mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
820
1,335
Habari wadau, niliwahi kuja na uzi hapa kuhusu D09 CLUB Miezi michache kabla haijapotelea kusikojulikana na nilishambuliwa sana na waliliwa pesa zao na bila kujua hatma yao wanarudishiwa vipi na nani. Leo naomba nije na mambo 30 usiyoyajua kuhusu Qnet.

Qnet ni network marketing ambayo imevuta member wengi waliokua d09 Club kuingia huko haina tofauti kubwa na network marketing zingine unazozijua wewe mfano lugha wanayotumia kukushawishi zinafanana na wale wengine.

Kiuhalisia wanakuekea mazingira mazuri ya kuona unapata pesa kirahisi sana lakini kiukweli hakuna pesa rahisi unawafanyia kazi na wanakulipa kama kazi zingine lakini mfumo wao wa ulipaji na uendeshaji wa biashara yao ndio uko tofauti na wengine.

1. QNET ILIANZISHWA LINI?

Mwaka 1998 kampuni hii ilianzishwa huko Hong Kong mwaka ambao:

-Kampuni ya kutengeneza magari ya Benz iliinunua kampuni ya Chrysler kwa gharama za $36 billion ambayo ilivunja rekodi ya Dunia na kua biashara kubwa zaidi kihistoria kufanyika mpaka mwaka huo.


  • Elton John anakua shoga wa kwanza kutunukiwa heshima ya "Sir" na malkia wa Uingereza
  • Mwaka huo huo mwanzilishi mwenza wa google Larry Page na mwenzie Sergey Brin, waliokutana Stanford University, wanaisajili rasmi kampuni ya google California kwa ajili ya kutoa huduma mtandao
  • Mwaka huo pia mmiliki na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft anatupiwa ice cream usoni akiwa Belgium

Ni mwaka uliokua na mapinduzi makubwa kiuchumi pamoja na vituko vingi vya kushangaza Dunia.

2. NANI MWANZILISHI WA QNET?
-Vijay Aswaran akiwa kama mwenyekiti wa QI Group na mwenzie Joseph Bismark akiwa kama Director wa QI Limited

3. Majina mengine ya QNET usiyoyajua:

  • Questnet
  • Goldquest
  • and QI Limited
4. Makao makuu yake na Office zao:
Makao makuu ya QNET yapo Hong Kong lakini wana Ofisi katika miji ifuatayo:

  • Malaysia
  • United Arab Emirates
  • Indonesia
  • Ireland
  • Singapore
  • Rwanda
  • Philippines
  • Turkey
  • India
  • Algeria
  • Azerbaijan
  • Cote D’Ivoire
  • Burkina Faso
  • Georgia
  • Guinea
  • Moldova
  • Kazakhstan
  • Myanmar
  • Niger
  • Mandalay
  • Ukraine
  • and Russia
5. WALIANZA NA BIASHARA GANI?
QNET walianza kwa kuuza "Custom Coins" mfano zile zinazotumika kutunuku washindi wa michezo mbalimbali katika mashindano ya michezo n.k na ilikua inaitwa Goldquest

6. QNET At The Olympics
Kampuni ya QNET ndio ilipata deal ya kutengeneza na kusambaza Olympic coins mwaka 2000 zilizofanyika Sydney,pia 2004 Athens Games na 2008 Beijing Games.

7. QNET At The World Cup
QNET tena wakalamba bingo la kombe la Dunia mwaka 2002 kama official coin distributor for the 2002 FIFA World Cup soccer championships.

8. QNET na QVI Club
Ili kujitanua zaidi na kuongeza kipato QNET iliingia ubia na kua mwekezaji mwenza na QVI Club kampuni inayohusika sana na Vacations and Travell.

9.QI Comm
Mwaka 2005 QNET ikaingia kwenye uwekezaji wa kampuni ya mawasiliano wakainunua British communications company na kuibadilisha kua QI Comm.

10. Prana
Mwaka 2005,QNET ikaingia kuwekeza Thailand na kuinunua Prana Resorts and Spa

11. Cimier
Mwaka huo huo 2005 wakakinunua kiwanda kikubwa cha kutengeneza saa huko Uswisi Swiss watch manufacturer Cimier.

12.Down To Earth
Mwaka 2007, kampuni ikapiga hatua zaidi na kununua kiwanda cha vyakula na afya huko Hawaii kinachoitwa Down To Earth.

13. Meritus
Kampuni ya QNET inaanza kusponsor the Meritus Malaysian Motor timu ya mashindano ya magari.Timu hiyo ilibadilishwa jina na kua MY QI Meritus.

14. Virgin Racing
Mwaka 2010, wakaingia ubia na Virgin racing ambao walikua wanashiriki pia the Grand Prix series mashindano makubwa ya mbio za magari Duniani.Haikufanya vizuri na waliacha nayo 2011.

15. Bidhaa ambazo QNET imewekeza tangu 1998 mpaka 2010
Mpaka mwaka 2010 QNET ilikua na bidhaa tofauti tofauti sokoni na zingine zikiwa ni zile mahitaji mhimu kwa binadamu kama afya na chakula.Kampuni ikaanz kujikita zaidi katika kutafuta wasambazaji katika category tofauti tofauti;

  • Health and wellness
  • Vehicle motor care
  • Personal Care
  • Beauty
  • Technology
  • Jewelry and watches
  • Holiday and recreational travel
  • and Education
Post ijayo ntakuja kuelezea namna QNET inavyolipa na nchi kadhaa ilikofungiwa na mmiliki wake kukamatwa mara kadhaa kwa mashtaka ya kutakatisha fedha (baadhi ya nchi)

======


Naomba tuendelee sehemu ya pili kisha ntatoa hitimisho kwa mtazamo wangu. Karibuni!

16. Namna wawakilishi/waliojiunga na QNET wanavyopata mgao
Haina tofauti sana na networking market zingine ama ile d09,lakini huku yule TOP (ambae ni QNET) ndio ananyonya member na member aliejuu yako hali jasho lako bali kwa juhudi zake ndivyo anapata commission zaidi na namna anavyoingiza member wapya ama kuuza bidhaa za QNET. kuna njia 10 za kupata pesa ya mgao wako baada ya kufanya kazi ya maana;

  1. Retail Profits
  2. Early Payout
  3. Step Commissions
  4. Repeat Sales Points
  5. Year-Round Incentives
  6. New Program Bonus
  7. Main Plan Rank Advance
  8. RSP Plan Rank Advance
  9. RSP Rank Advance Bonus
  10. and RSP Rank Maintenance Bonus
Sitazielezea hizi kwa undani kwa sababu si nia ya huu uzi labda tukijaliwa nafasi siku nyingine,nia ya huu uzi ni kukujulisha usalama wa uwekezaji wako juu ya QNET kisha uamue kujitundika mwenyewe, tuendeleee...

17.Quest University
Hiki ni chuoa cha QNET kipo Malysia (Perak) na wanatoa kozi za Afya na Uuguzi na zingine nyingi so far hakuna review mbaya kuhusu hiki chuo.

18. Australia
The Australian Office of Consumer and Business Affairs waliitaja QNET kama pyramid scheme 2002.

19. Nepal
Mwaka 2003, the Nepalese Home Ministry walifunga kazi na biashara zote zinazoihusu QNET nchini humo.

20. Sri Lanka
Mwaka 2005, waliishutumu QNET imeisababishia nchi hasara ya $15,000,000 kwa kuikosesha kodi na kufanya biashara zinazofanana na utakatishaji wa pesa, serikali ya Sri Lanka ikaipiga banned QNET nchini humo.

21. Iran
Mwaka huo huo 2005,Serikali ya Iran waliishtumu shutma zile zile QNET ilizokutana nazo Sri Lanka kua imesababisha hasara kwa nchi ya takribani $500,000,000 wakaipiga banned QNET pia nchini Iran.

22. Kukamatwa kwa Vijay nchini
Mwaka 2007, Direct Selling Association huko Indonesia waliishtaki QNET kwa serikali ya nchini humo, kua ni pyramid scheme. Interpol walimkamata Vijay Eswaran na wahusika wengine na kuwafungulia mashataka ya fraud. Wiki chache baadae washtakiwa wote waliachiwa huru na mashtaka yalifutwa na QNET ikaendelea kuoperate nchini Indonesia.

23. Maandamano ya kuipinga QNET nchini Afghanistan
QNET ilianza shughuli zake Afghanistan mwaka 2006.Na ilishika kasi kwa speed na kupata washirika wengi ndani ya mda mfupi na mwaka 2008 ikasajiliwa rasmi nchini humo.Ghafla siku moja kukazuka maandamano makubwa takribani watu 3,000 wakipinga namna QNET inavyofanya biashara zake nchini humo na mamlaka zikaibana QNET na kuipa masharti ya namna ya kujiendesha ikiwa nchini humo.

24. Sudan
Serikali ya Sudan government ika bann shughuli zote za QNET nchini humo kwa sababu ya malalamiko kutoka kwa watu walifanya nao biashara kutokupokea vitu walivyonunua na hata kama wakiletewa hivyo vitu quality yao ni mbovu Duniani hakuna hapo ilikua mwaka 2009.

25. Syria
Mwaka huo huo 2009, the Syrian Ministry of Economics wakaishtaki QNET kwa kufanya biashara kubwa nchini humo na bila kulipa kodi lakini pia kampuni inaendesha shughuli zake kwa mtindo wa pyramid scheme ambao ni kinyume na sheria za nchi hiyo QNET was not allowed to operate in Syria anymore.

26. Turkey
Mwaka 2010 huku ikijulikana kama Questnet, watu wanaojihusisha na Questnet wapatao 80 walikamatwa na 40+ walifunguliwa mashtaka ya "gaining an unfair advantage".Wakabadili jina la kampuni na kuanza kuitwa QNET, serkali ikaanzisha uchunguzi wa kina kuhusu QNET wizara ya biashara ya Uturuki. Mwaka 2011, QI Group wakanunua Dögan Hotel iliyopo Antalya, Turkey.

27.Egypt
Kampuni ilipelekwa katika chombo kinaitwa Dar al-Ifta al-Misriyyah ambacho kinasimamia maswala ya elimu na maadili ya kiislam. Dar al-Ifta al-Misriyyah wakasema QNET ni kinyume na hairuhusiwi pia italeta madhara kwa uchumi wa Egyptian hapo ilikua 2012.

28. Saudi Arabia
Mwaka 2010, the Saudi Arabia Ministry of Commerce and Industry walitoa onyo kali kwa wananchi wake kujihusisha na kampuni kama QNET. Na ilifungiwa mara moja kufanya shughuli zake nchini humo.

29. Kamata kamata nchini India
Mwaka 2008, the Central Bureau of Investigation huko India walianza uchunguzi na kupeleleza shughuli zote zinazofanywa na viongozi wa QNET.Walipitia historia ya mashtaka yote aliyoshtakiwa Vijay Eswaran and QNET ikiwa ni pamoja na yale ya kujihusisha na utakatishaji wa pesa. Walifreeze account za QNET na mwaka 2013 walianza kukamata wahusika wote

Serikali ya India haikua na sheria inayozungumzia kuhusu direct selling and multilevel marketing,hivyo hakuna mahakama ya India iliyoweza kuwatia hatiani wahusika wa QNET wakawa huru.

30. Sura nyingine ya QNET

Tutizame positive side ya QNET na Vijay kwa kiasi;
  • Forbes listed Vijay Eswaran as one of the biggest philanthropy heroes. You can read about that here: 48 Heroes Of Philanthropy
  • It is listed on the World Economic Forum
  • QI Comm is one of the fastest growing tech companies in the United Kingdom.
QNET inaendesha biashara zake kwa mfumo wa Multi-level marketing ambao unatumika sana na pyramid scheme nyingi kama d09 iliyokufa hivi karibuni na zingine.
Multi-level_marketing_tree_diagram.png


Kinachofanya usione kama ni pyramid scheme wanatumia kivuli cha bidhaa na vitu wanavyomiliki ili kuficha uhalisia wa pyramid scheme (ntaielezea siku nyingine hii).

Utajiuliza kwa nini haifungiwi sehemu nyingi duniani mpaka kutokee majanga ???
Ni kwa sababu sehemu nyingi duniani nchi nyingi hazina sheria inayosimamia multi level marketing na operations zake pamoja na direct selling kama ilivyotokea nchini India kweli mnaona kuna uovu unatokea watu wanarun business kinyume kabisa na mipango ya nchi lakini mnawatia nguvuni na kuwashtaki kwa sheria ipi ? Hii imefanya hawa jamaa kuendelea kupeta nchi nyingi ikiwemo na hapa kwetu na ndio maana hujasikia mtu kakamatwa kwa kupotea na pesa za d09 hata hii QNET itakuja kuishia hewani tu kama mvuke........(haya ni maoni yangu)

Mfumo wa Forever Living au Oriflame ni tofauti sana na mfumo wanaotumia hawa QNET as network market na hicho ndio kinachofanya kue na doubt nchi nyingi inakoingia na kuanza ku operate.

Niwakumbushe wanaotamani kuingia huku usiwekeze kiasi kikubwa cha pesa ambacho hutamudu kukipoteza namaanisha don't invest amount of money that you couldnt afford to loose it,that is risk management.....hata siku unaambiwa ime collapse au imefungiwa nchini kwetu hutaumia kwa ile pesa ulikua umeweka kule utaumia kwa mda ulio poteza ungeweza kufanya uwekezaji mwingine wenye tija.

Kwa wafanya biashara nafikiri ukiweza ku adopt hii system ya mult level marketing (kumfanya mtu awe part ya uwekezaji wako au part ya biashara yako na si kumuajiri) ni mfumo mzuri sana.

Kwa TRA kuna mirija ya upotevu wa pesa hasa kwa shughuli kama hizi niliwahi hata kuuliza hivi google,facebook si wanarusha matangazo yao online wanalipa kodi ? sheria zinasemaje ?

Ntaishia hapa kwa leo ntaendelea kukuletea zaidi na zaidi kwa kadri ntavyoibua haya mambo.
 
Naomba kujuzwa sawia kuhusu hii kampuni (networking bussiness company) ijulikanayo lwa jina la Qnet.

Nimefuatilia kiingilio chao ni kuanzia milioni 4. Kisha ili upate commission inabidi uingize watu wawili wenye uwezo wa kutoa hizo 4m kila mmoja. Na wao wakiingia wawaingize watu wawili kila mmoja kwa gharama hiyo au zaidi. Kila watu wanavyoingia ndivyo waliotangulia wanavyopata commission.

Hiyo 4milion ni kiwango cha chini na hutolewa kununua moja ya product za kampuni hiyo kama saaa, mikufu, na hereni.

Inasemekana ukijiunga, unaweza kuwa bilionea ndani ya mwaka mmoja. Naomba ufafanuzi ama ushuhuda juu ya hili.
 
Umetumwa kuja kufanya marketing huku au uko about kupigwa na upatu wa kisasa?
Hapana mkuu sijatumwa. Ila ni kwamba imeniumiza sana. Wife aliingia kwa siri bila mimi kujua. Baada ya movement zake nyingi kuwa sizielewi ndipo akaniambia ana biashara.

Nikataka kuijua akasema hawaruhusiwi kumwambia mtu. Ukitaka mpaka uende mwenyewe.

Basi nikajikongoja mpaka kule. Mafundisho yao hayakuniigia akilini. Ikabidi nikasome vizuri. Nikakutana na tegatives na positives.

Mashuhuda wengine wakaniambia ile kitu ni kama wanatumia mpaka ushirikina. Ndoa nyingi zinavunjika kwasababu mwanamke akiingia kule anabadilika tabia na kuwa wa ajabu sana.

Na kweli nilishaona hizo tabia kwa mke wangu. Ukigusia kampuni hiyo hata kwa kumshauri tu anakuwa mkali sana.

Mara jana kwenye profile picture yake kaweka gari ya mwalimu wake ambaye ndiye boss wake. Nilipomuuliza sababu ugomvi mkubwa ukazuka. Na akaapa kuwa haiondoi.

Tangu mwanzo nilishajua kuna tatizo akanibishia. Hata hiyo milioni 5 aliyojiungia huko sijui alikoitoa. Na nikimuuliza inakuwa balaa
 
Mimi nisingeogopa hiyo risk na hasa kwakuwa tayari wife alishalipa hiyo fedha. Tatizo ni huo uchizi aliopata na mpaka kuamua kuharibu family. Na tulionywa mapema. Inaniuma sana.

Naogopa hata kubeba silaha kwa ulinzi wangu maana naweza itumia ghafla. Nimejenga family yangu kwa taabu for years, sasa nasty things kama hizi zinakuja kuniharibia.
 
Hapana mkuu sijatumwa. Ila ni kwamba imeniumiza sana. Wife aliingia kwa siri bila mimi kujua. Baada ya movement zake nyingi kuwa sizielewi ndipo akaniambia ana biashara.

Nikataka kuijua akasema hawaruhusiwi kumwambia mtu. Ukitaka mpaka uende mwenyewe.
I see.............. hata mie nilipoulizia niliambiwa mpaka niende mwenyewe kwenye mkutano wao. Bora nlivyosita.
 
Back
Top Bottom