Anayebeza mgomo wa madaktari ni sawa na mtu asiye na maono ya hatima ya nchi hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayebeza mgomo wa madaktari ni sawa na mtu asiye na maono ya hatima ya nchi hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by luckman, Jul 9, 2012.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa nikafatilia watu mbalimbali wakitoa maoni juu ya mgomo wa madaktari, ni maoni mazuri yenye kuleta changamoto za hapa na pale, vilevile ni maoni yanayoonesha sura tatu tofauti kama ifuatavyo!

  1. sura ya kwanaza ni watu wanaotoa maoni hali hawajui hii picha ikoje, wanaongea kama wananchi pamoja na kuguswa kwao juu ya watanzania wenzao wanaopotea bila hatia, wanaguswa hata mimi naguswa lakini siwezi kutoa maoni yangu kwa sasa hadi mwisho wa hii makala,
  2. sura ya pili ni upande wa madaktari ambao wanagoma na wanajua kwa nini wanagoma, wana haki za msigi juu ya kugoma kwao, wana haki za msingi juu ya kuboreshewa mazingira ya kazi ili waifanye kazi yao kwa amani na usalama, wana moyo na huruma juu ya watanzania kwani ndo kazi wameisomea lakini wanahukumiwa na watanzanioa wenyewe amabao hawajui hasa mantiki ya kugoma kwao
  3. sura tatu ni serikali ambayo inajua fika kuwa madai ya madaktari ni ya msingi ila wanafake uma ili madaktari waonekane ni wauaji, watu wasio na huruma, watu wasiojua maadili ya udaktari, lengo ni kuminya haki zao na kugeuza swala hili as a political gain! nawawaambia no, hilo halikubaliki hata siku moja!

  Baada ya kuongelea hizi si=ula naomba sasa nidodose kidogo juu ya baadhi ya madai ya madaktari

  Sio rahisi kuamini yanayotokea na kusemwa ni maneno yanayotoka kwenye midomo ya viongozi waandamizi wa serikali, hapana nakataa! hivi kweli tunashindwa kuelewa hata kwa picha kuwa madaktari wanawatakia watanzania mema? kunahaja ya kudanganya uma na kuwatishia kisa unamiliki dola? je wanataka nini?

  1. Kuboreshewa mazingira ya kazi kwani kumekuwepo na mtiririko wa matukio kwa madaktari kuambukizwa magonjwa yasiyo yao wakati wanawahudumia wagonjwa! hilo hakuna anayeliona,
  2. Wanataka waboreshea malipo! iweje serikali unatenga shs 10,000 kama oncall allawance? hivi nikiwa nipo kimara unanipigia simu saa nane nakuja kwa usafiri wangu then unanilipa shs 10,000? kweli hali wabunge wanalipwa?.......
  3. wanataka wakopeshwe magari kwa dhamana ya serikali ili wakati wanalipa deni walipe with no interest, iweje serikali haitaki juu ya hili hali kwa wabunge haina mjadala? kwani wanataka kuufanya huu mkopo kuwa commercial loan? au hawa sio watu!
  yapo mengo sana amabyo watu hawayajui sema kila mtu anachangia kulingana na uelewa wake juu ya hili jambo?

  look here! Viongozi wa serikali yani mawaziri wastaafu na maraisi wametengewa shs 8bilion hali hospitali tano za serikali za rufaa zimetengewa 6 bilion! je nani ana huruma? fikiria juu ya hili na useme mwenyewe, hali hii kweli inatia hamasa kwa wafanyakazi wengine> gap la mishahara litatugawa kama hatutaangalia, kuna watu wanataka kuifanya hii nchi ni ya kwao, kodi za wananchi wanazigawa kama wanavyotaka wenyewe na si kufanya mambo yanatoa manufaa kwa wananchi wenyewe! NAWASII SANA SERIKALI, KILA MNACHOFANYA MJUE KINAWAFIKIA WANANCHI MOJA KWAMOJA! KWANI USALAMA WA TAIFA HAUPO! UMEGAWANYIKA KUTOKANA NA SERIKALI KUWA LEGELEGE! MJUE NJIA PEKEE YA KULETA UTULIVU NA KUONDOA MANUNGUNIKO NINKUFANYA YALE YANAYODAIWA NA WANANCHI NAWAFANYAKAZI WAKE NA SI KUUA WATU!UKIMUU ULIMBOKA, UJUE WATAIBUKA ULIMBOKA WENGINE TANO!
   
Loading...