Anapoondoka kiongozi wa miaka 73 na kurithiwa na wa miaka 72 sidhani kwamba...

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
....kirika hapo kuna mabadiliko
Posted Date::11/8/2007
Profesa Othman achambua mabadiliko ya viongozi CCM
*Asema mabadiliko ya mzee kwa mzee hayasaidii

Na Andrew Msechu
Mwananchi

MHADHIRI wa Taasisi ya Elimu ya Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haroub Othman amesema mabadiliko ya CCM hayawezi kufikiwa kwa kubadili sura katika safu ya uongozi kwa kuwa Ilani ya uchaguzi na Sera za chama zitabaki kama zilivyo.

Profesa Haroub alisema jana kuwa viongozi waliochaguliwa katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM walikuwemo katika uongozi wa juu wa chama hicho, hivyo hawatarajiwi kuleta mabadiliko.

Alisema kwa sasa inabidi CCM ifikirie njia madhubuti za kubadilishana uongozi kutokana na rika, kama wanavyofanya Wachina kwa kuainisha umri ambao mtu anatakiwa kustaafu uongozi.

"Anapoondoka kiongozi wa miaka 73 na kurithiwa na wa miaka 72 sidhani kwamba kirika hapo kuna mabadiliko. Tusisahau kwamba John Malecela alipokuwa Makamu Mwenyekiti kwa mara ya kwanza alikuwa na umri wa miaka 58! Mabadiliko haya kwa nafasi kama vile Makamu Mwenyekiti, Naibu Katibu Mkuu wa Bara, Katibu Mwenezi na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu si suala pekee linaloashiria mabadiliko ndani ya chama hicho," alisema.

Hata hivyo Profesa Haroub alisema kuondolewa kwa viongozi wakongwe hasa kwenye Kamati Kuu ya CCM na kuendelea kuwa na dalili za ugomvi wa makundi lakini pia baadhi yao wameonekana kuchoka.

"Sijui kwa nini wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM wameonelea wasiwapigie kura viongozi hao kuingia katika Kamati Kuu, lakini kwa Komredi Ngombale nafikiri wengi wanafikiri amechoka, anastahili apumzike na kwa Sumaye, nafikiri ni kutokana na ugomvi wa makundi ndani ya CC," alisema.

Naye Midraji Ibrahim anaripoti kutoka Dodoma kuwa; CCM kimesema kinataka kutumia wasomi wake kujitathmini jinsi wananchi wanavyokiona.

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa alisema, jana kuwa baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu, safu za uongozi zimejipanga upya kusimamia shughuli za chama kwa miaka mitano ijayo.

Msekwa alisema, kwa maeneo mengine CCM imepata nguvu mpya ya kutekeleza sera zake kuhusu majukumu kama chama tawala, kutoa uongozi na mwelekeokatika nyanja mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.

Miongoni mwa mikakati iliyoandaliwa na uongozi huo ni kushirikisha kwa karibu vijana wasomi wa chama hicho, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mpango maalum ya awamu mpya ya uongozi wa CCM.

Msekwa alisema, wanataka kutumia Novemba 17, mwaka huu kupata mawazo ya wasomi hao ili wakitathmini chama hicho na kinavyoonekana mbele ya umma. Siku hiyo ni maalum kwa vyuo vikuu duniani.

Makongamano hayo yatafanyika Dar es Salaam, Zanzibar, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mwanza, Arusha na Kilimanjaro na kwamba, mdahalo huo ni wa wazi na washiriki watakuwa huru kuzungumza mafanikio, matatizo na changamoto dhidi ya CCM.
 
Back
Top Bottom