Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Sitaki kuamini na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa kuna vita ya kweli inaendelea kuhusu kinachoitwa kupambana na madawa ya kulevya bali nahisi kuna jambo nyuma ya zoezi hii.
Maswali ya kujiuliza kama kweli kuna dhamira ya dhati ya kupambana na hii biashara.
1.Unaweza kweli kuanika hadharani majina ya watu unaowatuhumu kabla hujawakamata /hujawafanyia uchunguzi?
2.Wakitoroka au kuharibu ushahidi sio wewe ulietangaza ndio utakuwa umewapa nafasi na muda wa kuharibu ushahidi au kutoroka?
3.Unawezaja kuanika hadharani majina ya watu unaotaka wakupe taarifa za kiuchunguzi?
3.Nani atakuwa tayari kutoa taarifa wakati umeshamuanika hadharani?
4.Huku si kuhatarisha maisha ya watu unaotaka wakupe taarifa?
5.Kama kweli uko serious,unaendaje kum-search mtu ambae tayari anajua leo au kesho atakuja kukaguliwa nyumbani kwake na isitoshe tayari ameshaona waliotangazwa kabla yake wamekaguliwa?
6.Unapoenda kum-search mtu kama huyo,unatarajia yeye awe mjinga kiasi gani asifiche au kuharibu ushahidi?
7.Mwisho wa zoezi hili si itakuwa tu ni kusafisha baadhi ya watuhumiwa(kwa kukosekana ushahidi)huku wengine wakichafuliwa?
Nina mashaka sana na zoezi hili zima na mwenendo wake.