Anatamani turudiane, lakini hataki kukiri wala kuongelea kosa alilofanya..NIMFANYEJE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anatamani turudiane, lakini hataki kukiri wala kuongelea kosa alilofanya..NIMFANYEJE?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Uncle Jei Jei, Oct 26, 2011.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Mbarikiwe wote Wana JF! Leo nakuja kwenu kuomba ushauri, natumaini kwa kutumia uzoefu,ujuzi na Upendo mtanipa suruhisho! Nimienzi kama mitatu hivi tulitofautiana na msichana niliyetegemea angekuja kuwa mama wa watoto wangu siku za usoni! Tulidumu takribani miaka mitano kwani tulianza mahusiano tukiwa bado A'level! Kisa cha kutofautiana,mara nyingi nilifuma chatings za mahaba na mwanaume mwingine! Lakin pamoja na hayo hakuacha kuniheshimu! Kilichoniumiza mpaka tukanuniana ni siku moja kabla ya kuachana nilimuomba tutoke out akakubali,lakini cha ajabu mda ulipofika hakupokea simu zangu wala kujibu sms zangu mpaka ilipofika jioni akaniambia alikuwa na mama yake...lakini baada ya kufanya uchunguzi jioni hiyo hiyo(kwani baadae tulionana) niligumdua alitoka na huyo jamaa yake. Hii ni kutokana na sms za siku hiyo tangu wanapanga pa kukutania na msg aliyomshukuru kwa "campani"ya siku hiyo!! Nilipomuuliza hizo sms ni za nani na kwanini aliamua kunidanganya,hakuwa na usemi zaidi ya kutetemeka(nilichukua simu yake ghafla). Mpaka leo anasema nilimsingizia na hataki tuliongelee hilo ila ananilaum tu kuwa nimemuacha kwa sababu nimepata mwingine! Bado nampenda na anaonyesha nia ya kuwa na mimi, ila nahofia atakosa uaminifu ndani ya ndoa! MSAADA WENU PLZ..!
   
 2. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mrudie tu ndivyo walivyo ni dhaifu hao. Ulichopata wewe ni kujua kinachoendelea wengine hapa hatujajua kuna nini kinaendelea na wetu huku.
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Kweli mapenzi ni upofu...afanye nini ujue hataacha kukuchanganya na wenzio? wake up
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  unampenda?
   
 5. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  kweli nakiri ameönyesha dalili mbaya mapema! Ila kumjua ambaye ni msitaarabu na mtulivu ndo kazi!
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hata ukienda kwa mwingine jua nako utakutana na vituko
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Utamjua mstaarabu na mtulivu kwa matendo yake...kama ulivyoyaona ya huyu ulienae.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  umekuwa naye kwa miaka mitano halafu kwa miezi mitatu zinatokea mizengwe!
  Jichunguze isije kuwa na wewe una mapungufu, labda kuna kitu kakosa kwako
  Je, mapenzi yenu yapo kama mlivyo anza zamani?

  Mwanamke kutongozwa kupo hata kama umemweka ndani, ila chakuangalia ni reaction yake
  Mrudiane tu!
   
 9. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,200
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  kweli nakiri ameönyesha dalili mbaya mapema! Ila kumjua ambaye ni msitaarabu na mtulivu ndo kazi!
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama unampenda mwite kaa naye muulize sbb zipi zilimfanya yy kukusaliti na kutoka na mwanamume mwingine,huwezi jua lbd kn usichomridhisha, na akueleze msimamo/ malengo yk juu ya mapenzi yn
   
 11. s

  sawabho JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Uchumba wa muda mrefu kama huo (miaka 5) sio mzuri, humsisimui tena - amekuzoea, ndio maana anakuoana wa kawaida na kuanza kutafuta mwingine anayemsisimua. Kama unampenda mrudie, maana hata kama utamwacha na kumtafuta mwingine mambo yatakuwa hivyo hivyo. Ni afadhali uendelee na huyo uliyemzoea.
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280

  well said mkuu
   
 13. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kinadharia watapinga lakn kiuhalisia ndio ukweli mkuu
   
 14. JICHO LA 3

  JICHO LA 3 JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushathibitisha so unahitaji nn sasa
  mi kwa jibu rahs tu naona upo tayari kushea.
  big up kwa mdada aendelee kukudanganya hivohivo
   
 15. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  nafikiri ni katika kutimiza ile nadaharia yenu ya kutest kama jamaa yupi anaweza,......
   
 16. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,268
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Anaogopa kuzungumzia kwasababu anajua ni kweli na anaona vibaya kukiri kuwa alifanya hayo.. Kwa uzoefu wangu, huyo binti anaona unampenda na uko kwa ajili yake kila mara so kakugeuza tulizo lake pale anapoumia. Mkirudiana na akapata mshefa mwingine atakukimbia tena.

  Haya nilokwambia changanya na yako upate uamuzi. Maneno yangu si sheria
   
 17. m

  muhanga JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  yaelekea bado mnapendana, rudianeni tu kwani hakuna alie msafi hasa ktk mahusiano, kosa moja haliachi mke
   
 18. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kama unampenda mrudie tu,ni bora kichaa uliyemzoea,hujui utakayempata atakuwa na ukichaa wa aina gani,sie wanawake hatuishi vituko japo vinazidiana!
   
 19. 1

  1menARMY Member

  #19
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio wanapendana yeye anampenda lkn mwenzie wala,stuka mapema br anakutumia huyo
   
 20. 1

  1menARMY Member

  #20
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAKOSA MANGAPI NDO YANAACHA?????tutakufa sana na hili gonjwa kwa mitazamo hii
  Kaka hapo hupendwi unazugwa tu so shituka mapema
   
Loading...