Anayedaiwa msimamizi wa mali za mke wa Balali ashtakiwa kwa utakatishaji fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Dar es Salaam. Elizabeth Balali (54), mfanyabiashara mkazi wa Boko Magengeni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, amesomewa mashtaka hayo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wankyo amedai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge.

Anadaiwa kumuuzia eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo amedai katika kipindi hicho mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Naye Wankyo alieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24, 2019 itakapotajwa tena, mshtakiwa kupelekwa rumande.

-Mwananchi-
 
Huyu anaweza kukiri na kusamehewa fasta. Atumie fursa iliyopo ili kujinasua na balaa!
 
Ndugu zangu hili swala la uhujumu uchumi nadhani sasa ni kwa ajili ya kukomoa watu tu basi. angalia kesi kama hii yaani mtu unakosaje dhamana wakati swala ni hilo dogo tu halafu thamani ya fedha ni 25 mn tu.
 
Naomba kuelimishwa kidogooo,hivi mtu akimuuzia mwenzie kiwanja ambacho sio chake,hii inaingiaje kwenye uhujumu uchumi?hiyo di utapeli?
Wajuvi was sheria mnisaidie,Maana MTAANI haya mambo yapo Sana.
Utapeli ni utakatishaji wa fedha Money laundry
unapewa pesa upeleke FAT kwa ajili ya michezo unazichepusha na kuzalisha faida hapo ni UTAKATISHAJI (uhujumu)
unadai unaweza kufua umeme kwa mitambo yako kumbe unazima mingine ili wewe ulipwe zaidi kilichozidi ni kutuhujum
 
Hyu balali Ana jumba moja linangalia ufukwe mmja bahari ya hindi
Basi ndg upande wa mwanaume wanakwenda mbio kutaka kuliuza wanataka kumzidi mke wa marehemu
Sahv Ukienda pale nje Kuna mabaunsa full time

Ova
 
Dar es Salaam. Elizabeth Balali (54), mfanyabiashara mkazi wa Boko Magengeni amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh25 milioni kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo anayedaiwa kuwa msimamizi wa mali za mke wa gavana wa zamani wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Balali, amesomewa mashtaka hayo leo Alhamisi Oktoba 10, 2019 na wakili Wankyo Simon mbele ya hakimu mfawidhi, Kelvin Mhina.

Wankyo amedai kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia Sh25 milioni kwa ulaghai kutoka kwa Dk Roderick Kisenge.

Anadaiwa kumuuzia eneo la mita 900 ambalo halijapimwa lililopo Boko Dovya wilayani Kinondoni wakati akijua si lake.

Katika shtaka la utakatishaji fedha, Wankyo amedai katika kipindi hicho mshtakiwa alipokea Sh25 milioni kutoka kwa Dk Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Elizabeth hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza makosa ya uhujumu uchumi.

Hakimu Mhina katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 109/2019 alimueleza mshtakiwa huyo kuwa licha ya mahakama kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza, pia shtaka la utakatishaji wa fedha halina dhamana.

Naye Wankyo alieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 24, 2019 itakapotajwa tena, mshtakiwa kupelekwa rumande.

-Mwananchi-
[/QUOTE
aandike barua kwa DDP aombe msamaha, alipe pesa yaishe.

aandike barua kwa DPP aombe msamaha alipe deni yaishe.
 
naona ndio njia aliyotumia Mdai Dr Roderick Kisenge maana hizo 25m asingezipata, na huyu Mdada sio mrithi wa mali za Balali sasa sijui atauza nini ajiokoe
 
Utapeli ni utakatishaji wa fedha Money laundry
unapewa pesa upeleke FAT kwa ajili ya michezo unazichepusha na kuzalisha faida hapo ni UTAKATISHAJI (uhujumu)
unadai unaweza kufua umeme kwa mitambo yako kumbe unazima mingine ili wewe ulipwe zaidi kilichozidi ni kutuhujum

Nimekusome nimejaribu kukuelewa ila vimekataa.. utapeli ni utakatishaji fedha?
 
sawa lkn kwanini kwa Manji, Wambura, Rugemalila, Kaburu nk
siku hizi usijipatie zaidi ya 10m utazielezea wakishindwa utalipia Kodi
fuatilia
 
kesi za utapeli kwasasa zinaitwa 'kutakatisha fedha' na 'uhujumu uchumi', history will judge JPM harshly
Hata wangebadilisha sheria matapeli wakipatikana na hatia wafungwe miaka 30 ingekuwa sawa tu. Huwa sioni tofauti kati ya tapeli na jambazi. Cha muhimu ni kuwa watuhumiwa wasiwekwe ndani kwa muda mrefu bila dhamana na kesi ziharakishwe.
 
tapeli anataka fedha zako lakini hana mpango wa kukuua, jambazi anataka fedha zako na uhai wako ikibidi.
 
Nimekusome nimejaribu kukuelewa ila vimekataa.. utapeli ni utakatishaji fedha?
Kutakatisha. Kufanya kitu kuwa kisafi

Unapata fedha kwa njia isiyo halali. Wizi,utapeli,kukwepa kodi,kudhulumu,kuuza madawa ya kulevya.

Fedha uliyoipata unaenda kuitumia kununua vitu halali. Mpaka hapo unanunua Mali halali kwa kutumia fedha zisizo halali. Kwa kiingereza inaitwa money loundering. Laundry ni sehemu wanapofulia nguo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom