"Anakana, eti hajatembea na mwanae"

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Ndugu yangu mtu mzima sana ananizidi umri, siku nyingi nikiwa nae alikuwa anaonekana mwenye mawazo mengi sana (hakuwa anasema kinachomsumbua), hivi karibuni aliibukia kuwa mnywaji sana wa pombe tofauti na nilivyomzoea..leo kaniambia, "Bwanamdogo nina shida nataka nikueleze"..ananisimulia ,machozi yakimlenga, .."Bwana mdogo nina shida kubwa sana mwenzio, mama yako..mama yako (mke wangu) ametembea na mwanangu mkubwa wa kiume ambae nilizaa na mke wangu wa kwanza, hakika sina raha kabisa...kijana ametoroka nyumbani sijui halipo, mama anakana katukatu kuwa eti hajatembea na mwanae wakati mimi data zote ninazo, nimefikia uamuzi wa kuachana na huyu mwanamke muuaji.."..

Habari hii imenimumiza sana moyo, huyo mama ni mtu mzima sana, nimeshundwa kuamini kama hilo ni kweli au mashia ya ndoa na mama huyo yamefikia ukomo..nimemwambia mzee nipe muda nitafakari la kushauri..
 
Sasa hizo data zote mbbona umezibania??tueleze mwanzo mwisho tupate upenyo wa kuanzia, ujue haya mambo ya kuhisi tu ilhali huna uhakika ni dhambbi kubwa sana!! Toa full data mkuu.
 
Ndugu huyo mzee ameshasema ana taarifa zote na inaonekana hajakurupuka, ametulia akajipanga ndio akasema so kuna ukweli hapo, asimwache! yaishe ili wayape nafasi maisha yaendelee mbele
 
Ubaya wa watoto wa nje ya ndoa. Pombe itamsaidia kutatua tatizo lake?. Mwambie apunguze pombe a relax. Aachane na mwanamke muuaji.
 
msahuri kuwa maisha ni mafupi na walikotoka ni mbali hajui yalio mbeleni huenda baadae akaja kuwa msaada mkubwa kwake ktk shida nk, yameshatokea hayo asamehe hajampa magonjwa nk,wako wazee wanaotembea na mabinti zao mbona kina mama wakijua wanalia wanasamehe yanaisha iweje yy ashindwe kusamehe?
ni ngumu ndio kuvumilia but mwambie a give up, asali na atafute kitu cha kumpotezea mawazo kama kucheza draft, mazoezi ya jioni,kucheza mpira,kuangalia match kwa tv nk pombe haiwezi kumsaidia.
 
Ubaya wa watoto wa nje ya ndoa. Pombe itamsaidia kutatua tatizo lake?. Mwambie apunguze pombe a relax. Aachane na mwanamke muuaji.

Huyu ni Muuaji kweli...

Unajua kuna methali isemayo.... mwisho wa ubaya ni aibu!
Ila hizi tabia za wamama kunanihino na watoto wao kama hivi hazikuwepo.Zimetoka wapi? Nijuavyo wanaume wameshika kasi sana kufanya haya madudu..inaelekea kumetokea usugu... " wadudu' wamebadilika na kuhamia kwa wanawake? Tibuni gonjwa hili kwa wanaume jamani kabla halijamaliza dunia.Unajua baya likifanyika lisipokemewa likaachwa kuendelea hadi kuzoeleka, matokeo yake ni kama hivi!
 
hizi laana ndo zile za kuwapatiliza wana maovu ya babazao toka kizazi cha kwanza hadi cha nne...
 
Back
Top Bottom