Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,395
- 39,531
Ndiyo anatafutwa!
Kiongozi ambaye atakuwa jibu la maswali ya Watanzania
Ambaye atakuwa mkweli na mwadilifu
ambaye hatawazungusha Watanzania kwa maneno
Na kuwazuga kwa kauli!
Anatafutwa asiyefanya makosa, asiye na doa hata chembe
Ambaye historia yake haina makosa, ambaye ni mkamilifu katika hali
Mwende ndoa isiyo na utata, na mwenye pesa zinazojulikana
Asiye na majigambo ya aina yoyote, mkamilifu kwa kila hali!
Anatafutwa mtu yule ambaye ataweza kusimama
dhidi ya wale wote wanaoihujumu nchi yetu
ambaye hatokubali kukaa meza moja na wezi
Na kujadiliana makubaliano na matapeli!
Anatafutwa kiongozi ambaye atasimam upande wa wanyonge
Na ambaye hatokoma kuwatetea hata kama itaharibu jina lake
Ambaye atakuwa tayari kuwalinda na kuwasimamia ili na wenyewe wawe na nafasi
Anatafutwa mtu ambaye atakuwa tayari kuhakikisha kuwa
Sheria za nchi yetu zinatumika ipasavyo na si kama mapendekezo
Atakayeapa kweli kuilinda na kuitetea katiba yetu
Na kulinda mipaka yetu toka maadui wa ndani na wanje!
Anatafutwa kiongozi ambaye hatapiga magoti kwa watulao
Na hatatoa sadaka ya urafiki kwa watuchumao!
Ambaye hatalala kitanda kimoja na wanafaiki
Au kujifunika mablanketi ya woga na watuibiao!
Anatafutwa katika mitaa ya Tanzania
Na katika barabara za miji na vijiji vyetu
Kiongozi hatakoma kupambana na ufisadi
Hata kama unawagusa watu wa nyumbani kwake
Anatafutwa ambaye atakuwa tayari kuwatia pingu wezi
Na kuwasimamisha kizimbani waliobaka raslimali zetu
Na wale waliochukua bila kuomba mali zetu (walioiba)
Na ambao leo wanaendelea kunesa nesa na kujifanya maskini!
Anatafutwa Mtanzania jasiri, mwenye uzalendo wa kweli
Ambaye haogopi kuchukiwa, na ambaye anathamini Taifa lake kuliko uhai wake
Mtu ambaye yuko tayari kuacha sifa na jina lake vibezwe ili haki itendeke
Na siyo tu kutendeka bali ionekane imetendeka!
Anatafutwa kiongozi wa kuisaidia Tanzania kusimama
Mwenyekiti bora wa kijiji, Meya bora wa mji
mbunge mzalendo wa jimbo lake, na afisa makini wa taasisi yake
Yule ambaye kwake Tanzania ni kitu cha kwanza na tumbo lake cha mwisho!
Ni nani atampata, na kumleta
Ni nani atamkuta na kumuita
Ni nani atamtambua na kumjulisha kwetu?
Ni nani atasimama na kutuonesha kuwa huyu "ndiye yule"?
Ndugu zangu tunapoelekea 2010 na baadaye
Tanzania iko katika mchakato wa kumtafuta mtu yule
Ambaye anaweza kuwa tayari siyo kunyosha wapi kwa kwenda
Bali kuongoza njia ya kwenda pamoja nasi!
Tunapowasikia watu wanasimama na kufanya wanachofanya
Wanapozungumza na kujinadi, wakishangiliwa na kufurahiwa
Lazima tujiulize kama huyo ndiye tunayemtafuta au tusubiri mwingine?
Kama siye, huyu tunayemtafuta yuko wapi?
ANATAFUTWA - ATAPATIKANA?