Kasimba G
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 3,428
- 2,609
Kuna semi nyingi huwa tunazikuta humu majamvini juu ya matabaka na ukanda, lakini mala nyingi hoja hizi huibuliwa na wapenzi na mashabiki wa CCM, Sasa mimi nimekuwa nikitafakari kwa kina juu ya hoja hizi nikihusanisha na muonekano dhahili ndani ya jamii yetu, haswa kwa kuzingatia miundo ya vyama hivi hasimu vikubwa zaidi hapa kwetu Tanzania.
Kwanza, nikagundua kuwa kuna hoja kuwa CHADEMA ni chama cha kaskazini, kwa hoja hii nikajaribu kupitia makabrasha na kugundua kuwa ni afadhali kungekuwa na hoja kuwa CHADEMA ni chama cha kanda ya ziwa. Nasema hivi kwa nini? Ukiangalia mgawanyo wa wabunge utakuta wengi zaidi wametokea kanda hii mashuhuri kisiasa! Mfano ulio hai ni mkoa kama Simiyu nadhani asilimia 90 ni CHADEMA, sasa hoja ya kanda ya kaskazini inatoka wapi?
Huenda wajenga hoja labda wanachoangalia ni ngazi za viongozi wa juu kuwa mwenyekiti katoka huko na katibu mkuu katoka huko! Lakini je uongozi kabla ulikuwaje? Mbona kulikuwa hamna top wa huko?
Propaganda hizi zimeshika kasi na bahati mbaya watu wasio watafiti wanajikuwa outomatically wanaingia kwenye hoja hii dhaifu! CHADEMA mala nyingi hawajengi hoja za kutenganisha watanzania kama jinsi mahasimu wao CCM wanavyoona inafaa kwao na wanaiona ni hoja yenye mashiko kwao, labda ni kwa kuwa iliwahi kuwasaidia katika kipindi kilichopita, nakumbuka wakati Augustine Mrema akiwa kwenye CHati vilevile NCCR ilikuwa ni chama cha wachaga, na chama cha kaskazini!
Nonana kwa mtazamo wangu kama taifa inabidi hoja mfu za kutenganisha watu zipigwe marufuku!