ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

Wilson Gamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
777
749
Kama mada inavyojieleza hapo juu, huyu ndugu alikuwa askari magereza katika gereza la Musoma miaka ya 1980 na aliondoka Musoma mwaka 1983.

Anatafutwa na kijana wake anaitwa Matiku alimzaa na mama mmoja anaitwa Monika mwenyeji wa Musoma Vijijini,alizaliwa miaka ya 1981.Kwa mujibu wa mama Monika,mzee Michael Juma alikuwa na mke mnyilamba wa Singida ambapo kwa kipindi hicho walikuwa na mtoto wa kike jina lake Anna na huyu mama walikuwa wanamwita mama Anna.

Pia mzee Michael Juma alikuwa anasema wazazi wake walikuwa wanaishi Masasi na badae walihamia Mtwara Mjini kwa muda,bahati mbaya jina la babu yake mzeze Michael hatukuweza kulipata.

Kama huyu mzee bado yupo hai au kama kuna mtu anamjua au kama huyu binti yake yupo naomba sana kwani JF inaiunganisha Tanzania ,naomba tuwasiliane kwa namba 0789443404/0762364740.

Hii itasaidia huyu jamaa aweze kuwapata ndugu zake,kikubwa anataka tu amwone mzee wake na pia aweze kumsaidia hata kumjengea nyumba mbali na kwamba hakumlea lakini ni haki yake hafanye hivyo kwa baba yake.

ASANTENI
 
Hakuna lolote huo ni mtego tu ili baba ajitokeze.
ndugu hii siyo kumuadaa ili ajitokeze hapana,anaweza asijitokeze na haita kuwa na effect yoyote,ila tu nikueleze kiundani huyu mwanae ana lengo hilo na yuko vizuri kimaisha.
 
Matapeli wamepewa fursa.
Ndugu mpendwa,jaribu kufatilia kwa makini thread zangu ambazo huwa naanzisha humu ndo utajua mimi ni mtu wa kariba gani,pia kama hamjui haina shida,cha msingi mwanae anamtafuta na ana lengo zuri na yeye,wala hakutakuwa na effect yoyote hata kama hatajitokeza.Mungu akubariki.
 
Kiufupi inaonyesha kijana anapenda kuiona sura ya baba yake,Jamani mkumbuke baba ni baba tu
 
Mbona kama mna mshawishi. Inatosha kusema anatafutwa kuliko kuongeza anataka kumjengea nyumba,hii mnakaribisha matapeli tu na usumbufu.
 
Alizaliwa musoma miaka ya 1979-1980.Baba yake anaitwa Juma Michael.Mzee Juma alikuwa askari magereza-Musoma miaka ya 1980 na mkazi wa mtwara.Mama yake Anna alikuwa ni mnyiramba wa singida.Kama kuna mtu anamjua au yeye mwenyewe yupo naomba tuwasiliane anaweza kusaidia kupatikana kwa taarifa za mzazi wake mzee Juma,ambaye anatafutwa na kijana wake.
 
Samahani ni Dada au ndugu yako wa karibu?

Wasalimu Wana Gamba kuanzia Busumbiro wa Bunda na Majita-Makojo!
 
Back
Top Bottom