Anamuacha mke wake!

Bi. Senti 50

JF-Expert Member
Apr 17, 2007
290
12
Sijui kama ndiyo jambo limezua jambo au nini. Tuliporudi toka ile ziara ya Ulaya, mheshimiwa akawa yuko kimya kwa muda. Walipokuja Dodoma akawa ananitafuta na mimi nikawa namkwepa sana. Hata hivyo jana alipata nafasi ya kustop ofisini na akaniomba niende naye lunch. Kiufupi kaniambia kuwa yeye na mkewe wameamua kuachana.

Nikamuuliza kwanini ananiambia mimi? akasema alitaka nijue tu ili nitambue kuwa ni kweli ananipenda na yuko tayari kuwa nami. Sasa feelings zangu zimechanganyikiwa kweli kwani nilifuata ushauri wenu nilimuachia ndege aruke, sasa karudi, nimnase?

asante.
 
Ukiona mwenzio kanyolewa wewe tia maji" mwambiye mukapime HIV, atakupenda kwa muda tu, akishakinaiwa ndo basi, ataenda kwa mwingine, kitu kipya na atamweleza " kuwa yeye na mkewe/wewe wameamua kuachana.
naye atamuliza kwanini?

kwa vile sasa hivi kua viagra, atandelea hivyo hivyo mpaka atapokwaa UKIMWI
 
WARNING!!!

ikiwa Yeye Kamuacha Mke Wake Nawe Muache Mara Moja Tapeli Huyo, Siku Moja Atakuacha Na Kwenda Kwa Mwingine Na Atajinadi Kama Aliyofanya Kwako.

WARNING!!!​
 
Sijui kama ndiyo jambo limezua jambo au nini. Tuliporudi toka ile ziara ya Ulaya, mheshimiwa akawa yuko kimya kwa muda. Walipokuja Dodoma akawa ananitafuta na mimi nikawa namkwepa sana. Hata hivyo jana alipata nafasi ya kustop ofisini na akaniomba niende naye lunch. Kiufupi kaniambia kuwa yeye na mkewe wameamua kuachana.

Nikamuuliza kwanini ananiambia mimi? akasema alitaka nijue tu ili nitambue kuwa ni kweli ananipenda na yuko tayari kuwa nami. Sasa feelings zangu zimechanganyikiwa kweli kwani nilifuata ushauri wenu nilimuachia ndege aruke, sasa karudi, nimnase?

asante.

Umnase ndege hata hujui kwa nini anaachana na mkewe? :confused:
Kama wanaachana kwa sababu ana ukimwi bado utataka tu kumnasa? angalia usije ukanaswa wewe!!!!
 
Ushauri uliotolewa hapo juu nadhani ni wa busara, other things being constant-preference inaonekana kuchukua mkondo wake. Sasa kama wewe una range ya B katika choice kuliko A(aliyeachwa), then C might also be preffered to B. Hvy ukiachwa nawe jua kuwa preference bado ina-take place na usije-complain sana.
 
Kuna ndege halafu kuna midege, tena mingine midege ya jeshi, meli za sumu zilizobeba vikosi vya mizinga.

Just be sure which is which before embarking.
 
Kuna mengi ya kuulliza kabla ya kumhukumu huyo anayeacha mkewe, je maisha yao yakoje? walioana kivipi? uaminifu ukoje hata kwa upande wa pili, kuna matatizo yoyote ya tendo etc. etc.

Kuna watu tumewaona wameoa tena na wakawa na maisha mazuri zaidi kiuchumi, kijamii na kiimani. Lazima watu waangalie pande zote, sio kila kitu ni "kama ilivyoandikwa"
 
Sijui kama ndiyo jambo limezua jambo au nini. Tuliporudi toka ile ziara ya Ulaya, mheshimiwa akawa yuko kimya kwa muda. Walipokuja Dodoma akawa ananitafuta na mimi nikawa namkwepa sana. Hata hivyo jana alipata nafasi ya kustop ofisini na akaniomba niende naye lunch. Kiufupi kaniambia kuwa yeye na mkewe wameamua kuachana.

Nikamuuliza kwanini ananiambia mimi? akasema alitaka nijue tu ili nitambue kuwa ni kweli ananipenda na yuko tayari kuwa nami. Sasa feelings zangu zimechanganyikiwa kweli kwani nilifuata ushauri wenu nilimuachia ndege aruke, sasa karudi, nimnase?

asante.

Umempata au ndio umepatikana?
 
Bi. Senti 50, nakushauri USIMNASE huyo ndege bali JINASUE na kama umeshanaswa tayari JIKWAMUE na KUJIKOMBOA. Kwa kusoma ujumbe wako nahisi unawekewa mitego ili unaswe wewe. Kumbuka majuto ni mjukuu!!!!
 
... nilimuachia ndege aruke, sasa karudi, nimnase?
asante.

Ukimwachia ndege huyo utabaki unasikitika tu, na chochote utakachofanya badala ya kuchangamkia ndege sana sana ni ubatili. Ukimnasa ndege huyo utakachoambulia mwisho wa siku ni ubatili.

“Ni ubatili, ni ubatili!...ubatili mtupu! Kila kitu ni ubatili. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyajo chini ya jua?”
 
ndiyo ni "ubatili na kufukuza upepo"...
 
nilifuata ushauri wenu nilimuachia ndege aruke, sasa karudi, nimnase?

asante.

...ule ushauri ushapitwa na wakati, si unaona hata expirery date yake?

we mnase tu, "a bird in hand worth two in a bush!"

mnase umkamate kisawasawa, licha ya kumsahau mtalaka wake, hata wanawe pia awasahau!!!
 
1+1 haiwezi jibu likawa 1, cha msingi akili kichwani mwako maaana mwenzio alishanyolewa sasa uwe makini kuweka zako maji kabla hayajajirudi. Naaamini Mapenzi ni suala gumu sana hasa kwenye ushauri unaweza ukapotoshwa au kuongozwa. Angalia Moyo wako unataka nini na isiwe kwa tamaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom