Anataka nimuoe amechoka uchumba sugu, kimaisha sipo vizuri, naombeni ushauli

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Nina mpenzi wangu huyo ninampenda mno mahusiano yake na Mimi sasa hivi ni miaka mitatu imeshatimia tumefanya Mengi kama wachumba tunaheshimiana mno na Mimi nampenda sana mpz wangu.

Ila changamoto nilionayo hivi sasa mpz wangu amenibadilikia anachotaka ni ndoa amechoka uchumba sugu na Mimi kila siku ananilalamikia huwa anaumia kuona marafiki zake wanaolewa yeye bado mpka mdogo wake kaolewa yeye bado hivyo hili jambo linamuumiza akiri na yeye anafosi ndoa na yeye kanielezea kama nitashidwa kutimiza hili basi ameniomba nimuache afanye maisha yake.

Ukweli ni kwanga upande wangu kimaisha sipo vizuli bado napambana niweke mambo yangu vizuli nijipange vyema ila mwenzangu hanielewi aniona kama ni mbabaishaji japo hali yangu ya kiuchumi anaielewa.

Naombeni ushauli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mueleze hali halisi ilivyo mkiridhiana wote wawili fanyeni ndoa bila sherehe. Kama ni wa Katoliki mnaandikisha ndoa, inatangazwa kwa wiki tatu. Inafungwa asubuhi baada ya misa ya kwanza ni nyinyi na mashahidi wenu tu.

Huko mbele ya maisha Mungu akiwajalia mnafanya sherehe.
 
Kama haupo vizuli kimaisha kaa mbali na mambo ya ndoa jombaa ndoa isije kuwa ndoano vijana wengi ambao walikurupuka kuoa wengi wamejikuta maisha yao yameishia ukweni na familia zao na wengine nyumbani kwao wengine kukimbia familia zao ushauli wangu kwako kaa chini na mpz wako mueleze kinagaubaga hali yako halisia usimfiche Kitu kama anakupenda atakusubilia tuu cha muhimu kwao utambulike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa huleta baraka, wengi walipata mafanikio baada ya ndoa hasa mwenza akiwa muelewa. Baada ya ndoa utanunua chakula mke wako apike, utajikuta pesa uliyokua unatumia bar kula nyama choma ni nyingi kuliko unsyofanyia shopping ya nyumbani.
 
Jaribu kumwacha uone kama hajaileta mwenyewe hadi ndani ndoa akakuambia baadae.
Huyo lengo lake kuu ni ndoa ili aonekane laiti angekuwa anataka kuishi na wewe diku nyingi angeshahamia kwako C Programming, pos
 
Muoe, anajua hali yako Ila anataka umuoe.


Wanawake wa napenda hii ... 'Mke wa"


Alafu acha kuogopa maisha...ukioa utashangaa mambo yanavyonyooka.
 
Nipe mm nimuoe kwa mkataba,mambo yako yakiwa safi unamchukua mkeo.
Kuliko kumuacha akaolewa na mtu atakayetaka kuishi naye milele,mm nataka ndoa ya mkataba!
 
(umuache afanye maisha yake) mkuu unakwama mpaka happo mwache akaolewe anakoona ataolewa haraka oa uone balaa duniani
Anakutaftia sababu huyo....kuna mtu ashamdanganya...!!hapo anasubiri tu useme huwez kuoa kwa mda huo....upande wa pili aseme yes

Sent using Jamii Forums mobile app
Mh m sikushauri chochote ila utakapo muoa utakutana na changamoto nying san.....tafakar

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi nimeona kama nyie wadau mlivyoona.
 
Back
Top Bottom