Ananifanyia vituko ila nikitaka kumuacha anatishia kujiua

maddox

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,311
2,741
Mimi ni kijana wa miaka 30, sijaoa lakini niko kwenye mahusiano na Dada mmoja ni mwaka wa nne sasa. Nina kazi nzuri tu na kipato kizuri na kwakweli najitahidi kumhudumia huyu Dada kwa kila kitu. Yeye anafanya kazi lakini hata siku moja sijawahi kumuulizia kuhusu pesa yake. Hatuishi pamoja, yeye bado anaishi kwao lakini matumizi yote ya nyumbani kwao mimi ndiyo natoa.

Anaishi na wazazi wake wote ila ananiambia kuwa kwakua mimi ni mpenzi wake natakiwa kumhudumia na kwakua anaishi kwao basi ni lazima kuwahudumia na wazazi wake kwani hawezi kujinunulia chakula peke yake. Basi mimi hilo sina shida nalo kwani kama mwanaume naona kama ni majukumu yangu. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, huyu mwanamke bado hajamsahau X wake.

X wake ameoa lakini kila akigombana na mke wake anamtafuta mpenzi wangu wanaongea, nikimuuliza kwanini unaongea naye ananiambia ni urafiki tu kisha ananinunia hata wiki mpaka mimi ndiyo nimuombe msamaha. Niliamua kumpigia X wake na kumuambia kuwa yeye si anandoa basi aniachie mwanamke wangu lakini aliniambia kuwa hana mpango naye alishamuacha ila mimi ndiyo niongee na mtu wangu.

Shida inakuja hivi, baada ya mimi kuongea na X wake basi amebadilika, amekua mtu wa hasira na kila siku ananiambia kuwa tuachane. Ananiambia kuwa nimemdhalilisha kuwa kwa mimi kumpigia X wake ni kama nimemuita yeye malaya kuwa anarudia matapishi ili tuachane. Alilazimisha sana tuachane, akakata mawasiliano kabisa na mimi, kwakua nampenda basi niliamua kwenda kwa wazazi wake na kuwaambia ili waongee naye.

Niliwaambia kuwa nipo tayari kumuoa wakati wowote, wazazi wake waliongea naye na kweli alinisamehe. Basi niliona ili nisimpoteze na kumziba X wake nitoe mahari moja kwa moja, nilitoa mahari ingawa ishu ya ndoa aliniambia kuwa yeye bado hajajipanga lakini niliona kwa kutoa mahari basi atakua wangu.

Lakini haikua hivyo Kaka, pamoja na kutoa mahari ndiyo alibadilika zaidi, yaani amekua mtu wa hasira, amekua mtu wa kununa nuna sijui hata nifanyeje. Kuna wakati nilijikuta nakasirika na kumuambia kuwa bora tuachane kwani nimechoka, nikamtafuta mshenga na kumuambia ukweli kuwa nimechoka nataka aende kuwaambia wazazi wake kuwa nimechoka nataka kuachana naye, kweli nilikua nimechoka na nilipanga kumuacha.

Lakini baada ya kuona nimemtafuta mshenga aliniambia kuwa namdhalilisha kumtolea mahari kisha kumuacha. Alinizimia simu, nilikuja kupigiwa simu baadaye na X wake kuwa anataka kujiua na kanywa sumu wako hospitalini. Nilikua na hasira lakini nilienda na kwelia likua kalazwa hospitalini, alinilaumu mimi kuwa nimemdhalilisha kwani nikimuacha nisipomuoa hatapata mwanaume mwingine wa kumuoa.

Ana mika 32, kusema kweli nampenda na nipo tayari kumuoa, lakini nashindwa kujua kama ananipenda kweli au la. Ananiambia ananipenda ni mimi tu sijiamini yeye hana chochote na X wake ni marafiki tu lakini nilishawahi kuona anamtumia mpaka picha za uchi X wake, nikimuuliza ananiambia kwani kuna ubaya gani kama ni kumuona alishamuona kila kitu hakuna jipya, nimechanganyikiwa.

Kuna mambo mengi sana ambayo nashindwa kuyaongea, ubaya nikuwa, kila mtu sasa hivi ananilaumu mimi kwakua nimemuacha lakini hawajui mambo ninayopitia. Mimi kama mwanaume kuna mambo siwezi kuwaambia ndugu zangu wala ndugu zake, wao wanajua nimemuacha tu namharibia maisha yake lakini ukweli nashindwa kuamua kuwa huyu mtu ananipenda au vipi, nisaidie ushauri wako.

Nimeikuta sehemu nami nawasilisha.
 
Braza Achana na Hiloo Jike Shupaaa!

Nasemaaa kama unaweza kusamehe mahari samehee achana nalooo mapemaaa sanaa yani Ex wake ni bora mara 1000 moyoni mwake kuliko wewe mtarajiwa wake so piga chini mkuuu kama sumu linywee tuu kuliko kumuoa kwa huruma yako huko Mbele UTAJUTAAAA NA SEMA UTAJUTAAAAAA. UTAJUTAAAAA NARUDIA UTAJUTAAAAAA.
 
Ujue kuwa bado anampenda X wake na kuna uwezekano mkubwa huwa wanakutana na kunyanduana maana so kwa hatua ya urafiki wa kawaida wa kumtumka picha za utupu X wake alafu anakwambia ni kawaida.

Ni mtu mzima lakini hajielewi, miaka 32 anakwambia swala la ndoa bado? Don't you see the bad tricks she plays you ili aendelee kisirisiri na huyo X wake?

Nakushauri umuache angalia maisha yako, vinginevyo unakaribisha presha ya bure kwa kusalitiwa na kununiwa nuniwa ndani ya nyumba.
 
Ujue kuwa bado anampenda X wake na kuna uwezekano mkubwa huwa wanakutana na kunyanduana maana so kwa hatua ya urafiki wa kawaida wa kumtumka picha za utupu X wake alafu anakwambia ni kawaida..
Hamna mapenzi. She is just toxic person. Anaenjoy unavyompa attention. Na usipoangilia atakupotezea muda tu. Kaza moyo achana nae.
 
Braza Achana na Hiloo Jike Shupaaa.

Nasemaaa kama unaweza kusamehe mahari samehee Achana nalooo mapemaaa sanaa yani Ex wake ni bora mara 1000 moyoni mwake kuliko wewe mtarajiwa wake so piga chini mkuuu kama sumu linywee tuu kuliko Kumuoa kwa huruma yako huko Mbele UTAJUTAAAA NA SEMA UTAJUTAAAAAA...UTAJUTAAAAA NARUDIA UTAJUTAAAAAA.

Sasa baba rikiboy mwenzetu hela zimemtoka si kidogo, unamshauri apige chini? Kaka!😇😇
 
Kwanza kaka nakusikitikia sana kuangukia kwa hilo Shangingi.

Halafu nikuchane tu ukweli huyo mwanamke hana mapenzi ya dhati na wewe bali yuko kimaslahi zaidi na anakuchukulia wewe amekupata bwege lake.

Maana nimeshangaa sana pale uliposema unawahudumia nyumbani kwao hali ya kuwa hata bado hamjaoana.

Halafu unahudumia na bado anakutesa tabu yote ya nini na wanawake wamejazana kila kona wanatafuta wenza wa kuishi nao,unamganda hilo lishangingi lisilo na shukrani.

Hivyo anavyokutishia kunywa sumu ni mbinu ya kukuchanganya tu aendelee kukuvuna pesa zako maana anajua hawezi kumpata bwege mwingine wa kutoa hela zake kirahisi hivyo labda akamtafute Namtumbo au Koromije huko.

Neno langu la mwisho kwako ukija kujichanganya ukamuoa huyo mwanamke utaishi kwa mateso miaka yote hadi unaingia kaburini.
 
Ingawaje bado maamuzi ya mwisho juu ya hili yako juu yako ila for sure huyu hana nia nzuri na ww na ukichunguza kwa undani nahisi kuna kitu ameahidiwa na X wake so huenda kwako anazuga kusikilizia na ndio maana kwako yuko robo robo.

Still nadhani una nafasi nzuri ya kusubiri utakayematch naye, shida wengi mnadhani kuwa ukimpenda tu mtu basi unaweza kuishi naye vizuri ndani.

Are you happy with that relationship huwa hamtaki kuangalia hili ni kweli happiness come from within you but putting yourself in negative environment will distract you na si nzuri kiafya.

Nature doesn't hurry so nakushauri wait for someone you will match unless km unaona hapo ulipo kuna dalili za kubadilika. Always kumbuka ukimkuta mtu na tabia yake huwez kumbadili ila hadi atakapoamua kubadilika yeye. Wishing you well bro.

Best Regards
Ladam
 
One of the worst case.

Yaani mwanaume mwenzangu unaniangusha.

Siku ya msiba wako usisahau kutualika
 
Mimi nimefika nusu nikaacha kuendelea kusoma. Kiufupi huyo dem ndo kamtoa jamaa bikra sasa jamaa ukichukulia domo zege atapata wapi wa kufanana naye?
 
Jiulize, Kama kwenye uchumba tu mnagombana kiasi hiki kwenye ndoa si kila siku mtakuwa wa wakusuluhishwa?.
Huyo sio mtu sahihi, atakusumbua. Kama anajiua wewe sio mwokozi wake.
 
Back
Top Bottom