Anayebeza haya maendeleo basi hana nia njema na nchi yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayebeza haya maendeleo basi hana nia njema na nchi yetu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Annael, Sep 24, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  Kwa hakika nchi yetu imeanza kujikwamua tena kwa kasi sasa. Nataraji mda si mrefu nchi yetu itakuwa na maendeleo makubwa.
  Nimekuwa nikijionea kwa macho yangu jinsi miradi mbalimbali hapa nchini inavyoenda kwa kasi. Hii ni dalili tosha kabisa kwamba viongozi wetu wameamka kutoka katika usingizi waliokuwa nao.

  Nitajaribu kutaja baadthi ya miradi inayoendelea hapa nchini na italeta chachu kubwa sana ya maendeleo.

  1. Ujenzi wa Hospitali ya kimataifa: Huu ni mradi ambao tayari umekwisha kuanza. Hospitali hiyo itajengwa maeneo ya kisarawe ambayo itakuwa na kiwanja cha ndege. vilevile kutakuwepo na chuo cha madaktari, wauguzi na wafamasia. Hospitali hiyo itarajiwa kumalizika mwaka 2014.

  2. Ujenzi wa daraja la kigamboni: Huu mradi tayari umeshafunguliwa na tayari sasa daraja kwaajiri ya kuwasaidia wajenzi limeshawekwa. ni matumaini yangu mda si mrefu ujenzi wa daraja hilo utaanza.

  3. Mabasi yaendayo kwa kasi: Katika kutatua tatiza la foleni kwa wenyeji wa dar es salaam nadhani wanajionea wenyewe jinsi shughuli za ujenzi wa njia za mabasi yaendayo kwa kasi inavyo enda kwa kasi.

  4. Upanuzi wa barabara mbalimbali: Kila mmoja mwenye macho anaona jinsi miradi ya ujenzi na upanuzi wa barabara zetu unavyo enda kwa kasi.

  5. Kupitiwa kwa mikataba mbalimbali: Mikataba mbalimbali ambayo ni mibovu inapitiwa na kurekebishwa. Mikataba ya madini na na mingine mingi tu.

  6. Kuwa na umeme wa kudumu: Ujenzi wa bomba la gesi abao kwa uhakika utaondoa kabisa tatizo la umeme nchini.

  7. Reli ya tazara: Ukarabati wa reli ya tazara utarahisisha usafiri wa watu waendao kusini mwa tanzania tayari sasa serikali ya Tanzania, Zambia na China wameshaanza utaratibu wa kuikarabati reli hiyo.


  Kwa hayo machache tu na mengine yapo mengi. Hii ni dalili tosha kabisa nchi yetu inapiga hatua kwa kasi.
  Tutambue kuwa kuna nchi hawataki kuona nchi yetu ikiendelea maana itakapoendelea watakuwa hawana chao kwetu.

  Kwahiyo anayebeza maendeleo haya basi hana nia njema na nchi yetu.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  umesahau na uwanja wa NMC kufanywa soko....ni maendeleo pia......
   
 3. B

  Bona_Fide Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Umesaau safari za kila kukicha za jk pia ni maendeleo!
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Annael Mbona maendeleo yenyewe umeyaorodheshea kwenye toilet paper!!!! mbona una mazarau namna hii mkuu!!! Kwani tumekukosea nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. B

  Bona_Fide Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Umeme wakudumu usije ukasema ukiwa Arusha, utaweza kupigwa na mayai viza!
   
 6. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  Dada yangu sijui wewe ni mkimbizi au vipi? naomba uniambie
   
 7. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  Kaka kwa kweli sijakuelewa mimi nimesema ninacho kiona kwa macho yangu. Na toilet peper sijajua una maana gani.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Annael, kinachoangaliwa hapa sio final product on its own, bali what took us to get there. Kwa rasilimali tulizonazo, na ukubwa na deni la taifa, tulitakiwa tuwe mbali kabisa na sio hivyo viji miradi ya kuku.

  Daraja la Kigamboni kama umegundua ni tofauti na ilivyokuwa imepangwa. They've gone for a very cheaper daraja. Ukija kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi, kama kumbukumbu zangu ni sahihi mwaka jana tulioneshwa aina ya mabasi yatakayotumika - ni viji-bus vya TATA - daladala like. Sielewi kwanini hawakufikiria kuweka 'Trams'?

  Hela zipo (Swiss) na bado tunaendelea kukopa. For what? Kukarabative Locomotive Trains kwenda Kigoma?

  Kuzuru TAZARA, Tanzania tunachangia kiasi gani kukarabati? Another humialiation, baada ya miaka yote bado tumeenda kuwaangukia wachina watusaidie kuikarabati! Na hiyo hospitali ya kimataifa unasema inajengwa, unajua nani anafadhili huo ujenzi, na amepata nini in return?
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Dada Annael, kumsifu mumeo kwa kuleta kilo ya nyama kwa kitoweo cha familia yako ni kutoka chooni na toilet paper iliyotumika. Kwa akili ya aina yako ni rahisi kupendekeza tumpe musuguri reli ya kati kwa kusaidia ushindi dhidi ya iddi amini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,664
  Likes Received: 2,126
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa! Hata sisi Mbeya tunaona maendeleo kama vile kusimama kwa ujenzi wa barabara ya Mbeya-Chunya, kusimama kwa ujenzi Wa umanja wa ndege Songwe. Kusuasua ujenzi wa Soko la kimataifa la Mwanjelwa, kusimama kwa Mgodi wa kiwira na umeme wa mgao. Anaebeza haya si mtz.
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hivi swala la kigoma kuwa kama dubai bado liko kwenye mpango?
   
 12. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Unazungumzia MIRADI ambayo ingine iko katika makaratasi tangu uhuru tena wanafanyia amendments coz badala ya kupanua barabara documents za enzi za uhuru zina FlyOverz, leo tunapanua na kuleta miradi ya kuuza mabasi mwendokasi. Hilo number 1 hebu njoo na data stahiki coz napata ugumu kulielea kama walishindwa kuendeleza Hospitali ya magonjwa ya Moyo hapo ni kuokota embe Jangwani.

  ITUMBILI LIKAZWALAGA NG'WENDA, LAMANELA KIKUBHAKUBHA- Tumbili havai nguo, kazoeka kifua wazi.
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Preta huyu mutu anatia hasira sana, wajibu huu umetekelezwa kwa misaada, sasa kuna la kujivunia kutekeleza wajibu kwa kusaidiwa, kwa kweli na maupungufu ya hizi nguvu za kiume, dada jiandaeni sisimwewe wanaweza kuomba msaada wa kuwajawazito "kwa msaada wa watu wa marekani"
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,345
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  Rekebisho mimi sio dada ni kaka. Halafu sijaongelea reli ya kati nimeongelea reli ta TANZARA sawa mtu wangu?
   
 15. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  mkimbizi!!!.......what an insult.......
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nisamehe kwa kosa langu la kiitifaki.
  ISOMEKE KAKA NILIPOANDIKA DADA.
  samahani kwa usumbufu unaojitokeza.
   
 17. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wasiolipa kodi utawaona tu... Hata haki yako inayotokana na kodi unalipa kila siku unadhani ni fadhila za mkwerre,,, Hata hayo unayodhania maendeleo yamechelewa sana kuja, yamekuja wakati walipa kodi wa ukweli tunataka hiki chama kiondolewe kwa kupitia sanduku la kura na kazi ya kusimamia kodi zetu kwa maendeleo yetu kipewe chama kingine, hasa CDM.
   
 18. d

  dotto JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HAwa jamaa wanacheza na pesa zetu za mifuko ya jamii halafu wanasema wameleta maendeleo. Kila kukicha safari za nje ambazo hazina tija. na yule mzee misifa- magufull anahamasisha vasco akaze uzi kusafiri.
   
 19. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  maendeleo mazuri yanaitwa kwa kizungu 'organic growth' and sustainable.
  Haya unayoyaongelea wewe ni yale ya kuonekana machoni kwa watu. Mfano unavyosema hospitali Kisarawe iwe na uwanja wa ndege hiyo ndege anapanda nani maana hata pesa ya kununulia chakula acha dawa watu hatuna!
  Kwa kifupi ni kwamba kila maendeleo tunayoyaona kwa sasa ni kigogo sana kulinganisha na mikopo inayoyafanya (deni la taifa) ambayo inafikia Trillion 18?? na kila mtanzania kudaiwa 500,000/- huku budget ya nchi ikiwa ndogo zaidi ya hilo deni.
  Tulizoea umasikini wetu wa mali lakini naona umasikini wa fikra unatunyemelea kwa kasi ya ajabu.

   
 20. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160

  Safari za JK pia ni maendeleo ya kutobezwa maana duniani hakuna Rais mzururaji kama JK, amevunja record iloyowekwa na Henry Kissinger kwenda mashariki ya kati enzi zile.
   
Loading...