Anayefahamu hii namba ya simu +4915145132077anijuze

Namba hiyo imenitumia ujumbe(text message) hii:- Your Mobile no.has won you £750,000 pound in Nokia UK PROMO. For claims send your name,address,mobile no. and occupation to Email:- nokiaconnect106@live.co.uk.

Kwa kifupi ni Namba yangu ya simu imeshinda paundi 750,000.katika promosheni ya Nokia ya Uingereza na wanataka niwatumie namba yangu ya simu, anawani yangu na kazi ninayofanya kwenye email hapo juu.

Sasa naomba humu JF kama kuna aliyewahi kupata huu ujumbe kwani katika eneo langu kuna mtu mwingine aliyetumiwa ila tofauti ni iPhone UK PROMO na email ni appleconnect.

Na hiyo code namba ni ya nchi gani? Ninamashaka yawezekana ni matapeli kwani hakuna droo niliyocheza.

1. Ulishawahi Kushiriki?
2. Kama wamekutumia text ina maana namba yako wanaifahamu sasa wanaitaka tena ya nini?
 
achana nao matapeli, ,mi mwenyewe wamenitumia leo alfajiri kwa kutumia no 44 703-3595-5685 na nokia-verificational@hotmail.co.uk . matapeli hao ntashindaje kitu sijawahi kushiriki??
wapuuze tu hao watapeli wa mtandao halafu bado washamba kwani huo utapeli ushapitwa na wakati, hawana hata mbinu mpya...lol...bongo zao zimekaa kimdondomdondo....
 
Back
Top Bottom