Elections 2010 Ananilea Nkya amfagilia Regia Mtema

Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,701
1,799
Mkurugenzi wa TAMWA Bi Ananilea Nkya, leo katika Jambo tanzania amfagilia Regia kuwa ni mdada wa maono, anatoa upinzani mkubwa huko jimboni.
 
Ametulia kwa kweli! wanakilombero msifanye kosa kuto kumpa kura huyu dada. Mi namfagilia sana, ananikosha mpaka basi.
 
Yule dada ameiva kwa kweli, ni mtu makini na anazungumza mambo yenye akili

Hapa nayakubali maneno ya Reginald Mengi "watu wenye ulemavu wa viungo wasikae na kulia juu ya viungo vyao vilivyopotea bali watumie vile vilivyobaki au vilivyopo kujiletea na kuiletea jamii inayowazunguka maendeleo". na hii ni pamoja na kushiriki katika nyanja mbalimbali kama siasa, elimu na uchumi.

Yule Dada Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kuhimili changamoto za kimaumbile na kisiasa hasa wakati huu wa kampeni, I hope atashinda na kutoa changamoto mpya kwetu wenye viungo timilifu na walipungukiwa, na sio kubaki kulalamika.
 
Regia Mtema leo amehitimisha kampeni kwa kufanya mkutano uliovunja rekodi katika kata ya Lumemo.Watu wamemkubali sana ana mvuto kwa wapiga kura anajua matatizo yao na zaidi ya yote ana suluhisho la matatizo ya wapiga kura wake.Ni mwanamke jasiri sana anajiamini na anazungumza mambo ambayo ana uhakika nayo.Huyo ndiye mbunge wetu mtarajiwa kesho tunanampigia kura za ushindi.
 
Back
Top Bottom