuize. Kwasiku wanaweza tembelea kumbi hata nne.
 
Nimekuelewa mkuu. Unadhani ningewekaje heading maana kusema kweli mimi binafsi nachukizwa na hii tabia.
SASA MLITAKA MWAKUTE MITAANI? HUYO ALIYEFANYA MPANGO WA KUWAKUTANISHA NA WENYE ROHO NJEMA AMBAO SIO RAHISI KUWAKUTA BARABARANI WAPATE ANGALAU KIDOGO UNAONAJE? INASIKITISHA K6WAONA LAKINI NI KWELI WANAHITAJI MSAADA WAISHI KAMA WOTE WANAOHUDHURIA HAPO. KITU MUHIMU NI AIBU LAKINI MFICHA UC h HAZAI
 
Back
Top Bottom