Lisa
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 1,549
- 1,074
Ni mwanamke wa miaka 30, alikutana na kijana chuoni , wakapendana na wakaishi pamoja wakafanikiwa kupata mtoto mmoja.baada ya hapo walifunga ndoa ya serikali.mungu akawajalia wakapata mtoto wa pili.baada ya hapo mwanaume alirudi chuoni kuongeza elimu zaidi. huko akakutana na mwanamke mwingine wakapendana na kumtelekeza mkewe , na sasa wanataka kufunga ndoa na huyo mwanamkewaliyekutana naye chuoni ndoa ya kanisani. mkewe alipomwambia kuwa kwa nn unafanya hivyo akamwambia Baba yake amemwambia aoe kabila lake na aoe kwenye uwezo, na mbaya zaidi ni kuwa amezaa watoto wakike tuu hajazaa wakiume .je huyu mwanamke afanye nn ? anaomba ushauri wenu.