Princess Zara
Senior Member
- Dec 17, 2016
- 124
- 314
My best friend yuko dilemma.
Ameolewa mwaka jana mwanzoni yeye ana mtoto mmoja wa kiume miaka 5 alimpata katika harakati za ujana na shemeji ana mtoto mmoja wa kike ana miaka 6 naye alipatikana katika harakati hizo hizo; jumla watoto 2(na ana ujauzito wa miezi 5 sasa hivi).
Sasa tangu awali, baba wa mtoto wake anamhudumia mwanae kila kitu na walikubaliana na mumewe kuwa baba mtoto ataendelea kumhudumia mwanae maana uwezo anao na vyuma si mnavijua jamani
Mtoto huyu anasoma shule ya gharama kidogo(ukilinganisha na kipato cha kawaida cha mtanzania). Ndo shule anasoma tangu nursery hadi yuko primary sasa halikadhalika mtoto wa shemeji naye anasoma english medium nzuri tu lakini sio ya gharama kama ile ya kahandsome ka shogaangu.
Sasa mwezi uliopita shemeji kasema watoto wale ni wa familia moja lazima wasome shule moja. Rafiki yangu akasema sawa basi uongeze ada wakasome kule anakosoma huyu wangu sababu it is a better school. Akasema hapana watahamia anaposoma mwanangu akakubali kishingo upande.
Baba mtoto kufikishiwa taarifa akasema hapana, namsomesha mwanangu hivyo nina mandate ya kuamua anasoma wapi.
Kuambiwa shemeji akapanick akatema mitusi ya kutosha(sikuwepo sina uhakika) akamshutumu kutembea na huyo ex wake. Katika ugomvi akasema "hata Mama K aliniambia unaliwa tu huyo mwanaume wako wa Zamani."
Mama K ni mzazi mwenzie Shemeji baada ya uchunguzi wetu FBI tumegundua mama K ndo kashinikiza watoto wasome shule moja na hii ni baada ya yeye kuhoji iweje mwanae anasoma a cheaper school than yule mwingine? Alipoambiwa yule analipiwa na babaake ndo akamwaga sumu kibao.
Ninavyoongea hapa beste kamleta mwanae kwangu leo siku ya pili analala hapa anataka amrudishe mwanae kwa mamaake, mara anasema anavunja ndoa(najua ni hasira maana ana tumbo tayari).
Sasa akibaki na kale katoto ka kambo pekee si atakatesa tu kwa hasira maana bora wakiwa wawili.
Nimshauri nini arudi kwa mumewe aihandle hii situation? Mama Zara kashanichimba mkwara "Zara unashiriki kuvunja ndoa ya mwenzio".