Analoshindwa Putin aliliweza Magufuli kwa kutumia zawadi ya tausi watatu kwa Museveni na Kenyatta

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Video ya Vladmir Putin akihojiwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya magharibi inatembea mitandaoni. Putin anajitahidi sana kujenga hoja za kujibu maswali lakini kama kawaida yake anarudia makosa yale yale ya miaka yote. Putin aidha hana team nzuri ya Diplomasia au anaogopwa na wasaidizi wake ambao ni mawaziri wa Mambo ya nje wote aliowatumia tangu awe rais kwa mara ya kwanza mwaka 1999.

Putin anatumia nguvu kutaka Ukraine iwe karibu na Russia. Anataka kulazimisha wakati majibu atakayoyapata kutoka kwa Ukraine ni mepesi tu, sisi ni nchi huru wenye kuweza kufanya maamuzi yoyote muda wowote ule. Kwenye diplomasia kawaida nchi haitakiwi kulazimisha upendo au ridhaa ya mwingine. Ni mwendo wa ushawishi na nguvu ya kujenga hoja ndio inayotakiwa.

Hayati Boris Yeltsin ndio alikuwa kinara wa mahusiano ya kimataifa. Sauti yake akiongea ya mtu mlevi iliwachekesha viongozi mbalimbali wa wakati ule,. Ulevi wake wa pombe kali ulimpatia umaarufu haswa zile video zake zikimuonyesha akiwa na uso mwekundu akiwa kalewa chakali. Lilipokuja suala la diplomasia aliweza kuitawala Ukraine pasipo kulazimika kutumia majeshi.

Yeltsin alikuwa na mtu mmoja mahiri sana katika masuala ya diplomasia akiitwa Victor Stepanovich Chernomyrdin akiwa ni waziri wa mambo ya nje wa wakati ule. Asingeweza kusikika akiichimba mkwara Ukraine. Wala Russia isingeweza hata siku moja kulazimika kupiga mizinga kule Odessa. Silaha ya uhakika iliyoiweka Ukraine karibu na Russia ilikuwa ni nyepesi sana inaitwa 'nyama ya ulimi' waingereza wanaiita convincing powers, ukipenda unaweza ukaiita nguvu ya hoja. Unamteka mtu kwa hoja tu kwa kuyapangilia maneno mazuri mpaka anatulia na anakuwa upande wako kwa kila kitu.

Tanzania imeweza kudumu na umaarufu wake kimataifa ikibebwa na uteuzi mahiri unaofanywa na marais wa mawaziri wa mambo ya nje. Kuanzia RIP Mkapa alivyomuamini Kikwete kama waziri wake wa mambo ya nje. Akaja Kikwete akamwamini Benard Membe kama waziri wake wa mambo ya nje. Akaja JPM akamwamini Profesa Kabudi. Na sasa SSH anavyomuamini na kumtumia Mama Mulamula.

Jinsi Putin anavyoishindwa hii tasnia nzima ya mahusiano ya kimataifa ananikumbusha ile mbinu ambayo RIP Magufuli aliitumia ya kuwavuta kwake marais wa Kenya na Uganda kwa kuwapa ndege aina ya tausi. Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza asielewe maana ya wale ndege. Lakini leo unampa tausi Mzee Museveni halafu kesho anakupa mradi wa kupitisha bomba la mafuta lenye urefu wa maelfu ya kilomita litakalotoa ajira nyingi za moja kwa moja.

Leo unampa tausi Kenyatta halafu kesho likitokea tatizo la kidiplomasia anakuwa wa kwanza kusema sisi ni majirani tusiokuwa na shida yoyote katika uhusiano wetu. Hiyo ni nguvu ya kidiplomasia ambayo Tanzania siku zote tunajua kutengeneza misingi ya kuiweza lakini cha ajabu Russia na ukubwa wa taifa walionao wanaonekana kuishindwa. Putin angeweza kabisa kumvuta karibu Ukraine kama ambavyo Yeltsin aliweza lakini hana maarifa hayo. Anaishia kutungua ndege za Uholanzi zinazokatiza juu ya anga la Ukraine na kutengeneza uhasama na taifa la mbali kabisa kwa kutaka tu kumtawala jirani.

Hayati JPM ulale mahali pema peponi, umenikumbusha maana ya wale tausi. Kwa wakati ule sikuona ni ishara zipi zilizojificha katika kitendo kile, ila baada ya kutazama namna Russia wanavyoshindwa kulinda utawala wa mataifa ya jirani yake ndio naelewa ujumbe mpana wa zawadi ya tausi kwa majirani wetu wawili wa kaskazini.
 
Unafananisha ukraine na uganda au rwanda......
UsA anawafitinisha ili auze gasi ulaya.....lakini pia france alianza chokochoko za kuanzisha military alliance yao ili wasiwe tegemezi kwa NATO,....... Sasa USA anawagombanisha ili waone NATO ndio kimbilio
 
Haya masuala hayakuanzia hapo ulipoyaanzia, yameanzia parefu. Ukianza hapo ulipoanzia utaona Urusi ina makosa.

Mgogoro huu inakubidi uanzie kwenye vita baridi. Uje mpaka kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti. Uangalie uhasama baina yao. Uangalie makubaliano yapi waliekeana na NaTO (pande zote mbili Urusi na NATO) baada ya Umoja wa Kisovieti kuvunjika.

Bunge la Senate la US lilitoa mustakabali wao US na Urusi ni upi! Mustakabali walioutoa Urusi ni Taifa adui kwao. Inabidi uangalie mikataba ya kiusalama dhidi ya silaha za kivita waliyoingia US na Urusi ili amani iwepo. Kisha ufuatilie na mambo yanayoendelea baina yao kwa ujumla; yaani West na Urusi.

Baada ya hapo utajua ukweli ni upi na uongo ni upi!
 
Ujerumani na Urusi naweza kusema wana historia mbaya baina yao hususani ukiangalia WW2. Mfano battle of stalingrad. Ni moja ya pambano baya sana yenye unyama mkubwa sana lililopiganwa baina ya Urusi na Ujerumani ya Hitler kuliko pambano lolote lililopiganwa kwenye WW2.

Ujerumani ilipeleka wanajeshi millioni 1, vifaru 1700 na ndege jeshi 2000. Zote kwa uelekeo mmoja kwa wakati mmoja zilielekea Urusi kuiweka Moscow chini ya Ujerumani. Ni jeshi kubwa ambalo Mjerumani hakupeleka sehemu yoyote isipokuwa Urusi. Kwa hili, Urusi ilipoteza wanajeshi na raia waliyojitolea kupambana na Ujerumani millioni 1+.. Ni sacrifice kubwa haikutokea mahala popote duniani kwenye hii vita isipokuwa Urusi tu.

Hii ni historia, inabeba maumivu na inabeba hisia. Wakati mwengine in a we za kubeba uhasama baina ya hizo nchi ikiwa juhudi za kimakusudi zisipochukuliwa ili kusameheana kwa kujenga urafiki na kusonga mbele.

Ujerumani analifahamu hili! Hivyo hataki kuingia mgogoro wa aina yoyote utakaoleta mkwaruzano mkubwa kati ya nchi yake na Urusi. Yupo NATO lakini bado ana mahusiano ukiyaangalia ni mazuri na Urusi. Licha ya mradi mkubwa wa gesi kwa manufaa ya mataifa yote mawili lakini ukiiangalia Ujerumani kiumakini haitaki kuingia kwenye mgogoro wenye mvutano mkubwa na Urusi. Njia iliyochagua Ujerumani ni kujenga urafiki wa kiuchumi ambayo ni manufaa kwa mataifa yote mawili.

Na hili Marekani linamuuma.
 
Putin hana maarifa ya diplomasia. Upo muungano mwingine unaoongozwa na Russia, humo kuna kina Kirgystan na Belorussia, mataifa ambayo kwa Russia hayana nguvu ya kupinga maamuzi yao.

Wanataka na Ukraine nao wawaheshimu na wawanyenyekee, kitu ambacho ni ngumu kutokea. Ukraine ni nchi yenye ushawishi inabidi itumike akili ya ziada kuweza kuwa na ushirikiano nayo.
 
Yani unamfananisha super power Mr Puttin na Marehemu katika utawala wake!!! Are you serious? Mtake radhi bwana puttin mkuu
Marehemu alipata ushauri sahihi wa kushughulika na majirani yake. Putin kiburi na udikteta unamsumbua. Aliongoza Russia halafu kipindi chake kilipoisha akajifanya kuwa waziri mkuu ili ategeshee tena nafasi ya kuingia ikulu.

Ni sawa na hapa bongo Kikwete arudi tena ikulu mwaka 2025 baada ya Samia kuongoza kwa miaka minne.
 
Magufuli alishindwa. Alihonga tausi wetu na bado uhasama haukuisha, aliyemaliza uhasama na Kenya ni Samia Suluhu
Bomba la gesi linalokwenda kuuchangamsha uchumi wa Tanzania lilisainiwa mara ya kwanza na hayati JPM, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Ujerumani na Urusi naweza kusema wana historia mbaya baina yao hususani ukiangalia WW2. Mfano battle of stalingrad. Ni moja ya pambano baya sana yenye unyama mkubwa sana lililopiganwa baina ya Urusi na Ujerumani ya Hitler kuliko pambano lolote lililopiganwa kwenye WW2.

Ujerumani ilipeleka wanajeshi millioni 1, vifaru 1700 na ndege jeshi 2000. Zote kwa uelekeo mmoja kwa wakati mmoja zilielekea Urusi kuiweka Moscow chini ya Ujerumani. Ni jeshi kubwa ambalo Mjerumani hakupeleka sehemu yoyote isipokuwa Urusi. Kwa hili, Urusi ilipoteza wanajeshi na raia waliyojitolea kupambana na Ujerumani millioni 1+.. Ni sacrifice kubwa haikutokea mahala popote duniani kwenye hii vita isipokuwa Urusi tu.

Hii ni historia, inabeba maumivu na inabeba hisia. Wakati mwengine in a we za kubeba uhasama baina ya hizo nchi ikiwa juhudi za kimakusudi zisipochukuliwa ili kusameheana kwa kujenga urafiki na kusonga mbele.

Ujerumani analifahamu hili! Hivyo hataki kuingia mgogoro wa aina yoyote utakaoleta mkwaruzano mkubwa kati ya nchi yake na Urusi. Yupo NATO lakini bado ana mahusiano ukiyaangalia ni mazuri na Urusi. Licha ya mradi mkubwa wa gesi kwa manufaa ya mataifa yote mawili lakini ukiiangalia Ujerumani kiumakini haitaki kuingia kwenye mgogoro wenye mvutano mkubwa na Urusi. Njia iliyochagua Ujerumani ni kujenga urafiki wa kiuchumi ambayo ni manufaa kwa mataifa yote mawili.

Na hili Marekani linamuuma.
Ukraine inamuumiza kichwa Putin kwa sababu zinapakana, ule ukaribu wa pua na mdomo halafu Russia anakosa mbinu wala ushawishi wa hoja wa kumvuta karibu. Ni masuala ya ulinzi zaidi.

Ni sawa sawa na Zanzibar inavyoshikiliwa na Tanganyika. Huwezi kuelewa wala kuona umuhimu wa visiwa vikiwa chini ya Muungano lakini vikishakuwa huru ni hatari kwa uhuru wa huku Bara.
 
Tatizo sio Ukrane tatizo ni NATO na Marekani, Ukrane anatumika tu kama Nyasi.
Russia ya Putin haina maarifa ya diplomasia kulinganisha na ile ya hayati Yeltsin. Aidha wasaidizi wanamuogopa Putin au uongozi mzima hauna mtu mwenye kipaji cha maongezi ya ushawishi.
 
Marehemu alipata ushauri sahihi wa kushughulika na majirani yake. Putin kiburi na udikteta unamsumbua. Aliongoza Russia halafu kipindi chake kilipoisha akajifanya kuwa waziri mkuu ili ategeshee tena nafasi ya kuingia ikulu.

Ni sawa na hapa bongo Kikwete arudi tena ikulu mwaka 2025 baada ya Samia kuongoza kwa miaka minne.

Rais kama anakubalika kwa wa2 wake shida nini? Pro amerika mnamuona putin ni dikteta, ila mnajitoa ufahamu kwa marais wa marekani ndiyo madikteta wenyewe, wameshauwa wengi tuu waco na hatia, so utasemaje wao co madikteta!!!!
 
Back
Top Bottom