Anatarajia ndoa, ila mimi siitaji japo nampenda.. Nimchomolee vipi?

Wadau nina msichana nampenda sana na yeye ananipenda zaidi.

Ishu ni kwamba mapenzi yamekolea kiasi kwamba yamevuka matarajio yangu, mimi nilikuwa namchukulia kama msichana wa kula nae maisha tu huku tunakuwa.

Ila mwenzangu amekolea sana sana kiasi ameshanitambulisha kwa kila mtu wake wa karibu mpaka mama yake. Ameweka picha yangu kwenye kila account yake fb na insta ata Watsapp ameniweka dp.

Sasa wadau nachoomba mnishauri ni jinsi ya kuondoa hii hali kwake bila kuachana, nataka asiwe na mategemeo ya ndoa maana kwa marafiki zake na ndugu zake ni mchumba tayari japo sijawai mtamkia ilo.

Nimwambie nini bila kumkwaza na kuachana aelewe kwamba mupenzi yetu ni ya kupita tu.

Sababu kubwa ya kumuondoa kwenye future yangu ni tabia naona hatuendani mimi nimekuwa mtu wa kumvumilia kila siku, nahisi sababu ya malezi na mazingira ya makuzi hivyo naamuaga nimuelewe tu .

Kingine yeye akumaliza ata form four mimi nna elimu ya chuo hivyo tunakua na gap fulani kwenye maamuzi maongezi ata priorities za kimaisha.

Kuna kipindi nataka kumwacha ila namuonea huruma sababu alivyo kolea, na nikiendelea nae anazidi kudata na anategemea ndoa ndio inanukia.

Nishaurini nimweleshe vipi bila kugombana ata tukigombana tusiwe maadui tuwe marafiki wa kawaida , maana sitaki aondoke kwenye maisha yangu japo siitaji kumuoa.
Maepenz ya kwel hayaangalii elimu ila kuliko kumpotezea muda boraw umwambie ukweli pengine wapo wenye malengo nae anawakataa kwa ajili yako ila pia utakuja mpata aliyefika chuo na nn na utasumbuka na pia wadada msikurupuke kumweka mpenz, boyfriend ,mchumba wasap cjui facebuku, histagram acheni mana wanaume wanajua kuigiza anaweza kukuandalia mazingira kua anafuture na ww kumbe anaitaji kupunguza uzito kiunon, ni vizur kumweka mume mana ata hao wachumba hua wanakimbia, pole yake Mdada ,anajua kapata mume Wa chuo, sa iv shule Nayo naona nikigezo chakuoa au kuolewa
 
Chuo chenyewe utakuta tumaini af unasomea education. Acha dharau kwa mdada wa watu
 
Hivi kwani mwenye ELIMU ya CHUO KIKUU...kuoa mwanamke ambaye hajamalizs ELIMU YA O LEVEL.... pia ni KIKWAZO?hivi ktk MAPENZI ya kweli elimu inahusikaje?inaonyesha WEWE humpendi huyo msichana..sasa... Dawa yake..njoo inbox nipe no ya huyo msichana wako..niwaachanishe...ili uwe free... umtafute wa CHUO MWENZIO.. mtaendana tu...
 
Si uachane nae tu!!! Usimpotezee mda dada wa watu! Utakuja muumiza zaidi ya hapo
 
Chuo chenyewe utakuta tumaini af unasomea education. Acha dharau kwa mdada wa watu
Mbona mkuu na wewe umedharau chuo cha watu na taaluma za watu?
Kama ni dharau na wewe unayo ila sema mmetofautiana vitu vya kudharau!

Ila huyu ndugu yetu atakipata kile anachokitafuta kama kweli anamuonea huyu mwanamke! Lakini basi akumbuke malipo ni hapa hapa duniani asije kudhania ana hadhi sana kiasi cha kuwa amefikia kwenye kilele cha ubora! Pia aelewe kuwa anapoishia yeye kuna wengine ndio wanaanzia hapo hivyo asidharau wale ambao hawakujaliwa kupata kile yeye alichojaaliwa!
Muhimu tu amwombe Mungu aweze kumsaidia kufanya maamuzi sahihi na ya haki vinginevyo atakuja kulia machozi ambayo hatokuja kupata mtu wa kumpangusa!
 
My killer technique ninayotumiaga kwa ving'ang'anizi ni hii, mwambie kuna binti umempa mimba ivo kwa sasa utakua nae bize kuhakikisha mimba na mtoto inakua. Hii mbinu haijawahi niangusha.
 
umenichekesha ulivyosema kuwa, hutaki kumuoa pia hutaki aondoke kwenye maisha yako.
chagua moja kumuoa ili abakie maishani mwako au kumuacha aende na umfute maishani mwako.
 
Ananipenda sana lakini kuishi nae ndio roho imekataa, kuna vitu naona vitanitesa Mimi.
Sikwambii muowe na wala sitosema usiowe, nakuelewa sana juu ya vitu unahisi vitakutesa. Kwenye ndoa kuna changamoto nyingi sana lazima uzikabili kama unavyo yakabili maisha ya kawaida.
 
Mwambie tu kuwa umejitathmini mwenyewe kwa tabia zako za Kitukutu ulizonazo umeona hutamfaa na kama akizidi kukung'ang'ania kutaka kuolewa na Wewe mtishie kwa kumwambia kuwa una rekodi mbaya za Kiuhalifu na kwamba hivi sasa unajuta kumpoteza Ben Saanane, kisha unajuta kumtesa Roma Mkatoliki na hivi majuzi tu ulikuwepo katika tukio baya la Kibiti hivyo kama atavumilia basi Mkuu huyo atakuwa ni halali yako kutoka kwa Maulana ila nina uhakika kwa huo mkwara ukimpa nadhani hapo mtakapokuwa mmekaa Watu wanaweza kudhani Mwanariadha Usain Bolt amekuja kufanya mazoezi yake ya maandalizi ya Olympic kwa jinsi atakavyotimua mbio kwa kuogopa kuwa pengine na yeye asije kuwa the NEXT.
duuuuuu nimejikuta nacheka kwasauti japo usiku wa manane
 
Ss huo ndio inafki wenyew km mtu unampenda why usimuoe ama mackini na ww unatka ukaoe tajiri?
 
Utajisikiaje kama ukigundua naye anamawazo kama yako...na ikitokea akakuwahi kufanya maamuzi na kukuacha itakuwaje...kuwa makini na unachokiwaza na kukitamani.
Mtenda akitendwa hujivika nafasi ya kusalitiwa na kuonewa.
 
Vunja ukimya mueleze dada wawatu huna future nae...

Tena mueleze leo hii akae akijua asiendelee kupoteza muda wake kwako
 
Wadau nina msichana nampenda sana na yeye ananipenda zaidi.

Ishu ni kwamba mapenzi yamekolea kiasi kwamba yamevuka matarajio yangu, mimi nilikuwa namchukulia kama msichana wa kula nae maisha tu huku tunakuwa.

Ila mwenzangu amekolea sana sana kiasi ameshanitambulisha kwa kila mtu wake wa karibu mpaka mama yake. Ameweka picha yangu kwenye kila account yake fb na insta ata Watsapp ameniweka dp.

Sasa wadau nachoomba mnishauri ni jinsi ya kuondoa hii hali kwake bila kuachana, nataka asiwe na mategemeo ya ndoa maana kwa marafiki zake na ndugu zake ni mchumba tayari japo sijawai mtamkia ilo.

Nimwambie nini bila kumkwaza na kuachana aelewe kwamba mupenzi yetu ni ya kupita tu.

Sababu kubwa ya kumuondoa kwenye future yangu ni tabia naona hatuendani mimi nimekuwa mtu wa kumvumilia kila siku, nahisi sababu ya malezi na mazingira ya makuzi hivyo naamuaga nimuelewe tu .

Kingine yeye akumaliza ata form four mimi nna elimu ya chuo hivyo tunakua na gap fulani kwenye maamuzi maongezi ata priorities za kimaisha.

Kuna kipindi nataka kumwacha ila namuonea huruma sababu alivyo kolea, na nikiendelea nae anazidi kudata na anategemea ndoa ndio inanukia.

Nishaurini nimweleshe vipi bila kugombana ata tukigombana tusiwe maadui tuwe marafiki wa kawaida , maana sitaki aondoke kwenye maisha yangu japo siitaji kumuoa.
Mbona njia ya kuachana ni rahisi sana kata mawasiliano nae tu ila jiandae kuopoa garasa.
 
Naona watu mmeamia kwenye kumuonea huruma msichana. Ata mimi namhurumia ndio maana nikaomba ushauri hapa . Kiukweli moyo umekataa na sitaki kuishi kwa regrets hiyo ndoa itakuwa na matatizo kwa maono yangu
Hiyo hali huwa inatokea....mi nadhan huna experience na hawa viumbe, yeye kukupenda leo siyo guarantee ya kukupenda kesho...hata usipomuumiza siyo guarantee ya wewe kutoumizwa..fanya vile moyo wako unakwambia, huruma yako itakuponza kijana!!
 
Back
Top Bottom