ANALYSIS: CCM cadres’ new book revisits Mkapa’s troubled legacy

WASHINGTON - Former White House press secretary Scott McClellan blames President Bush and Vice President Dick Cheney for efforts to mislead the public about the role of White House aides in leaking the identity of a CIA operative.

In an excerpt from his forthcoming book, McClellan recount the 2003 news conference in which he told reporters that aides Karl Rove and I. Lewis "Scooter" Libby were "not involved" in the leak involving operative Valerie Plame.

"There was one problem. It was not true," McClellan writes, according to a brief excerpt released Monday. "I had unknowingly passed along false information. And five of the highest-ranking officials in the administration were involved in my doing so: Rove, Libby, the vice president, the president's chief of staff and the president himself."


Mkuuu Bubu,

Huu wa huyu mkuu ndio ushujaaa, maana anamsema Bush, akiwa bado rais yani madarakani, sio kusubiri amekosa mlo kama kina Butiku, hapana mkuu anampa Bush vipande vyake live tena bado akiwa kwenye power liwalo na liwe,

Hawa kina Butiku, matatizo yao ya binafsi wanataka kutuingiza taifa zima, NO! wangeandika kitabu kuhusu mapungufu ya katiba then tungeeelewa kwa wana uchungu na taifa, lakini eti gossip ndani ya CCM, yaani hiyo ndio hasa tunaita NONESENSE!
 
Mkuu, Mkapa aliiga kila kitu kwa Nyerere sasa ilikuwaje Mwalimu alikuwa ameshaanza kuonyesha kupinga sera za Mkapa? Je Mkapa aliiga hata kujilimbikizia mali, kusaini mikataba mibovu, kufanya biashara akiwa Ikulu kwa Mwalimu Nyerere!?

Nimeshasema mara nyingi hapa ukumbini Nyerere hakuwa perfect hata yeye mwenyewe aliwahi kutamka hivyo, lakini kumlinganisha na fisadi Mkapa, kwa maoni yangu Nyerere ni malaika bila wasi wasi wowote. Ufisadi alioufanya Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani huwezi kabisa ukaulinganisha na mabaya yote aliyoyafanya Nyerere alipokuwa madarakani kwa miaka 24

Mkuu Bubu,

Tunachokataa ni ujanja ujanja wa watu kukosa mlo na kujaribu kutudanganya taifa zima kuhusu matatizo yetu, kati wa waliyoandika kwenye hicho kitabu tatizo letu hasa as taifa ni moja tu nalo ni mapungufu ya katiba, wewe unayoyaongelea sio wanayoyaongelea kina Butiku, Mwalimu was the greatest hilo halina ubishi, tatizo tu ni kwamba kina Butiku wanajaribu kumlaumu the wrong person kwa matatizo ya ndani ya CCM, ambayo ukweli ni kwamba yalianzia kwa Mwalimu, Mkapa aliyaiga tu,

Tunashindwa kumpa sifa Butiku na kitabu chake kwa sababu yeye alikuwa na nafasi nzito sana serikalini as number two, zamani huyu alikuwa akiwatisha sana viongozi wakuu na alikuwa very abusive kwa viongozi, katiba mpya ilianza kutumika 1977 mpaka 1984, Butiku akiwa number two hakuiona kuwa ina kasoro? Butiku alikuwa na nafasi ya kuleta mabadiliko muhimu sana kwa taifa, lakini kwa sababu alikuwa kwenye mlo hakuyaona matatizo, sasa baada ya kukosa mlo ndio ameyaona? Ndio tunaita unafiki huuu hatuutaki, sasa wananchi tumeamuka sio tena yale mambo ya kutudanganya tuu, tunasema hapana mambo ya mageuzi wawaachie kina Zitto, wasioogopa, Butiku apeleke matatizo yake huko CCM!
 
Mkuu tuweke milango wazi bila kujali watu kama wamenyimwa mlo au wamepewa mlo ili kuanika maovu mabli mbali ndani ya chama au siri kali. Hawa wanaoyaandika haya wanayaandika kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania na hivyo yanaweza kabisa kusaidia kupunguza maovu ndani ya chama na sirikali kwa kuwa viongozi watakuwa na wasiwasi kwamba maovu yao yanaweza kuanikwa hadharani. Vinginevyo tutawatisha watu wanyamaze kimya hata wanaposhuhudia maovu. Always remember not to shoot the messenger
 
Si vibaya kuurudisha huu mjadala ukurasa wa mbele.
 
Ninaposoma kuwa kuna watu wanatetea utawala wa Mkapa, ukweli huwa nasikia kizunguzungu sana. Ni kweli kuwa kuna makosa yatokanayo na upungufu wa kibinadamu ambayo ni vigumu mtu mwenyewe kuyathibiti. Mkapa alikuwa nalo moja la namna hiyo kama vile kile kiburi chake cha kuamaini kuwa yeye ndiye mwenye akili tu na wengine wote wasiokubaliana naye ni wajinga; na tabia hii alikuwa nayo tangu hata kabla hajawa rais. Nadhani sote tunakumbuka onyo lililotolewa na balozi Mwakasakufya (sina uhakika na spelling) aliyewahi kufanya naye kazi kwa muda mrefu sana kuhusu tabi hiyo hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 1995. Makosa haya bado anaweza kuyafanya hadi leo hata kama hayuko madarakani kwa vile hayo ni inherent kwake

Hata hivyo makosa tunayomlaumu bwana Mkapa siyo ya aina hiyo, bali yale aliyofanya kwa makusudi huku akijua kuwa ni makosa ila kwa vile alikuwa na madaraka hakuna ambaye angemfanya lolote; ni makosa ya dhidi ya ethics za madaraka aliyokuwa amekabidhiwa. Na kwa vile madaraka hayo ndiyo yalikuwa ultimate, yaani hakuna zaidi yake, ni lazima tutamlamu sana kwa vile makosa yake yaliitia nchi hii katika matatazio makubwa sana kwa kipindi cha miaka mingi ijayo. Sitaki kuyataja makosa hayo kwa vile yameshaandikwa sana na yote yameacha athari ambazo zitavikumba vizazi na vizazi vijavyo.

Si sahihi kujaribu kumtetea Mkapa kwa kumlumu Nyerere kwa vile Mkapa aliaza kuvuruga nchi baada ya Nyerere kufariki na kuwa ameoshaondoka madarakani takriban miaka kumi na tano. Wakati Nyerere akiwa hai, Mkapa alikuwa anazingatia sana maadili yake ya kazi (japo kwa kinafiki.) Tangu Nyerere atoke madarakani, kuna matukio mengi duniani hapa ambayo yamebadili sana mwelekeo wa uchumi wa dunia, la muhimu likiwa ni lile la kuisha kwa vita baridi. Kama bwana Mkapa ndiye angekuwa kiongozi wa nchi hii wakati wa vita baridi, sina wasiwasi kuwa huenda bwana huyu angekuwa kama Mobutu tu.
 
Sasa yupi ana manufaa kwa taifa, mtu aliyekosa "mlo" akaamua kuyaweka maovu ya waliomnyima "mlo" hadharani au aliyekosa "mlo" akaamua kujichimbia kwenye shughuli zake binafsi na kuachana na wale waliomnyima "mlo"?.
 
Duh, yaani inasikitisha sana kuona haya yaliyoandikwa humu..
Ama kweli safari ndefu sana..
Kuna rafiki yangu ana matatizo na mkewe sasa matusi yote kati yao hurudi hati kwa mababu na jinsi walivyolelewa. Hakika mimi binafsi nikiangalia matatizo yao na tofauti zao zinatokjana na wao wenyewe kuwa limbukeni wa maisha waliyokuwa nayo. Wameshindwa kabisa kujitazama wao ili wapate kuyaona mapungufu yao badala yake mazungumzo makubwa ni hali za familia zao kabla hawajaoana..Kila mmoja wao anaona ujanja kutafuta sababu nje ya yeye mwenyewe kuwa ndio tatizo.
Come to think of it nadhani hii ni hulka ya Wadanganyika maanake naiona kila sehemu..

Haya ndio yanayoendelea hapa JF hivi sasa na hakika hakuna suluhisho ktk jamii yetu.
 
Hapa kazi kweli kweli.
Mkuu FMES heshima mkuu,
Sasa kitabu kimeshatoka na kiko mitaani. Unaonaje ukitunga chako ukieleza pointi zako hizo ili uvunje nguvu ya kitabu kilichotangulia?
Ni kweli ninakubali kabisa kwamba BWM mkapa kwa ujumla wake yako mengi sana aliyoyafanya na hatutokwenda kuyasahau.
Lakini pia ni ukweli ulio dhahili kwamba yako mabaya aliyoyafanya ambayo atahukumiwa kwayo.
Hata hivyo ni hulka ya mwanadamu kutenda mema na kujiadhali asitende mabaya. Na mwanadamu u wheigh ni mabaya kiasi gani na mazuri kiasi gani umefanya kisha yanayozidi mengine ubebwa. Sasa kwa BWM iweje? ebu tupime kwa hayo basi ili tutoe hukumu ya haki.
 
Back
Top Bottom