* Anatafutwa kuisaidia Tanzania *

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Ndiyo anatafutwa!

Kiongozi ambaye atakuwa jibu la maswali ya Watanzania
Ambaye atakuwa mkweli na mwadilifu
ambaye hatawazungusha Watanzania kwa maneno
Na kuwazuga kwa kauli!

Anatafutwa asiyefanya makosa, asiye na doa hata chembe
Ambaye historia yake haina makosa, ambaye ni mkamilifu katika hali
Mwende ndoa isiyo na utata, na mwenye pesa zinazojulikana
Asiye na majigambo ya aina yoyote, mkamilifu kwa kila hali!

Anatafutwa mtu yule ambaye ataweza kusimama
dhidi ya wale wote wanaoihujumu nchi yetu
ambaye hatokubali kukaa meza moja na wezi
Na kujadiliana makubaliano na matapeli!

Anatafutwa kiongozi ambaye atasimam upande wa wanyonge
Na ambaye hatokoma kuwatetea hata kama itaharibu jina lake
Ambaye atakuwa tayari kuwalinda na kuwasimamia ili na wenyewe wawe na nafasi

Anatafutwa mtu ambaye atakuwa tayari kuhakikisha kuwa
Sheria za nchi yetu zinatumika ipasavyo na si kama mapendekezo
Atakayeapa kweli kuilinda na kuitetea katiba yetu
Na kulinda mipaka yetu toka maadui wa ndani na wanje!

Anatafutwa kiongozi ambaye hatapiga magoti kwa watulao
Na hatatoa sadaka ya urafiki kwa watuchumao!
Ambaye hatalala kitanda kimoja na wanafaiki
Au kujifunika mablanketi ya woga na watuibiao!

Anatafutwa katika mitaa ya Tanzania
Na katika barabara za miji na vijiji vyetu
Kiongozi hatakoma kupambana na ufisadi
Hata kama unawagusa watu wa nyumbani kwake

Anatafutwa ambaye atakuwa tayari kuwatia pingu wezi
Na kuwasimamisha kizimbani waliobaka raslimali zetu
Na wale waliochukua bila kuomba mali zetu (walioiba)
Na ambao leo wanaendelea kunesa nesa na kujifanya maskini!

Anatafutwa Mtanzania jasiri, mwenye uzalendo wa kweli
Ambaye haogopi kuchukiwa, na ambaye anathamini Taifa lake kuliko uhai wake
Mtu ambaye yuko tayari kuacha sifa na jina lake vibezwe ili haki itendeke
Na siyo tu kutendeka bali ionekane imetendeka!

Anatafutwa kiongozi wa kuisaidia Tanzania kusimama
Mwenyekiti bora wa kijiji, Meya bora wa mji
mbunge mzalendo wa jimbo lake, na afisa makini wa taasisi yake
Yule ambaye kwake Tanzania ni kitu cha kwanza na tumbo lake cha mwisho!

Ni nani atampata, na kumleta
Ni nani atamkuta na kumuita
Ni nani atamtambua na kumjulisha kwetu?
Ni nani atasimama na kutuonesha kuwa huyu "ndiye yule"?

Ndugu zangu tunapoelekea 2010 na baadaye
Tanzania iko katika mchakato wa kumtafuta mtu yule
Ambaye anaweza kuwa tayari siyo kunyosha wapi kwa kwenda
Bali kuongoza njia ya kwenda pamoja nasi!

Tunapowasikia watu wanasimama na kufanya wanachofanya
Wanapozungumza na kujinadi, wakishangiliwa na kufurahiwa
Lazima tujiulize kama huyo ndiye tunayemtafuta au tusubiri mwingine?
Kama siye, huyu tunayemtafuta yuko wapi?

ANATAFUTWA - ATAPATIKANA?
 
Huyu mtu mimi nimeanza kumuona kwa mbali na hivi karibuni nitamtangaza hapa JF. Nina hakika kuwa huyu (hawa) mtu (watu) yu(wa)po na ni suala la muda tu......
 
It Is a time for change, the true change
From Magogoni down to manzese
Through Chalinze upto idodomya, heading to ujiji upto ibwera
Down to ndanda without forgeting mwanarumango,
Change in the north, change in the south
Change in the heart land
Change in the east,change in the west.
And Change in ourselves.

How can we do the same thing in the same way and expect different results?
How can we do nothing and expect to get something?
That is why i say we need change.
Change my brothers
that is what we need !

I tell you who we are!!!!
We are the warriors!,fierce than fire
with hearts sharp like Spears of Mkwawa
Grand Children of kinjekitile
Who will stop us if we mean it?
We need change.

When we shouted go!
The colonialists run
What if we had raised our spear
They would perhaps have died with horror!
We are the conqueror of the Nyikas
we dine with lions
and dance with lionesses
Now we say that
we want our country back
We want change.

We want medicine in our hospitals
We want books in our schools
We want roads in the hinterlands
We want want water from our tapes
We want electricity even in the msonge house
We want transparency in our government affairs
We want jobs and opportunities
We want rule of law
We want true peace and security
But we need Change!!!
 
Anatafutwa asiyefanya makosa, asiye na doa hata chembe

"...will remain in but a fleeting illusion, to be pursued, but never attained..." - H.I.M. Haile Selassie I 18th Season of the General Assembly of the United Nations, October 4, 1963
 
Mwana wa Mwita nimesikia,siko mbali hakika.
Kilio na machozi yenu futeni, suruhisho mmelipata
Upanga uta mkuki shikeni, mafisadi kuwatoa
Mwkjj, Mwk, Invisible Pundit nipitisheni,jamani mkiweza

Siko mbali jamani nipeni hii nchi mshuhudie mijitu ikiikimbia nchi, sisemi nitawala kwa jaziba bali busara na maarifa, watu mmechoka na kubezwa na hawa jamaa, nipeni muone kazi.Sitamuonea mtu kamwe, hakli itatawala hakika,

acheni mnijadili, ili mje na jawabu.
 
"...will remain in but a fleeting illusion, to be pursued, but never attained..." - H.I.M. Haile Selassie I 18th Season of the General Assembly of the United Nations, October 4, 1963

Only you could've noticed that...
 
naungana na mwafrika wa kike kuwa huyu atapatikana si punde.
tatizo watajitokeza wengi wenye kusema wana mioyo safi ila matendo yatawanyammbua
 
sisi wote tuna jukumu la kumpata huyu myu kama ifuatavyo

1. kutengeneza taifa lenye watu wa kulipenda taifa lao. TAIFA ambalo wananchi wake wanakiburi ya kujiweka kifua mbele na kudai hili ni taifa letu, na sisi ni wanachi wake. kwa kujipusha na dhana ya kujivunia vyama vya siasa pekee. kama tunalipenda taifa letu basi tutawafyekea mbali, mafisadi, mafedhuli, wabaguzi, wakabila na waroho walewa madaraka.

2. tukiweza kuwaondoa hawo wote niliowataja hapo juu, tujue kuwa waliobaki wataingia madarakani kwa hofu ya Mungu, kamwe hawatathubutu tena kucheza michezo ya kugiza kama richmond, epa n.k

hakuna mtume au nabii atakayeshuka Toka peponi kuja kutawala nchi hii, sisi wenyewe ndiyo tutakayemtengeneza huyo mtume kati yetu, kwa kuweka mazingira mazuri
 
mwikimbi maneno mazito hayo; kwa mtu yeyote anayeangalia hali inavyoandelea ni wazi kuwa tuna matamanio ya kiongozi atakayetokea wakati muafaka. Baadhi ya watu waliamini na wanaendelea kuamini kuwa kiongozi huyo yupo tayari na sasa ndiye aliyeshika madaraka. Sijui hili lina ukweli kiasi gani hasa nikikumbuka jinsi watu walivyokuwa wanaandamana kumuona na kushikana naye mikono wakati wa kampeni 2005.. ja asilimia 80 ya wapiga kura wanaweza kuwa wamekosea hivyo?
 
Tukipewa muda wa kuwachambua vizuri wanaoutaka UONGOZI wa NCHI YETU kama inavyofanyika USA, tunaweza kumpata Kiongozi wa aina hiyo?
 
Ninajisikia raha kuwa mmoja wa wanaJF, vichwa vilivyojipanga humu vinanifanya nifarijike kuona kwamba siku moja atapatikana huyo tunayemtafuta. Kiongozi muadilifu kwa maneno na vitendo!
 
Ndiyo anatafutwa!

Kiongozi ambaye atakuwa jibu la maswali ya Watanzania
Ambaye atakuwa mkweli na mwadilifu
ambaye hatawazungusha Watanzania kwa maneno
Na kuwazuga kwa kauli!

Anatafutwa asiyefanya makosa, asiye na doa hata chembe
Ambaye historia yake haina makosa, ambaye ni mkamilifu katika hali
Mwende ndoa isiyo na utata, na mwenye pesa zinazojulikana
Asiye na majigambo ya aina yoyote, mkamilifu kwa kila hali!

Anatafutwa mtu yule ambaye ataweza kusimama
dhidi ya wale wote wanaoihujumu nchi yetu
ambaye hatokubali kukaa meza moja na wezi
Na kujadiliana makubaliano na matapeli!

Anatafutwa kiongozi ambaye atasimam upande wa wanyonge
Na ambaye hatokoma kuwatetea hata kama itaharibu jina lake
Ambaye atakuwa tayari kuwalinda na kuwasimamia ili na wenyewe wawe na nafasi

Anatafutwa mtu ambaye atakuwa tayari kuhakikisha kuwa
Sheria za nchi yetu zinatumika ipasavyo na si kama mapendekezo
Atakayeapa kweli kuilinda na kuitetea katiba yetu
Na kulinda mipaka yetu toka maadui wa ndani na wanje!

Anatafutwa kiongozi ambaye hatapiga magoti kwa watulao
Na hatatoa sadaka ya urafiki kwa watuchumao!
Ambaye hatalala kitanda kimoja na wanafaiki
Au kujifunika mablanketi ya woga na watuibiao!

Anatafutwa katika mitaa ya Tanzania
Na katika barabara za miji na vijiji vyetu
Kiongozi hatakoma kupambana na ufisadi
Hata kama unawagusa watu wa nyumbani kwake

Anatafutwa ambaye atakuwa tayari kuwatia pingu wezi
Na kuwasimamisha kizimbani waliobaka raslimali zetu
Na wale waliochukua bila kuomba mali zetu (walioiba)
Na ambao leo wanaendelea kunesa nesa na kujifanya maskini!

Anatafutwa Mtanzania jasiri, mwenye uzalendo wa kweli
Ambaye haogopi kuchukiwa, na ambaye anathamini Taifa lake kuliko uhai wake
Mtu ambaye yuko tayari kuacha sifa na jina lake vibezwe ili haki itendeke
Na siyo tu kutendeka bali ionekane imetendeka!

Anatafutwa kiongozi wa kuisaidia Tanzania kusimama
Mwenyekiti bora wa kijiji, Meya bora wa mji
mbunge mzalendo wa jimbo lake, na afisa makini wa taasisi yake
Yule ambaye kwake Tanzania ni kitu cha kwanza na tumbo lake cha mwisho!

Ni nani atampata, na kumleta
Ni nani atamkuta na kumuita
Ni nani atamtambua na kumjulisha kwetu?
Ni nani atasimama na kutuonesha kuwa huyu "ndiye yule"?

Ndugu zangu tunapoelekea 2010 na baadaye
Tanzania iko katika mchakato wa kumtafuta mtu yule
Ambaye anaweza kuwa tayari siyo kunyosha wapi kwa kwenda
Bali kuongoza njia ya kwenda pamoja nasi!

Tunapowasikia watu wanasimama na kufanya wanachofanya
Wanapozungumza na kujinadi, wakishangiliwa na kufurahiwa
Lazima tujiulize kama huyo ndiye tunayemtafuta au tusubiri mwingine?
Kama siye, huyu tunayemtafuta yuko wapi?

ANATAFUTWA - ATAPATIKANA?

kwa nini tusifanye mpango tukatengeneza bango letu lenye haya maneno halafu tukalibandika mitaani kama matangazo ya biashara ili hata hawa watawala waliokuwepo wajue kabisa hatuwahitaji tena na hii itamfanya naye jk atambue kuwa ameshachemka na watu hatumuhitaji tena hiyo 2010
 
huyu mtu tunaweza kumpata punde wanachi wote tutakapo shikamana na kukataa flana,kanga,flana,ubwabwa,nyama na buku 2X2 za vocha.
 
tuliokuwa tunamjua jk, tuliona jinsi wanachi walivyokosea, never on earth populist has become a good leader. watu wenye majina wanaishia kama akina hitler na wengine. katika biblia tunaambiwa kuhusu mfalme aliyekuwa na jina kubwa sauli. lakini bwana akamchagua daudi yule ambaye hawakumjua lakini bwana alimjua.

ninachoandika hapa ni kwamba, urais uwe ni tasisi, na taasisi tuijenge siye wenyewe. kwa mfano kama tulilijenga taifa lenye maadili mema, ni wazi jambazi hatakubali kupigania kuwa kiongozi wake. kwa kuwa ataumbuka.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom