Anataka akasomee Community Development lakini hajui atakuja kuwa nani

Hajui na ameniuliza hata mimi sijui hii kozi kazi zake ni zipi na ataenda kufanya wapi. Sijui akimaliza kozi atakuwa nani (aina gani ya kazi au post). Je, serikalini ina soko hii kozi kwa diploma?

Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Afisa maendeleo ya jamii. Naona hii kazi ipo sana kwa NGO's. Serikalini pia ajira zipo sema wapo wengi mno. In short atakuwa ana-deal na jamii.
 
Atakuwa Afisaa Maendeleo ya Jamii, Chini ya Wizara ya Wanawake jinsia na Watoto, ila Kazi siku hizi Ni Mtambuka sana,unaweza Kusomea kitu flani ukaja Kufanya Kazi Tofauti kutokana na Fursa Unayokutana NAYO.

Haswa kozi za Arts,Sayansi hii kitu pia IPO ila Sio sana ukilinganishwa na Mchepuo wa Sanaa!
Mama maendeleo,Afisa Maendeleo wa Wilaya,Mkoa,nk,huwa hawa watu wapo Halmashauri,Wilayani,mkoani,nk!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi siyo msomi kwahiyo haya mambo siyajui kabisa. Binti wangu ana D ya History, D ya Geography, D ya Kiswahili, D ya English na D ya Civics. D zote kazipata baada ya kurisiti mtihani wake. Sasa anauliza aende akasomee mambo gani ambayo ataweza kupata ajira kwa urahisi serikalini au ikibidi kupangiwa kituo cha kazi mara baada tu ya masomo. Hataki upolisi wala ualimu. Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka leo anategemea kwenda kuajiliwa serikalini?

Kama hajui hiyo course itamsaidiaje sasa na mbeleni aache kabisa!! Naona kuna pesa inaenda kupotea bure...
 
Hatuanzii huko. Tunaanza kwa kujinyumbulisha tunapenda kuwa nani, na ndipo tunatafuta kozi zitakazotufanya tuwe hivyo. Hatuanzi kwa kupenda kozi kwanza.
 
Hajui na ameniuliza hata mimi sijui hii kozi kazi zake ni zipi na ataenda kufanya wapi. Sijui akimaliza kozi atakuwa nani (aina gani ya kazi au post). Je, serikalini ina soko hii kozi kwa diploma?

Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani anakwenda kusoma ili kuja kuwa bani au snakwenda kusoma ili ku gain/establish/accomplish jambo?
Mwambie akae ajiulize kwanza anataka kusoma baada ya kuona gap lipi? Asije akaenda kusoma ili kuja kutumiwa
 
Hii kozi inahusu masuala ya Maendeleo ya Jamii ni Chuo kilichobobea katika fani hizo ni kile cha TENGERU, Arusha japo vipo vingine vinavyotoa astashahada (BASIC CERIFICATE) na Dilpoma.
 
Mimi siyo msomi kwahiyo haya mambo siyajui kabisa. Binti wangu ana D ya History, D ya Geography, D ya Kiswahili, D ya English na D ya Civics. D zote kazipata baada ya kurisiti mtihani wake. Sasa anauliza aende akasomee mambo gani ambayo ataweza kupata ajira kwa urahisi serikalini au ikibidi kupangiwa kituo cha kazi mara baada tu ya masomo. Hataki upolisi wala ualimu. Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aende akajifunze ufundi VETA ili aweze kujiajiri
 
Nilipata kumshauri kijana mmoja akasome VETA.

Aliangua kilio.

"Lakini nataka na mimi nisome!"

VETA siyo kusoma -- ndivyo yalivyo mawazo potofu ya vijana wengi.
Kule kuna fani nyingi zenye uwezo mkubwa kumuezesha mtu kujiajiri
 
Back
Top Bottom