ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Ndugu yangu mtu mzima sana ananizidi umri, siku nyingi nikiwa nae alikuwa anaonekana mwenye mawazo mengi sana (hakuwa anasema kinachomsumbua), hivi karibuni aliibukia kuwa mnywaji sana wa pombe tofauti na nilivyomzoea..leo kaniambia, "Bwanamdogo nina shida nataka nikueleze"..ananisimulia ,machozi yakimlenga, .."Bwana mdogo nina shida kubwa sana mwenzio, mama yako..mama yako (mke wangu) ametembea na mwanangu mkubwa wa kiume ambae nilizaa na mke wangu wa kwanza, hakika sina raha kabisa...kijana ametoroka nyumbani sijui halipo, mama anakana katukatu kuwa eti hajatembea na mwanae wakati mimi data zote ninazo, nimefikia uamuzi wa kuachana na huyu mwanamke muuaji.."..
Habari hii imenimumiza sana moyo, huyo mama ni mtu mzima sana, nimeshundwa kuamini kama hilo ni kweli au mashia ya ndoa na mama huyo yamefikia ukomo..nimemwambia mzee nipe muda nitafakari la kushauri..