Baba Erick
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 483
- 75
Habari za leo ndugu zangu kama mnakumbuka kichwa cha habari hapo juu leo nimekutana na wahusika na nimewapa ushauri wenu ila nilitumia njia ya kuchunguza kama ujauzito ni kweli wa rafiki yangu kwa kumdanganya yule msichana kuwa kuna daktari namfahamu ana uwezo wa kuchunguza DNA mtoto akiwa tumboni na nimejitolea kutoa hela kwa ajili hiyo kwa hiyo tukishapata uhakika kwamba mimba ni ya mshikaji atatoa huduma zote za kutunza mimba. Jamani dada wa watu aling'aka ile mbaya na baada ya yote tuligundua mimba ni ya mtu mwingine. So vijana wenzangu tuwe makini na tuepuke ngono zembe. NASHUKURU SANA..