Ananilea Nkya apata Mrithi TAMWA. Ni Mwandishi wa RTD zamani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ananilea Nkya apata Mrithi TAMWA. Ni Mwandishi wa RTD zamani...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana Mpotevu, Sep 27, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,292
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  [h=2]Mabadiliko ya Uongozi TAMWA: Valerie Msoka achuku nafasi ya Ananilea Nkya[/h]


  Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimepata Mkurugenzi Mtendaji mpya ambaye anachukua nafasi ya Ananilea Nkya anayemaliza muda wake baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka kumi na moja.

  Mkurugenzi huyo mpya wa TAMWA, Valerie Msoka ambaye ni miongoni mwa wanahabari wanawake 12 walioanzisha TAMWA, amefanya kazi za kutukuka katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

  Valerie Msoka atakabidhiwa rasmi ofisi Alhamisi tarehe 27 Septemba katika sherehe fupi itakayofanyika kuanzia saa 3.30 hadi ya 5.00 asubuhi.

  Sherehe hiyo itakayofanyika katika ofisi za TAMWA zilizoko eneo la Sinza-Mori, Dar es Salaam inatarajiwa kuhudhuriwa na wahariri na wanahabari kutoka vyombo vya habari mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya wanahabari, Wakurugenzi Watendaji kutoka mashirika ya kiraia na viongozi wa TAMWA wa zamani na sasa.

  Valerie Msoka alifanya kazi Radio Tanzania Dar es Salaam, shirika la utangazaji la Uingereza BBC idhaa ya Kiswahili na Kiingereza kabla ya kujiunga na Umoja wa Mataifa.

  Kadhalika Valerie Msoka mwenye shahada ya Uzamiri katika fani ya Uandishi wa habari wa Kimataifa (M.A in International Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha City nchini Uingereza, amefanya kazi kwenye maeneo ya vita ikiwemo Iraq, Sudan, Rwanda, Congo na Burundi.

  Valerie Msoka anachukua uongozi wa TAMWA wakati shirika hili likiwa linajiandaa kuanza kutekeleza mradi mkubwa wenye lengo la kuimarisha vuguvugu katika harakati za kujenga usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

  TAMWA itatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama Cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Chama Cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi (CRC).

  Wilaya kumi zitanufaika na mradi huo ambazo ni Wete (Pemba Kaskazini), Unguja Magharibi (Unguja Urban West), Wilaya ya Unguja kusini (Unguja South district), Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruhangwa (Mtwara), Kinondoni na Ilala, (Dar es Salaam).

  Ananilea Nkya
  Mkurugenzi Mtendaji  MY TAKE: Tunasubiri kuona kama TAMWA itarejea kuwa msaada kwa wanahabari wanawake ama itaendelea kufanya harakati zaidi na kusahau taaluma ya Habari
   
 2. UPIU

  UPIU JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 602
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Afadhali amelazimishwa kujiudhuru alikuwa ni disgrace kwenye fani ya habari. Badala ya kutetea misingi ya taasisi yake akajaribu kupora majukumu ya mama Bisimba
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,595
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni mama hodari sana Lucy Nkya, tunakuomba uendelee na harakati zako kama kawaida, ni mmoja wa wanawake jasiri sana ktk nchi yetu.
   
 4. K

  KIGOMA KWETU Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana Tamwa,huyu nkya alisahau majukumu yake akawa anaingilia kazi watu,nimefurahi sana kumpiga chini.

   
 5. k

  kasahunga Senior Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hongera, ila timiza malengo ya tamwa
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  yule mama mpalestina ni jembe kweli kweli...kila la kheri mmachame !
  lakini wanasema ingawa simba ni mkali lakini anazaa !
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,507
  Likes Received: 879
  Trophy Points: 280
  Come on, Ananilea Nkya na Lucy Nkya ni watu wawili tofauti mkuu. By profession the former ni mwanahabari na the latter ni Doctor wa magonjwa ya wanadamu. The former amestaafu baada ya kumaliza muda wake TAMWA na the latter aliachishwa Unaibu Waziri baada ya kukataliwa na Madaktari.
   
 8. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  huyo msoka nae si mchaga au?
   
 9. C

  CAY JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 500
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndiyo hicho tu ulichokioona?
   
 10. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,839
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  'Kama anaperform sioni tija'.....mh mwakyembe [bandari]
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Naye ni mpiganaji kama Ananilea Nkya??
  Tupeni taarifa zaidi wenye CV yake.
   
 12. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,717
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Shame on you, I should say more, but your face made me to have a sympathy
   
 13. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,595
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Alikuwa jasiri, siyo mwoga kamwe, ni mmoja wa wanawake washoka wa nchii hii.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 15,633
  Likes Received: 8,420
  Trophy Points: 280
  Uzazi umeuhusishaje tena na hii habari, Smile yako inaonekana ni ya kinafiki.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,599
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Big up Ananilea Nkya!! Sasa Msoka kazi ya Nkya utaiweza? Mziki wake hadi serikali inakoma ubishi. I like hili jembe la kimachame, ni hodari na mtekelezaji na haogopi mabomu. SSM watakuwa wanashehereka sasa. Ila naomba aendelee kubaki TAMWA na awe front tu katika kupambana na utesaji wa nchi hii kwa raia na kwa wale akina mama wanaoteswa na watoto wa kike pia.
   
 16. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,751
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Lucy Nkya? ni Ananilea Nkya!- watu wawili tofauti!!!
   
 17. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,847
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Huyu mpya alishawahi kuajiriwa radio tanzania?hapo ndipo tatizo linapoanzia sababu radio tanzania sasa hivi inaitwa tbccm taifa..
   
 18. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,285
  Trophy Points: 280
  Lisije kuwa gamba tu hilo
   
 19. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CV yake imetulia, ameoshatoa Matongotongo! Sitegemei mambo ya ki RTD au sasa TBC-cm !
  kila la kheri Dada.
   
 20. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,817
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Kila la kheri Valerie Msoka
   
Loading...