Analysis ya Wanasiasa Vifo vya Magonjwa na Mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Analysis ya Wanasiasa Vifo vya Magonjwa na Mgomo wa Madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jodoki Kalimilo, Apr 16, 2012.

 1. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,645
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Ukiwa mwanasiasa hasa Tanzania, usipokuwa makini hata kama una PHD uwezo wako wa kuainisha mambo unakuwa wa chini kushinda wazee wa kimila ambao role yao ni kushauri jamii yao. Wiki iliyopita nilikuwa nasikiliza bunge nikashangaa kumsikia naibu waziri akisema mgomo wa madaktari haukusababisha vifo vya wagonjwa kwa kigezo kwamba takwimu zilizochukiliwa kutoka Muhimbili ambako ndiko waligoma sana zimeonyesha vifo vilivyotokea kipindi cha mgomo vina uwiano sawa na vifo vilivyotokea kipindi cha nyuma kwani alisema idadi yake kwa siku ni kama inafanana. HAPA NILISHANGAA KWA JINSI ANAVYOZUNGUMZIA TAKWIMU YA VIFO KAMA VILE ANAZUNGUMZIA MAKADIRIO YA IDADI YA WATU AU WANYAMA MAANA LENGO LA HOSPITALI NI KUPUNGUZA VIFO KUWA CHINI IWEZEKANAVYO, ANAVYOSEMA HIVYO MAANA YAKE HAKUNA MKAKATI WOWOTE WA KUPUNGUZA VIFO, ndo maana anasema takwimu hazitofautiani sana kama siku zilizopita.

  Hapa wanaJF mnasemaje, naomba kuwakilisha
   
Loading...