Anasema anajuta, nimsamehe

super black

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
566
532
Mwaka Jana mwezi 12 nilikutana na Dada mmoja katika moja ya mitandao ya kijamii na tukaanzisha mahusiano Mimi Niko mkoani yeye yuko dar es salaam.

Mwaka huu mwezi wa pili nilionana na huyu Dada jijini Dar baada ya kwenda mishemishe kwa muda wa mwezi mmoja.
Kipindi nawasiliana na huyu bidada nilishawai mgusia swala la kum hack nijue anawasiliana na nani nilimwambia Nina uwezo wa kufanya hivyo(truly siwezi)alikataa kabisa na nikamwambia kuna kitu anaficha yes akakili kua anawasiliana na ex wake akaomba msamahe yakaisha.

Nilivorudi mkoani nikagusia tena kuhusu kum hack akakataa kabisa nikajua kuna kitu siku iyo usiku nikajifanya mechanganyikiwa baada ya kumhack nilianza kulalamika kwanini kanifanyia aliofanya.Aliuliza kama memuhack nikasema yes

Alianza kulalamika ila mwisho akakiri kutoka na mume wa MTU na sababu kubwa ni ugumu wa maisha sababu kwao anaishi na mama yake na wadogo zake na wote wanamtegemea yeye amekiri kosa kalia sana anaomba asamehewe anasema hawezi kufanya ivo tena.

NB:nilipanga mwaka huu nikajitambulishe kwao nimuoe ila mpaka sasa sijui nifanyaje ingawa nilikutana nae mtandaoni nilitokea kumuamini sana sana sana.

Anaomba msamaha anasema kajutia kosa lake na SIJUI NIFANYE NINI.

Nisaidieni ushauri wakuu.
 
Unayatafuta matatizo mwenyewe kisha unaanza kulalamika bro? Acha kuleta hisia za kuibiwa katika mapenzi, yaani wewe unaishi na mtu ila mateso unayatengeneza mwenyewe ina maana gani kuwa kwenye mahusiano na yeye.

Usitegemee kuna mwanamke kamilifu utamtafuta hata katika jamii yako hautampata kila mmoja ana mapungufu yake.

Yaani unakaa na kuibua kitu kikianza kukuumiza unalalamika? Acha mambo yasiyo na maana kama kweli una nia ya kuwa naye kimapenzi/kindoa.
 
Yan unataka kwenda kwao!!
Mosi mmekutana mtandaoni sawa sio shda,
Pili vimbwanga vyote hvyo bado umella

Nakutakia kila la kheri
 
Halo ni ngumu kujua kama anafanya hivyo kwa shida au ndio tabia yake, so inabidi uwe mwangalifu sana vinginevyo utakuja kulia kulia badae

Sent using kidole gumba
 
Wewe mwenyewe unaichoka amani, halafu unataka tukushauri?!
Ulitaka akiri ili iweje, umuache au umsamehe?!
Sio kwamba hujui la kufanya, unaogopa kufanya hivyo!! Sasa fanya venye moyo wako unataka!
 
I recommend you to go on with her. Yaonekana ulikuwa umuhudumii ndiomana akakwambia ukweli kuwa kutokana na ugumu wa maisha ilibidi afanye hivyo. Pia hatarudia kama alivyosema kwasababu keshaamini kuwa una uwezo was kufuatilia mawasiliano yake.

Omba asiwe member humu akauona huu uzi
 
Upekee wa wanaume anapoamua kumpenda mwanamke kwelikweli. Huwa haijalishi niwapi amemkuta , atamwamin utadhan wamejuana miaka kadhaa ilopita


Shida nihuyo alochaguliwa kuaminika ....


Tatizo haya mambo, ukishayathibitisha huwa yanabaki kuzunguka zunguka kichwan na kuondoa Amani.


Humchukua Mwanaume Jasiri sana kuendelea kupenda kwa kipimo kile kile , na anayeweza hapa, ataweza hata kuishi na mdada mwenye mtoto.


Anyway ,unamsamehe ndio, lkn shida atafanyaje umuamin ? ( inabaki ni imani tu).

Unamsamehe, lkn je shida anazozisemea kwao zimeisha ??.



Aya, akiamua kua anakushirikisha shida zake, je utazitatua ? Au wee kumpa pesa ni pale utakapokua unakutana naye tu siku hiyo unakula mzigo nandipo unampa naela ??.....ataishije sasa ???.



Mambo ni Mengi sana, na mambo yana changanya sana..



Ila mwisho, Hamnaga sababu ya kuhalalisha MTU KUCHEPUKA ,haipo haipo haipo..... Kwann usiombe mtaji?...



Mtoa mada Fanya kitu kimoja, wakati Fulani ni ngumu, Ila ukweli nikwamba kuna baadhi ya watu wakiomba msamaha humaanisha , embu mpe nafasi nyingine, na wewe sasa JITAHIDI KADIRI ya uwezo wako ,umwondelee "Ushawishi anaoupata" ili asiseme "Nilichepuka sababu ya kitu Fulani ".... ikiwezekana na ujitambulishe .





Kuna watu ni wachepukaji hodari hao nahautakaa ujue !.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom