Anapataje updates za group la Whatsapp mbalo hajajiunga ?

Dio

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
1,274
158
Habarini washikadau wangu wa nguvu, naomba kuuliza kuna uwezekano wowote mtu kufuatilia mambo yako unayochat kwenye groups mbalimbali kupitia kwenye email yako, ikiwa anaifahamu na password.

Kwa kifupi kwenye group hayupo,lakini ananiambia kila kitu kinachoendelea kwenye group,hyo inawezeka? au kuna mtu anamwambia kinachoendelea kwa group? au ana account mbili za whatsapp yupo kwenye group bila kujua, au kuna njia unaweza kutumia mtu kufuatilia msg zako za whatsapp
naomba msaada wenu,

Na samahanini kwa usumbufu,
 
Kaka hakuna mahusiano kati ya email yako na whatsapp. kwanza ulitumia namba ya simu kutengeneza account na sio email.

inawezekana yupo kwenye group au kuna mtu anamwambia kama unavyosema.

pia whatsapp inasave chat zako kwenye simu yako na una uwezo wa kujitumia kwa email hiyo backup ya chat, kama unamuachia simu yako inawezekana kazichukua.
 
Asanteni sana wadau kwa maelezo yenu
 
kaka hakuna mahusiano kati ya email yako na whatsapp. kwanza ulitumia namba ya simu kutengeneza account na sio email.

inawezekana yupo kwenye group au kuna mtu anamwambia kama unavyosema.

pia whatsapp inasave chat zako kwenye simu yako na una uwezo wa kujitumia kwa email hiyo backup ya chat, kama unamuachia simu yako inawezekana kazichukua.

Mkuu hivi Inawezekana kuwa na account mbili za whatsapp kwenye simu moja?

Simu yangu ni ya line moja single sim card, sio dual sim.

Je, naweza kutumia line tofauti za simu kufungua account mbili tofauti whatsapp?
Au mpaka niwe na dual sim?
 
Admin ka left group automatically u admin ukaenda kwa mwingine!! Kuna njia ya kumrudisha???@ whatsapp
 
Back
Top Bottom