Anasambaza UKIMWI kazini kwa makusudi, naweza kumsaidia vipi huyu dada?

caxton

Senior Member
May 8, 2015
145
149
Najua mmepumzika majumbani mwenu mkimalizia weekend,

Hapa kwenye shirika letu kuna jamaa mmoja ambae anaishi na HIV kwa muda mrefu sasa, wote na mkewe wanahudhuria kliniki kwa zaidi ya miaka mitano sasa, mkewe sio staff wetu ila wote wanatibiwa na yeye anatibiwa na shirika kama dependant, for the past three years amekuwa na relationship na wasichana kama 3 hivi ninaowafahamu hapa kazini.

Sasahivi anafukuzia msichana mmoja mgeni fresh from college, i mean alimaliza mwaka jana ndo tumemwajiri hivi karibuni.

Dalili zinaonekana there is something in the pipeline, maana jamaa asubuhi huwa anampitia binti kwao (lift) na jioni huenda kukaa sehemu pamoja wakipata vinywaji na baadae humpeleka kwao, na lunch pia pamoja.

Kwa sisi watu wazima hizi ni dalili za mtu anaetongoza mimi na watu wengine wawili hapa HR ndio tunaojua status ya huyu jamaa na yeye hajui kama mimi najua nilijuaje? Health insurer wetu huleta report HR ya wafanyakazi wetu kwa ajili ya auditing na mahesabu, hawaleti report ya staff wote, bali hutuletea report ya wale staff wenye magonjwa ya kudumu mfano Kisukari, Hypertension, Kidney problems, HIV na kadhalika, hii ni kwa sababu wagonjwa hawa hutumia gharama kubwa sana kulinganisha na wagonjwa wa kawaida hivyo huwa tunahitaji kufanya verification wenyewe.

Hivyo inakuja taarifa ya ugonjwa, number of visits against price. Hata hivyo taarifa hizi hubaki siri ya HR department watu wachache tu wenye access nazo, ingawa binadam ni binadam tu wakati mwingine taarifa zaweza toka nje.

At this juncture nimeshindwa nichukue hatua gani kumsaidia huyu binti bila kuleta collateral damage kwa pande zote. Katika taratibu za kazi hatuna mwongozo wa kumbana huyu jamaa kisheria, sijaona popote kwenye HR manual yetu panapombana swala la UKIMWI limeachwa kuwa la hiari sijajua kwa sheria za nchi mtanisaidia hapo.

Najiuliza kwamba inakuaje mtu anajijua ana HIV, anatumia dawa mwaka wa tano, mkewe pia hivyo hivyo, anawezaje kutongoza wasichana huku akijua ana hali hiyo? Maana huyu ni binti wa nne tangu nimejiunga na hili shirika, hao wengine walishaolewa wote lakini alitembea nao, labda kama walitumia kinga. Uvumi wa ukaribu wa hawa watu wawili umeenea kwenye idara yao yote na watu wanachukulia poa tu maana wengi hawajui status ya huyu bwana.

Wakuu,
Nawezaje kumsaidia huyu binti?

Wale wengine nilikaa kimya lakini naona trend inaendelea hivyo hivyo.

Na je nawezaje kuongea na huyu jamaa asinielewe tofauti?

Au ya ngoswe nimuachie ngoswe? Watajijua wenyewe?
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,174
10,561
Mtumie binti text kwa namba mpya ukimtahadharisha na kwamba maamuzi ya mwisho anayo yeye .

Hata huyo jamaa unaweza kufanya hivyohivyo, ila kuwa mwangalifu asijue taarifa imetoka wapi.

Mtawa mmoja wakati wa Adolph Hitler kwa ujasiri alisema "dawa ya kuzuia tairi linalokanyaga watu na kuwajeruhi si kutibu wenye majeraha, bali kulistopisha lisiue zaidi"
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,825
48,907

fuata ushauri wa jamaa
 
mzurimie

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,143
3,617
Ila unadhani hadi leo wenzako hawajakuja na ID hii kwa kuleta habari za ofisini humu, esp ulipoelezea mzungu bosi wenu etc?

Hii kitu inasikitisha, tuma tu sms kama alivyoshauri hapo juu

Haya msisahau kuwapigia kura wanaopeperusha nchi yetu kimataifa

Kupiga kura
Diamond Platnumz kategori 3 (tatu) - Best MALE, Best COLLABORATION na Best LIVE and Vanessa 1(moja) -- Best FEMALE

ilj ngia kwa link hii chini

http://mama.mtv.com/voting/

Bonyeza bonyeza VOTE usichoke
 
Focus120

JF-Expert Member
Nov 10, 2014
1,088
776
Mtumie binti text kwa namba mpya ukimtahadharisha na kwamba maamuzi ya mwisho anayo yeye .

Hata huyo jamaa unaweza kufanya hivyohivyo, ila kuwa mwangalifu asijue taarifa imetoka wapi.

Mtawa mmoja wakati wa Adolph Hitler kwa ujasiri alisema "dawa ya kuzuia tairi linalokanyaga watu na kuwajeruhi si kutibu wenye majeraha, bali kulistopisha lisiue zaidi"
.

fata jamaa anachosema, it might be the best way of not causing a collateral damage both sides.
 
Asabaya

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
1,311
414
Ivi kwani simu hazisajiliwi sikuizi eeh? manake nilisikia ukichukua sim card mpaka usajili.
 
newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,377
544
Mwambie binti akapime status yake.kisha aende kwa huyu jamaaa apime.si ajabu wote ni HIV +ve.
Ila nimeskia kuwa wanaotumia dawa vizuri wanapotwza uwezo wa kuambukiza.ARV zinatuliza nguvu ya maambukizi mapya.
 
theoka

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
374
100
Mtafute kijana wa street tumia cm yake kisha akipigiwa cm atokujua na umbie asiseme nan kaitumia usiposema nawe utakua umeshiriki mauaji
 
Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,555
1,267
Nipe namba za mmoja wao huyo jamaa au bint nimgongee mmoja wao usiogope jamaa ngoja tuokoe maisha
na Hawa mabint wamezidi bana ngoja wapgwe
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
45,436
53,129
Mkubwa Hiyo issue ipo sana watu wanaambukiza makusudi cha ajabu January amekomaa na cyberlaw badala ya kuleta sheria ya kuwabana hawa +'ve kuwaambukiza wengine makusudi wao wamekomaa na cyber crime.
 
Mr. Wise

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,679
6,363

Nawezaje kumsaidia huyu binti?
Wale wengine nilikaa kimya lakini naona trend inaendelea hivyo hivyo

Na je nawezaje kuongea na huyu jamaa asinielewe tofauti?

Au ya ngoswe nimuachie ngoswe? Watajijua wenyewe?

Mkuu sioni damage yoyote otherwise ukiendelea kukaa kimya ndio damage tena kubwa tu, maana uyo binti atavibeba virus na ataendeleza chain iwe ndefu.

Ushauri : Kaa na binti pembeni mpe A to Z, naamini kabisa kama bado alikua hajawahi kuvuliwa chupi na uyo jamaa basi atakushukuru saaaaaana kwa kumuokoa ( Uyo jamaa mtafutie siku usimuingie ktk iyo relationship)
Usiseme ya Ngoswe imagine uyo binti after 1yr anakuja tembea na ndugu yako wa damu, Utakuja sema ningejuaaa.... na si Ngoswe tena.
 
love more than100

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
2,062
707
Ivi kwani simu hazisajiliwi sikuizi eeh? manake nilisikia ukichukua sim card mpaka usajili.

Unaweza kutumia ID fake kusajili mybe card ya hata house girl wenu ukaitumia kwa nia njema after that uunaidestroy hiyo chip but sio haraka unaitumia kwa muda kumweleza huyo binti, achukue taadhari gani na afanyaje jamaa asijue amemjua ni mgonjwa na by z way kama akiamua kumwambia jamaa amwambie na kama jama anabisha akampime sehem 3 tofauti ambazo asimtaji jamaa zime kwa mshtukizo n awe makini maana jamaa anaweza kumppa mpimaji signo na akatoa majibu sio.
 
Mnondwe

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
4,022
3,644
Dah!key pad!namaanisha nipe namba ya babu na binti nimalize tabia chafu
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,753
6,522
Mtumie binti text kwa namba mpya ukimtahadharisha na kwamba maamuzi ya mwisho anayo yeye .

Hata huyo jamaa unaweza kufanya hivyohivyo, ila kuwa mwangalifu asijue taarifa imetoka wapi.

Mtawa mmoja wakati wa Adolph Hitler kwa ujasiri alisema "dawa ya kuzuia tairi linalokanyaga watu na kuwajeruhi si kutibu wenye majeraha, bali kulistopisha lisiue zaidi"

nunua simu ya 15,000/- laini sajili temporary waandikie sms halafu watumie wote kisha simu usiitumie tena
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom