Anataka niweke status: 'Nakupenda mume wangu' kwenye WhatsApp, kuna maana yoyote ktk hili?

kamankula

Member
Nov 5, 2016
5
1
Bila shaka wote muwazima wa afya.

Leo imekuwa Siku trick sana kwangu mpenzi wangu ambaye tunaitana mke na mme kwa miaka mitatu sasa. Anataka niweke neno nakupenda mume wangu katika status yangu WhatsApp jambo ambalo limezua mzozo kati yetu.

Mimi sitaki kuweka kwa kuwa yeye so mume wangu bado hatujafunga ndoa wala hatuishi pamoja ila ameniahidi kunioa kama mke wa pili.

Nimekuwa nikimtii na kuwa mwaminifu kwake na kumpa heshima zote kama mume wangu, naenda kwake anakuja kwangu.

Mwezi uliopita tulipanga kufunga ndoa ya bomani nilipogundua hajamwambia mkewe nikaghairi nikitegemea atafanya chochote katika mipango ya ndoa, lakini mpaka sasa hajafanya lolote. Mimi nimetulia namsubili yeye, ila kuweka neno la nakupenda mume wangu ndo nimegoma.

Sijui kama nimekosea ila nimeona itazua maswali kwa ndugu na jamaa zangu huyo mume wake ni yupi? Ingawa ni maisha yangu naweza fanya chochote.
 
Usijali sana we andika nakupenda mpenzi wangu , but,

√√hizi wahtsap status huwa hazimaanishi hasa kile kilicho moyoni unaweza andika lakini hayupo moyoni mwako,, kama huna mchepuko mwengine andika hiyo status
 
Sijaona sababu hapo ya kotokumuweka au unaona afadhali ya ugomvi??? Siku zote umekuwa ukimuheshimu kipi kinakufanya usimuweke mumeo mtarajiwa na ndugu, jamaa na marafiki wamuone na kumjua??? Muweke haraka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom