ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

Kama mada inavyojieleza hapo juu ,wiki hii niliweka tena thread kuhusu husaidizi wa kumpata huyu ndugu,lakini alitokea member akanipigia kuwa atakuwa anamfahamu: ilivyokuwa,siku ya kwanza niliongea naye na kunihaidi kuwa kuna mdogo wake ambaye(m) anasoma bording mbozi mjini,na angeenda siku ya sikukuu ya idd ili amwone mzee akanipa namba tukawasiliana ,naye akahaidi kunipa ushirikiano,akanambia mzee alikuwa ni rafiki wa baba yake mzazi na hivyo anapajua anapoishi katika kijiji cha isansa wilaya ya mbozi.

Basi m alinambia kutoka hapo alipo hadi hapo isansa ni km 16,na inagarimu kiasi cha 15elfu nikaone hisiwe shida nikamtumia 25elfu,kwa maelezo yake akaenda hadi kwa mzee na hakumkuta alikuwa hospitali ya mbozi misheni,bahati nzuri kuna watu nimesoma nao chuo wako huko na ndugu zao wanafanya hapo kazi ,nikawambia waende waulizie hapo,wakamtafuta hawakumkuta,nikaona nimtarifu huyu member na mdogo wake ili nende nao kidogo kidogo ili wajue sijui chochote,badae wakabadili maelezo kuwa yuko kijiji cha mpito bahati nzuri university mates wangu wakatoa ushirikiano hadi tukapata namba za wenyekiti wa vitongoji wa hapo nao wakatoa ushirikiano na kuambiwa huyo mtu hayupo hapo kijijini.

Jana huyu member akanambia amepata taarifa huyo mzee yupo kijiji cha wasa anatibiwa huko ,bahati nzuri tena university mates wangu wakatoa ushirikiano hadi tukapata mawasiliano ya diwani wa kata hatimaye wenyeviti wa vitongoji wakasema huyo mtu hayupo hapo na wakasema wenda akawa anatibiwa kwa waganga pia wakafika kwani member alikuwa ametoa jina la mtu anayemtibu,hawakumkuta.

Leo mchana huyu member akapiga kunitarifu yuko mbozi kaondoka dar na gari ya magazeti na pasipokujua nimeshafanya critical analysis juu yao akanambia anaitaji elfu 10 aweke mafuta kwenye boda aende hapo kijijini,nilimjibu kwa mkato kuwa siwezi,haachane na hiyo kazi yake. Analysis yangu ikawa imekamilika kuwa hawa jamaa walikuwa si watu wema.

Nawashukru sana mates wangu wote walonipa ushirikiano na wote wenye mapenzi mema hasa hawa waheshimiwa wenyeviti wa vitongoji na diwani pia manesi walonipa ushirikiano wa karibu kabisa.Mungu awabariki sana.
 
unaweza kuweka uzi wako wa awali hapa na sisi tukauona labda kuna mtu anaweza kukusaidia bila kumtumia hela
 
Weka jina la huyo member hapa .otherwise na wewe pia ni tapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu yangu jaribu kufatilia mada zangu humu ndani kabla ya kuhoji chochote,fikiri kabla ya kutenda, jaribu kuwa mtu wa kuheshimu wengine, najua utu wa mtu,hakunipa jina ila alisema ni member humu,namba yake ninayo.UNA UHURU WA KUANDIKA CHOCHOTE ILA PIA HUSOME NA SHERIA ZA MATUMIZI YA MITANDAO ZINASEMAJE ILI UITUMIE VYEMA
 
Back
Top Bottom