Anas Aremeyaw Anas Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi gumzo Afrika

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,738
155,427
Anas Aremeyaw Anas Mwandishi wa habari za kiuchunguzi aliyezaliwa Ghana mwishoni mwa miaka ya 1970. Maudhui yake makuu ni WATAJE, WAUMBUE na WAFUNGE. Anas ni maarufu sana kwa namna yake ya kuripoti matukio. Yuko kila sehemu, ni kama mzimu unaojibadilisha, mara mtoto, mara mzee, mara mwanamke, ili mradi anabadilika kama kinyonga. Kuficha utambulisho wake ndio silaha yake kuu.

Na kujificha kwake huku sura, amewahi kuiweka wazi sura yake mbele ya camera za BBC mwaka 2015, lakini hamna mtu anayeamini kuwa ile sura iliyoonyeshwa BBC ni ya ANAS. Anas ni mwandishi huru asiye egemea mrengo wa chama chochote cha kisiasa, na nimbobezi kwenye upigaji wa picha za video kwa usiri mkubwa na kwa ustadi wa hali ya juu. Amekuwa ni mripotiji wa matukio ya ufisadi unaoishtua Afrika nzima na dunia kwa ujumla wake, ukandamizwaji wa haki za kibinaadamu pamoja na matukio kadha wa kadha ya rushwa kusini mwa jangwa la Sahara.

Anas ameweza kujishindia tuzo za heshima ya juu kwa kutetea haki za binaadam hasa kwa kuripoti na kufichua mbinu mbalimbali zinazotumiwa kwenye biashara ya utumwa inayoendelea chini ya zulia.

Kazi zake zimempa utambulisho mkubwa sana kwenye jumuia ya kimataifa kiasi kwa raisi anayemaliza muda wake wa Marekani Bwana President Barack Obama alimwagia sifa kedekede alipokuwa akihutubia kwenye ziara yake nchini Ghana mwaka 2009












 
Back
Top Bottom