Anataka kujua neno "happy Christmas" kwa kiswahili

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kuna Boss wangu hapa Ofisini, Mjerumani, tangu asubuhi ananisumbua anataka kujua hilo neno kwa kiswahili ili amtumie rafikiye salam za sikukuu ya Christmas kwa kiswahili..........................

Mie nimesahau, hebu nisaidieni fasta, nisije tia aibu kwa kutojua lugha yangu.....LOL
 
Kumbe wengi humu ni VILAZA kama mie...........................LOL
 
Noeli njema yenye furaha

Naungana na Msangafm kwa hilo.

Ila wakati mwingine kiswahili huwa tunapeana tu sikukuu njema, yenye heri na fanaka!

Hii inatokana na kuwa ki mila na utamaduni watanzania tulikuwa hatubaguani ki dini, hivyo basi zote zikawa sikukuu tu, yaani Noeli, Iddi, Pasaka, Maulid, za mashujaa au hata za huu uhuru mchwara tulosherehekea juzi! Sikukuu ya Noeli au Idi Majirani, ndugu, jamaa na marafiki bila kujali dini zao wanajumuika pamoja na kusherehekea pamoja.

Hii ni kama vile kiswahili hakuna "He" na "She" unapomzungumzia au kuelezea mtu (binadamu) kiswahili wote ni sawa na hakuna sababu unapomtaja mzazi, mwalimu, jirani, ndugu nk uelezee jinsia yake kwani havihusiani kabisa. Kama ni mwalimu ni mwalimu tu, mzani ni mzazi tu, meneja ni meneja tu, polisi ni polisi, jirani ni jirani tu nk. hashima haiongezeki au kupungua kwa sababu yeye ni wa kike au kiume! Sherehe za kidini ni vivyo hivyo! Sote tutasherehekea pamoja na majirani, ndugu na marafiki bila kujali wao wasalia msikitini, kanisani au wana dini zao za kale.
 
Nakubaliana nawe kwa falsafa zako.
Lakin maana halisi itabakia pale pale.....ona X-mass mara christmas!.
Maana hata hyo sikukuu yenyewe imekaa kaa tafauti na maana yenyewe.
Changanya na zako!
 
Anataka kujua maana ya HAPPY CHRISTMASS au MERRY CHRISTMASS? mi nimezoea kuona neno merry linatumika badala ya happy.
 
We mtambuzi we koma wewe alaa! Kilaza mwenyewe. Wanaume tulikuwa hatujaamka, sasa ndio tunakamata uzi.

Na huyu aliyesema hakuna neno la kiswahili la Christmas sijui naye kama ni Mtanzania au ndio wale mliokulia 'Mayami' ambao hata kiingereza chenu kimetushinda.

Haya hiyo hapo: Heri ya Noeli

Noeli ndio X-mass
 
1. heri ya noeli ni blessed chrismass ,

2. happy chrismass ni furaha ya noeli kwa kiswahili (au noeli yenye furaha).

3. fanaka ni mafaniklio, kwa hiyo fanaka ya noeli ni sawa na kusema prosperous chismass!
 
Good!!
Linganisha na

1. Book-keeping
Book ni kitabu,
Keeping ni tunzwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom