Anamjali mama yake kupita kiasi……………….

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Inatokea kwenye ndoa nyingi, ambapo unakuta mume anamjali mama yake kuliko mkewe. Kumjali nina maana kwamba, yuko tayari kupinda haki, kumuumiza mkewe, kumchukia na kumfanyia visa kwa sababu ya kumridhisha mama yake.

Kwa mfano, mama kumtukana mke na mume kumwomba mke avumilie tu, mama kusema maneno ya umbeya dhidi ya mke, na mume kuyatilia maanani, mama kumtaka mwanaye amchukie mkewe na mwanaye kufanya hivyo na mengine ya aina hiyo.
Hebu fikiria kwamba hiyo imekutokea wewe. Je ungefanyaje?
 
mmmmh hapa pagumu, mama nampenda na mke nampenda. Dawa ni kuwaweka mbali mbali kadri inavyowezekana
 
Njoo nikuoe hapa; mpwa hao bado ni ndugu usijaribu kuutenganisha undugu wao hata hivyo nashauri kuwa, jaribu kuwa karibu na mumeo na kisha jiepushe sana na huyo mkweo, umeskia eeeh maana sijui ulikua wapi hadi mama mkwe anajenga ukaribu na mwanae kiasi hicho kwene nyumba yenu! Pole na mimi nimeshoana vituko vya namna hio mahali fulani! Ndoa ndoano ati!
 
title ya thread ni tofauti na maudhui. mwanaume asiyemjali mama yake na ndugu zake wala hafai kuwa mume. lakini mwanaume anayekubali mkewe kuonewa na mama yake,na kusemewa maneno ya uongo akaamini,yeye ana kasoro kubwa. nahisi kasoro hizi sio kwa mama yake tu,bali hata kwa mahusiano mengine aliyonayo.mh,,kazi kweli. bibie hakusoma alama za nyakati?
 
Nimekupata AshaDii, nitaisoma............... Ahsante sana
 
mama ana nafasi yake na mke naye ana nafasi yake........inakuaje mwanaume unamjali mama yako kuliko mkeo????????...
 
Mama muhimu zaidi na daima ubaki kuwa1 tu mke ukimpoteza wako wengine watakuja tu muhimu wajengee maelewano
 
Ni vizuri mume akimjali mama yake na ndugu zake kwani wana nafasi kubwa tu katika maisha yake ila na mke naye ana nafasi kubwa na muhimu sana ndio maana mume pamoja na kuwa na mama na ndugu wengine bado alitafuta mke. Akumbuke kuwa yeye ndio kiunganishi cha mkewe na ndugu zake,akimheshimu,kumthamini,kum defend na kumlinda hata ndugu zake watamheshimu pia. Huyo mume ndio tatizo,jaribu kuongea nae kama bado hujafanya hivyo.
 
AshaDii, samahani nimeshindwa ku-attach swali lako kutokana na mtandao kuwa down....... lakini nitakujibu kama ifuatavyo:

kama ni mimi Mtambuzi, kwanza kabisa, naomba ukubaliane na mimi kuwa yule ni mama yangu na atabaki kuwa mama yangu, lakini pia mke anayo nafasi yake kwangu na anazo haki zake kwangu, kwa wale wasomaji wa vitabu vya dini watakubaliana nami kuwa katika kitabu cha KIKRISTO. I mean Bible imebaishwa kwamba mtoto atawaacha wazazi wake na kwenda kuanza maisha na mkewe au mumewe, kama ilivyokuwa kwa mama na baba yako, waliwaacha wazazi wao na kuishi pamoja na kutengeneza familia, sasa iweje aniletee KIDAMISI KWENYE NDOA YANGU?

Nitakuwa muwazi, maana kama nitamuendekeza atanivurugia ndoa yangu, nitamwambia ukweli kama atakuwa na nia ya kutaka kuivuruga ndoa yangu, na kama mke wangu ndiye mwenye tatizo, itabidi nichunguze ili nijue sababu, na nikishajua sababu, bila shaka nitajua namna ya kulitatua.

Mama anayo nafasi yake kama mama na si vinginevyo........

Nadhani nimekujibu.
 
Nimependa saaana ulivo nijibu... Na worry not about being quoted...
 
kila kitu kina wakati na muda wake .. na pia kila mmoja ana umuhimu na nafasi yake kwa wakati wake
 
Back
Top Bottom