Anaposahau siku yako ya kuzaliwa

KIDOLEGUMBA

JF-Expert Member
Apr 17, 2013
498
109
Habari zenu wana jamii, mi naomba kuelimishwa juu ya hili swala la kukumbushana siku ya kuzaliwa haswa kwa wapenzi, je mmoja wapo anaposahau kumpa heri ya siku ya kuzaliwa mpenziwe inaonyesha hampendi, hana umuhimu saana au kapitiwa tu?
 
Sio inshu........mambo madogo sana hayo.Watoto wa familia bora ndo mnazo sana hzo,uswaz sisi hata mambo ya b'day hatuna shobo nayo
 
Mimi ndio nitaachwa kila siku. Kuendekeza uzungu.
Ya kwangu mwenyewe sikumbukagi. Kwanini tukumbushane kuzeeka?
 
Sa wengine wanasahau mpk b.day zao wenyewe. Km hao inakuaje?

Kwanza kuongeza mwaka ni kusogeza siku yako ya kufa. So badala ya kupongezana bora kupeana pole
 
haya mambo bana,
watu mmekutana ukubwani lkn mnataka kufanya kama mmezaliwa wote,
hao waliokufuta nyaa wenyewe wanasahau siku yako ya kuzaliwa, sembuse mtu mmekutana ukubwani tena baada ya barehe loh! vitu vingine vya ku-ignore tu jamani havitaki complication otherwise maisha na mapenzi yatakuwa complex too!
 
Zamani nilikuwaga nachukulia ka Big issue..........
kwa nini usahau na tulikuwa tunagombana kabisa
 
Wengine mazingira tuliyolelewa ni ya kuchunga ng'ombe hayo mamboo yenu ya birth day tumeyajulia ukubwani sasa unataka kunilazimisha nikumbuke yako wakati hata yangu mwenyewe ni majanga utaishia kuumia tu na kama kipimo chako cha upendo kiko kwenye kukumbuka siku yako ya kuzaliwa basi mimi utanipiga kibuti mapema sana maana sijuag hayo makitu ya birthday
 
Back
Top Bottom