Ananifanyia vituko ila nikitaka kumuacha anatishia kujiua

Hakuna mwanamke hapo, Waite wazaz wake na yeye uwachane live Kila kitu. Unaibiwa tu hapo.....kweli maisha Yana siri nyingi hayahitaji kifua Cha gym, uamuzi wa kuoa au kuacha ni wako maake wewe ndo utaishi nae. .full stop
 
Yan nimesoma nimepata hasira mbaka natetemeka wewe unataka ushauri gan apo sasa
 
Mjomba unakwama wapi aiseeeee?? Unawezaje kuhudumia familia nzima kama umeoa? mwache ili afe vizuri wewe umefanywa mgodi wa kutoa pesa na matumizi siku ukiwa huna atakublock kabisa,alafu hata kama X alikuwa anakula Enzi hizo bado anatumiwa na picha? mjomba badilika bhasi achana naye kuna wanawake wazuri hata humu Jf Zaidi ya huyo .
 
Nimeshindwa kumaliza hii story, ujinga uliopitiliza.
Huyo mke mtarajiwa atakuja kukusumbua sana maishani iwapo utaendelea naye, ukiangalia yeye ana umri mkubwa kuliko wewe hivyo suala la ndoa kwake angelipa uzito mkubwa ukizingatia yeye ni wa jinsia ya kike.

Hata hivyokwa maelezo yako hali ni kinyume chake , bado ana some reservations ambazo hataki uzibaini . Jipemuda wa kutafakari na chukua hatua stahiki. Mahari uliyolipa acha iwe sadaka
 
Kwa kweli nimesikitika sana kuona ni jinsi gani ulivyo bwege, sisi tuliopo kwenye ndoa tunakushauri kuwa makini sana siyo kila mwanamke uliyempenda lazima awe mke wako.

Huyo mwanamke bado anampenda sana x wake na ndomana anamtumia picha za uchi na pia nakuhakikishia kuwa huyo jamaa bado anaendelea kupewa mzigo.

Nakushauri achana naye jikaze kiume piga chini vinginevyo ukilogwa ukamuoa utakuja juta maishani mwako.

Dalili kubwa ya kuwa hakupendi ni kitendo cha kumlipia mahari lakini anaonekana bado hayupo tayari cha ajabu umri umekimbia. Sisi wengine kila siku tulikuwa kila saa tunaulizwa lini mahari, lini ndoa mpaka ilikuwa kero.

Akili kichwani mwako usiseme hatukukushauri. Kama unaona ni kazi kumkwepa bora hata uame mtaa unaoishi.achana naye utakuja kutushukuru
 
Naandika machache,, kama ifuatavyo

Dogo unataka kuoa mtu anaekunywa sumu?

Unaoa mtu wa kununa nuna na kumtumia x wake picha za kipochi chake!!!

Ushauri, hiyo mahari usidai achana nae, manzi ni Majanja sana kakupiga limbwata kabla hajaingia ndoani, nakuhakikishia akiingia ndoani kila rangi utaiona.
 
Mkuu umezama kabisa mapenzini,hakika hakuna cha kukushauri mpaka utakapoamka toka kwenye usingizi tororo wa mapenzi.
 
Huyo wala awezi jiua ila ana uhakika wewe ni mmoja ya watu wajinga anao wajua wajinga ndio maana ana kuzungusha kama pia!

Anajua kuwa uwezi kumuacha kwakuwa hujiamini na una moyo laini sana na unapenda kulia lia!

Muache wala awezi kujiua
 
Sioni Mwanamke wa kuoa
Sioni mwanaume rijali hapo
Wamekutana mapoyoyo tu
Pwagu na Pwaguzi wajinga
Wote ni mazezeta watupu
Ila mume ni juha punguani
Kusoma hajui, picha haoni?

Bazazi
 
Wanatumiana picha chafu halafu hakuna kitu, haingii akilini, hakuna ukaribu na X kama anakupenda kuna haja gani awasiliane na X, Kuna kitu gani kimabaki kati yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema ulienda hospitali ukakuta kweli amelazwa, je ulimuuliza dr amemkuta mgonjwa wako na tatizo gani, wakati anakunywa hiyo sumu hakika alikua na X wake maana kama angekua ni mwenyewe angeshakufa, changanua mzee mbona mambo yapo wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom