Anataka kunisaidia kupata kazi.....je nimkubalie? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anataka kunisaidia kupata kazi.....je nimkubalie?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tindikalikali, Jul 21, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Wana Jf habari zenu, kwanza natanguliza shukrani kwa wote wanaoleta na kuchangia mijadala yenye tija kwani imekuwa ikinijenga kila siku. Wadau nilikuwa na "Penpal friend" wa kike, toka nikiwa form.... na yeye alikuwa form...., nakumbuka alijieleza vilivyo jinsi kwao walivyo "familia bora" nami sikumficha nilimweleza ufukara uliokuwa ukiniandama, urafiki uliendelea na "automatically" tukawa wapenzi kipindi nipo A level. Nilifanikiwa kuonana naye nikiwa "first year" , "First time" naonana naye aliniita kwao, ukweli niliouona ni kwamba maisha yao ni bora sana ukilinganisha na ya kwetu/kwangu. Kikubwa nilichoki-note toka kwake ilikuwa ni jeuri na dharau ambavyo vilinichosha kadri siku zilivyokwenda, kuna kipindi alikuwa anadiriki hata kunifokea, ndipo niliposema ya nini malumbano? Niliamua kukaa pembeni, nakumbuka nilibadilisha mpaka namba kuepuka usumbufu wake. Sasa hivi majuzi kafanikiwa kupata namba, kanitafuta na tumeonana. Sera aliyokuja nayo ni kuniwezesha kupata kazi kupitia kwa ndugu zake. Kinachonitatiza ni ujeuri na dharau zake, hivi nikifanikiwa kupata kazi kwa juhudi zake haiwezi kuwa mtego wa kuninasa? Na nikipata alafu nikamkataa hawezi kuleta matatizo? Naomba mawazo yenu kwani ajira nahiitaji ila mapenzi na yeye siyataki!
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,314
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  kwani we hujiamini?
   
 3. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  najiamini, tena siku zote naamini nimezaliwa ili niweze. Bado sijui lengo ni nin hapa
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Muweke wazi kuwa ungependa kupata kazi lakini usingependa kuendeleza mahusiano naye kutokana na sababu utakazoona zinafaa kisha uache aamue mwenyewe kukusaidia ama kutokusaidia.
   
 5. nzedanze

  nzedanze Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unamuona bado hajajirekebisha bac ni bora ukampotezea kabisa...harafu kuhusu kazi wewe unatafuta kazi gani na professional yako ni ipi?
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kazi zenyewe za shida,pata kazi kwanza na kwakuwa unajiamini na umasikini umeshapitia juhudi zako kazini ndio zitakuwa nanga yako na sidhani mwajiri atakubali kukupoteza kwa sababu za kijinga.Juzi kidogo machozi yanitoke niliongea na vijana wawili wanauza duka Kariakoo binti na kijana walioishia kidato cha 4 huwezi amini wanalipwa elfu 30 kwa mwezi,chakula na nauli 1600/- kwasiku,kila jumamosi elfu 5 -jumla haifiki 90.
   
 7. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kamata kwanza kazi saini mkataba, akitaka mapenz mwambie No. Hana la kukufanya ww tayar utakua na mkataba wako.
   
 8. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah mm siamin jaman mtoto wa kile ataletaje dharau? Au ww humbanjui kisawa sawa kunako 6 by 6?!
  Ok ww kuwa mpole kamata kwanza kazi saini mkataba, akitaka mapenz mwambie No. Hana la kukufanya ww tayar utakua na mkataba wako.
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kazi kwanza mkuu. Mkataba wa kazi utasaini na mwajiri, sio yeye. Mengine yatajiset mbele kwa mbele.
   
 10. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kazi inayoingia katika "commerce", kuhusu proffession ni "manunuzi na ugavi"
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  nashukuru, ntazingatia ushaur wako.
   
 12. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kaka hata mimi nilikuwa siamini kama msichana anaweza kunipanda kichwani, lakin kwa huyu sisimuliwi..!
   
 13. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu chuo umemaliza na una degree yako, hebu mkuu itumie elimu hiyo kukabili hilo tatizo mbona simple sana? Elimu uloipata ni kwa ajili ya nini sasa mazee ni pamoja na hayo mambo, solve it mkuu...kama unataka ushauri wa kijiweni kanyaga hiyo mutu yenye dharau na kimbia...kazi utapata tu kama unajiamini...
   
 14. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Kuhusu kazi nakubaliana na wengine wanaosema ichukue.
  Lakini kuhusu uhusiano wenu huoni kuwa anaonyesha dalili za kutubu? Kitendo cha kutafuta mawasiliano yaliyokatika na kukupa offer ya kazi ni sawa na kusema 'samahani kwa kukukwaza'.
  Kwa nini usimpe chance nyingine ili aonyeshe kwa matendo kama kweli amedhamiria kujirekebisha? Akirudia upuuzi wake mpige chini jumla. Sioni kama ni sahihi kumnyima chance nyingine tambua kuwa huenda ni malezi aliyopewa ya kudekezwa na si makusudi yake kukufanyia kiburi.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  mwenyewe unasema yeye hukufokea sasa hili kukuwekea mitego latoka wapi.......................kama njaa yako ni ajira kadunde mzigo yakijia hayo mengine yapangue kulingana na matakwa yako binafsi..........................hakuna kulipizana fadhila zozote zile...................
   
 16. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usiwe mjinga mkuu, fanikisha kwanza la kupata kazi, unajua malezi mengine yanachangia, hizo dharau akiukuletea mpotezee,wewe si utakuwa ushachukua mpunga bwana. Anyway kiselasela ongeza bidii kwenye ubanduaji, hawanaga noma kama unajua kutimba..
   
 17. C

  Chumvi1 Senior Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  fanya kkitu kimoja ndugu yangu ukitafutiwa kazi kupitiwa kwa watu majungu huwa yanakuwa mengi ukikorofishana na yule aliyekutafutia utatafutiwa sababu wewe na kazi utaikosa acha short cut hizo pambana mwenyewe bwana kazi utaipata tu kwa nini ukate tamaa na huyo anataka kutumia kutokuajiriwa kwako kama mtego wa kukunasa ukiingia utakoma atakuzingua sana kwenye mahusiano hata kama kwenye sita kwa sita utapachimba vizuri ila ana tabia mbaya haiwezi kufa kirahisi hiyo.
   
 18. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pole sana mwanadada, mi naomba nitofautiane na walio wengi. Mi nakushauri uachane naye kwa kila kitu pamoja na offa zake, kwani ukikubali akutafutie kazi afu ukamzingua atakuwekea zengwe kazin kwa kuwatumia hao hao ndugu zake hata wakakuharibia future kabisa. Angalia wanaweza kukupa ofa ya kwenda nje ya kituo cha kazi ambapo utalala guest huko wakakufanyia kitu mbaya na wala hutalalama. Wanaume wanatechnic nyingi sana mi nashauri utupilie mbali ofa hii kwani utakuwa mwanzo wa manyanyaso kwenye maisha yako ukizingatia umeishi kwa tabu. Nivema ukapata kazi ya elfu 20 lakini ukaishi na amani ya moyo. Epuka vishawishi epuka tamaa mbaya. Nakutakia mafanikio mema
   
 19. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  nimekuelewa lakini mimi ni mwanaume
   
 20. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Mh asante kwa mawazo mazuri, japo yanazid kunichanganya
   
Loading...