Anasa (Sherehe, Pombe & Kutalii) zitozwe kodi zaidi

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,421
7,080
Katika kutunisha mfuko wa taifa, itafaa kutoza kodi shughuli zote za kifahari ikiwemo HARUSI, Vileo na kutalii ikijumuisha kwenda Hijja, nje ya nchi (kwa imani zote). Hawa wanaoamua kufanya haya wana pesa ya ziada hivyo si mbaya wakituchangia 10% ya bajeti yao. Nawasilisha.

NB: Usichafue hali ya hewa hapa ni katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
 
hapo kwenye sherehe watu wanachangia mpaka 100m kwa harusi moja, TRA waanze kuzunguka kwenye vikao vya harusi kila wikiendi kukusanya taarifa kwa siri ili kikao cha mwisho kabla ya harusi wanawaletea barua ya kiasi kinachopaswa kulipwa RA kabla ya shrehe kufanyika.
 
Katika kutunisha mfuko wa taifa, itafaa kutoza kodi shughuli zote za kifahari ikiwemo HARUSI, Vileo na kutalii ikijumuisha kwenda Hijja, nje ya nchi (kwa imani zote). Hawa wanaoamua kufanya haya wana pesa ya ziada hivyo si mbaya wakituchangia 10% ya bajeti yao. Nawasilisha.

NB: Usichafue hali ya hewa hapa ni katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Duuh mtuache bana,za rambirambi haziwatoshi??
 
... Hawa wanaoamua kufanya haya wana pesa ya ziada hivyo si mbaya wakituchangia 10% ya bajeti yao. Nawasilisha.

NB: Usichafue hali ya hewa hapa ni katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Umefanya research mtu wangu?

Wajua tayari kila chupa ya bia inalipiwa ushuru?
Developed countries of the world walifika huko waliko kwa kufanya hivyo? Je, wanafanya hivyo?
Unafikiri utapata "mchango wa bajeti" kwa siku ngapi kabla watu waache kufanya harusi? Bunge itapitisha?
Hivi tuseme, kila mtu hufanya harusi kwa sababu ana pesa za kutesa?
Wajua kua kuna wale ambao huchangia waumini wenzao ili waende sehemu fulani au hata wafanye harusi kwa kua hawajiwezi kivile?
Ukisikia mtu ni milionea au bilionea, ushawahi kujiuliza kiasi cha ushuru ambacho yeye hulipa kukujengea nchi?

Maswali ni mengi kuliko majibu!
Lakini hebu nikuulize hili:-

Wewe binafsi, unafanya nini kuchangia hiyo bajeti unayozungumzia?

Maneno yako kidogo yanatoa taswira ya mtu ambaye anasubiri wengine wamjengee nchi pamoja na kumpakia rangi
 
Back
Top Bottom