Anaswa Akiangalia Ngono Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anaswa Akiangalia Ngono Bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa nchini Indonesia ambaye alijipatia umaarufu kwa kusimama kidete kushinikiza sheria kali zipitishwe kama vile kutupwa jela miaka 15 kwa kushiriki kwenye video za ngono, mbunge huyo amelazimika kujiuzulu baada ya kunaswa akiangalia ngono bungeni.
  Arifinto, mwanasiasa wa nchini Indonesia ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupigania sheria za kupinga video na picha za ngono, amenaswa akiangalia video ya ngono ndani ya kikao cha bunge.

  Arifinto alilazimika kujiuzulu ubunge baada ya picha zake kusambaa kwenye vyombo vya habari zikimwonyesha akiwa bize kwenye laptop yake akiangalia video ya ngono.

  Arifinto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza na hatimaye kupitishwa kwa sheria ya kupinga picha, video na vitendo vya ngono hadharani.

  Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2008 inaweka wazi kuwa adhabu ya kutupwa jela hadi miaka 15 au kupigwa faini itamkumba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kubusiana hadharani au kuangalia picha au video za ngono.

  Kuzionyesha, kuzimiliki au kuzihifadhi video au picha za ngono ni marufuku kwa mujibu wa sheria hiyo.

  Arifinto mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa ndio msemaji mkubwa wa kushinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo.

  Arifinto aliitisha kikao na kutangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa anajiuzulu ubunge wake mara moja.

  "Huu ni uamuzi wangu, hakuna mtu aliyenishinikiza kufanya hivyo", alisema Arifinto ambaye kama raia wengine wa Indonesia anajulikana kwa jina moja tu.

  Indonesia, ni nchi ya kidemokrasia yenye jumla ya watu milioni 237, ndiyo nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.

  5603734.jpg
   
 2. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbunge Anayepiga Vita Sinema za Ngono Anaswa Akiangalia Ngono Bungeni

  Arifinto akipiga chabo video za ngono ndani ya Bunge Friday, April 15, 2011 2:40 AM
  Mbunge wa nchini Indonesia ambaye alijipatia umaarufu kwa kusimama kidete kushinikiza sheria kali zipitishwe kama vile kutupwa jela miaka 15 kwa kushiriki kwenye video za ngono, mbunge huyo amelazimika kujiuzulu baada ya kunaswa akiangalia ngono bungeni.
  Arifinto, mwanasiasa wa nchini Indonesia ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupigania sheria za kupinga video na picha za ngono, amenaswa akiangalia video ya ngono ndani ya kikao cha bunge.

  Arifinto alilazimika kujiuzulu ubunge baada ya picha zake kusambaa kwenye vyombo vya habari zikimwonyesha akiwa bize kwenye laptop yake akiangalia video ya ngono.
  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Arifinto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza na hatimaye kupitishwa kwa sheria ya kupinga picha, video na vitendo vya ngono hadharani.

  Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2008 inaweka wazi kuwa adhabu ya kutupwa jela hadi miaka 15 au kupigwa faini itamkumba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kubusiana hadharani au kuangalia picha au video za ngono.

  Kuzionyesha, kuzimiliki au kuzihifadhi video au picha za ngono ni marufuku kwa mujibu wa sheria hiyo.

  Arifinto mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa ndio msemaji mkubwa wa kushinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo.

  Arifinto aliitisha kikao na kutangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa anajiuzulu ubunge wake mara moja.

  "Huu ni uamuzi wangu, hakuna mtu aliyenishinikiza kufanya hivyo", alisema Arifinto ambaye kama raia wengine wa Indonesia anajulikana kwa jina moja tu.

  Indonesia, ni nchi ya kidemokrasia yenye jumla ya watu milioni 237, ndiyo nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hatari tupu! Mwosha huoshwa.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Fuateni nisemayo...Siyo Nitendayo!...ha ha haaa!
   
 5. K

  KWELIMT Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yaaap angalau wenze2 wana utamaduni wa kuwajibika,mmmh ingekuwa hapa kwetu angekmaa mbele ya waandishi wac habari.
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaa mtu hatoki na chama unakuta kinamuogopa kumtoa!umenikumbusha mabomu ya mbagala na gongo la mboto
   
 7. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nzuri.....uwajibikaji co mpaka upigiwe kelele na watu!!!....
   
 8. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,121
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Njemba iko bize ina concetrate..smh!
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hapo ishu ya dowans na katumwa na wananchi!
   
 10. One and Only

  One and Only Senior Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huo ndio uzuri wa sheria, kawajibika na bado uchunguzi unafanyika ili kujua kama ana kosa na ahukumiwe kwa sheria aliyoipigania kwa nguvu zake zote
   
 11. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kweliii! raha jipe mwenyewe!
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu na huyu yupi bora?
  [​IMG][​IMG]
   
 13. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :yield:

  Hapo sio kuwajibika kwa kujiuzulu....Lazima meno ya sheria aliyoisimimamia kidete yamtafune otherwise itakuwa habari ile ile ya kutunga sheria kwa ajili ya maskini na makapuku wa kawaida na sio wao viongozi......aende 15 na yeye
   
 14. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  dah! isije ikawa wamembambikia kwa kumtumia virus mail.. anaifunguwa ngoma ika staki ..:tape:
   
 15. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,075
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280
  juzi imekuja thread ikiwa na picha zinazomwonyesha mwanamke mwenye umri wa miaka 34 kutoka Indonesia akichapwa viboko kwa kosa la kutembea na mwanaume mwingine huku akiwa kapewa talaka na mumewe.

  sasa huyu mbunge nae inakuwaje?
   
 16. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,075
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 280
  hiyo nimeipenda.
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Bora huyo alyelala manake akiamka hapo atakuwa kaoteshwa kikombe!!
   
 18. M

  Msharika JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu aliyelalal anamwaza CD wake aliyemchosha, sasa heri huyo atimzaye picha kuliko..........................
   
 19. c

  chetuntu R I P

  #19
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dah, huyu alielala yuko mbali sana anapanga mistari mipya ya kusifu kujibua magamba.
   
Loading...