Anajijua yeye ni namba moja, hakuna wa kumshusha kipindi hiki lakini kitu kinachomuumiza kichwa ni uwepo wa Alikiba katika muziki wa Tanzania

G_real

JF-Expert Member
Aug 23, 2019
684
851
Ni usiku wa manane, Diamond yupo chumbani kwake, alikuwa amechoka, usingizi haumpati kwa sababu anaifikiria safari yake atakayoianza kesho kuelekea kwenye matamasha yake nchini Marekani.

Kichwani mwake anafikiria mambo mengi ila kubwa zaidi ni upinzani wa muziki uliokuwa nchini Tanzania. Anajijua yeye ni namba moja, hakuna wa kumshusha kipindi hiki lakini kitu kinachomuumiza kichwa ni uwepo wa Alikiba katika muziki wa Tanzania.

Amemuacha mbali, ila bado anaamini mtu huyo akitoa ngoma, hata kama ni mbaya, kuna watu watasema ni kali, kwa nini? Kwa sababu wanataka kumuaminisha kwamba Alikiba ni mkali zaidi yake.

Hataki kuona hilo likiendelea, hataki kuona akishindanishwa na mtu kama Alikiba, anahitaji kuwa peke yake, atoe muziki wake, asikike yeye na kusiwe na mtu yeyote ambaye atakuja na kumwambia kuna fulani ni mkali kuliko wewe.

Kwa sababu tangu awe mwanamuziki wa kimataifa ndipo, alijiingiza kwenye usomaji mkubwa wa vitabu na ndipo akakikukumbuka kitabu cha Think Smart kilichondikwa na Muisrael Michael Jericho ambapo humo alizungumzia mambo mengi, ila kubwa zaidi ni kushindana na wewe mwenyewe, yaani mpinzani wako mkubwa awe wewe.

Anapokumbuka hilo, anakurupuka, anakaa kitako na kumwangalia Tanasha aliyelala pembeni yake. Anatoka kitandani na kusimama kwenye pembe ya chumba na kuanza kufikiria, mambo yanamjia lukuki kichwani mwake ila jambo kubwa lilikuwa ni lazima kutengeneza ushindani wake mwenyewe.

Anatoka kwenye pembe ya nyumba na kukifuata kioo chumbani pale, anajiangalia, anatoa tabasamu pana, halafu ghafla, analiondoa tabasamu hilo.

“Harmonize....” ndilo jina linalomjia kichwani mwake. Hataki kubaki chumbani hapo, haraka sana anatoka huku akiwa na simu yake mkononi, anafika sebuleni, muda huo ni saa nane usiku, kupo kimya, hakuna sauti yoyote ile, anakaa kwenye kochi.

Anaanza kutafuta namba ya mtu kwenye simu yake, wala hatumii kazi kuipata, anaichukua na kuanza kuipiga.
“Harmonize pokea simu...” anajisemea.

Simu inaita na kukata, hataki kukubali, anapiga tena na tena na mwisho kupokelewa, sauti ya kichovu ya Harmonize inasikika kwenye simu.

“Bro!” anaita.

“Sarah kakukamata nini?” anauliza Diamond huku akitoa tabasamu kwa mbali.

“Hakuna! Alikwenda kwao leo! Nimechoka tu, kumbe kulala bila mwanamke ni kugumu hivi!” alisikika Harmonize kwenye simu, anaanza kucheka, naye Diamond anaitikia kwa kicheko.

“Nataka uje home tuongee!” anasema Diamond.

“Leo?”

“Sasa hivi!”

“Sasa hivi?” anauliza Harmonize huku akionekana kushtuka.

“Ndiyo! Kuna kitu nimekifikiria, naomba uje tukijadili kidogo!”

“Usiku huu?”

“Dogo acha ufala, kwani unatumia daladala? Hebu njoo mara moja,” anasema Diamond kwa sauti ya kicheko kilichomaanisha utani wa tusi lake.

“Na Rayvany nimshtue ama?”

“Hapana!”

“Mboso?”

“Hapana!”

“Lavalava!”

“Dogo unazingua! Njoo wewe kama wewe! Hata baunsa usije naye!” alisema Diamond.

“Sawa.”

Simu inakatwa, haishii hapo, anampigia meneja wake, Salam SK na kuzungumza naye, anamwambia vilevile kwamba anahitaji kuzungumza naye, afike nyumbani mara moja. Salam anakubaliana naye.

“Ngoja nimshtue Babu Tale....”

“Hapana! Njoo peke yako!”

“Yaani hata Mkubwa Fela?”

“Ndiyo! Achana nao! Hiki kitu tunachotaka kukifanya ni kikubwa na cha siri sana,” anasema Diamond na kukata simu.

Sasa moyo wake unashuka, anashusha pumzi ndefu na kutulia kwenye kochi. Ni ndani ya dakika mbili tu, Tanasha anatokea mahali hapo huku akiwa na nguo ya kulalia, anamwangalia mpenzi wake, anaonekana kuwa na hofu, anamsogelea na kumuuliza tatizo nini.

“Kuna kitu nataka kufanya!” anajibu Diamond.

“Kulipua ikulu?” anauliza Tanasha huku akiachia tabasamu, Diamond anamwangalia halafu anatoa tabasamu pana, anamvuta msichana huyo na kumuweka kwenye mapaja yake.

“Umependeza sana!” anamwambia.

“Na nini?”

“Na hiyo nguo!”

“Hahaha! Hebu toka huko!”

“Serious! Kila nikikuangalia napata jibu la kwa nini watu wananiambia nafaidi sana,” alisema huku akitoa tabasamu.

“Eti unafaidi!”

“Ndiyo! Kwenye mitandao wamesemaje leo?”

“Sijaingia kuangalia!”

“Tanasha! Unajua nakupenda sana, hilo ndilo jambo ambalo ninakwambia mara kwa mara. Sisi binadamu hatujakamilika, kama kuna kitu kitatokea kwa kuanzia huko, unaweza ukakiamini lakini si cha kubaki nacho moyoni!” alisema Diamond.

“Najua hilo!”

“Mwanzo wakati naanza muziki, nilijisemea kwamba nitahitaji familia yangu izungumziwe kuliko familia zote Tanzania, kama ilivyokuwa kwa The Kardashians! Yaani watu wawe bize na familia hii, nimefanikiwa! Si unaona hakuna page ya kimbeya isiyoandika kuhusu hii familia? This is what I wanted,” alisema huku akichukua simu yake.

“Umetumia nguvu sana kufika hapa! Ila bado sijajua kwa nini upo sebuleni usiku huu!”

“Kuna jambo muhimu nataka kulifanya!”

“Lipi? Kujiua?” anauliza Tanasha, muda wote anaonekana kuwa mtu wa utani.

“Hahaha! Halafu haya mabilioni nimuachie nani?”

“Jambo gani? Unaweza kunishirikisha?”

“Nitakwambia! Ila namsubiri Salam na Harmonize nizungumze nao!” alisema Diamond.

“Mh! Kuna usalama?”

“Asilimia mia tano!”

“Sawa! Ngoja nikalale!”

“Usiku mwema mpenzi!”

“Kwa mara nyingine tena!”

“Nitakwambia hata mara hamsini kwa usiku mmoja!” alisema Diamond, Tanasha anasimama na kuelekea chumbani kulala.
Diamond hayupo sawa. Pale kwenye kiti, ni jina la Alikiba ndilo lililokuwa likija mara kwa mara. Anaonekana kutokuwa sawa, ilikuwa ni lazima afanye jambo moja kubwa ambalo lingeweza kumshtukiza kila mtu.

Baada ya nusu saa, Salam na Harmonize wanafika mahali hapo, wanaingia ndani na wote kukaa sebuleni. Wamechoka, wanamwangalia Diamond, wanatamani kufahamu alichowaitia kwani inaonekana si suala la kawaida hata kidogo.

“Nataka tupambane wenyewe kwa wenyewe!” alisema Diamond.

“Sijakuelewa!” anasema Salam, anaonekana kuwa na wasiwasi kidogo na kauli hiyo.

“Namaanisha ninataka kufanya kama kitu alichokisema Jericho!” alisema.

“Jericho? Ndiye nani?” anauliza Harmonize kwa mshangao.

“Ni mwandishi fulani. Alisema ili ufanikiwe ni lazima ushindane na wewe mwenyewe, yaani mpinzani wako mkubwa awe wewe!” alijibu Diamond.

“Bro kila siku unakuwa na mambo mapya! Unamaanisha nini?”

“Yaani namaanisha kama unaishi sehemu, unauza chipsi, basi hakikisha jirani na sehemu hiyo pia unaweka banda jingine la chipsi bila watu kujua kama ni lako!” alijibu.

“Ili?” aliuliza Salam.

“Watu wanaokuchukia watasema hawanunui chipsi zako, wataenda kununua kwenye banda la jirani, watakuwa hawajui kama lile ni lako, watakuingizia pesa bila wao kujua, hivyo utatengeneza pesa zaidi,” alijibu.

“Mh! Hicho kitabu niazime kwanza!” alisema Harmonize.

“Utaweza kusoma Kiingereza?”

“Sarah atanitafsiria!” anajibu Harminize na wote kuanza kucheka.

Diamond alikaa kimya kwa muda, akawa kama mtu aliyekuwa anajifikiria kitu fulani hivi, akasimama na kwenda kufungua friji, akatoa kinywaji cha Pepsi na kuanza kunywa.

“Hivi mnamchukuliaje Alikiba?” aliuliza huku akiendelea kupiga fundo kadhaa.

“Ni mwanamuziki!” alijibu Salam.

“Yaani muziki wake!”

“Wa kawaida sana,” alijibu Harmonize.

“Unakubaliana na ukawaida wake?” aliuliza Diamond.

“Nakubaliana nao!”

“Sisi kama WCB ni lazima tufanye kitu dhidi yake!” alisema Diamond, kidogo akaonekana kubadilika.

“Kitu gani bro?” aliuliza Harmonize.

“Tumuueni!”

“Tumuueni?” aliuliza Salam kwa mshtuko.

“Yaap! Namaanisha kimuziki! Yaani asisikike hata kidogo!” alisema Diamond huku akitoa kicheko cha chinichini.

“Mh! Itawezekana?” aliuliza Harmonize.

“Kabisa. Nitahitaji tumuue katika staili ambayo hapatakuwa na mtu yeyote yule atakayefahamu kama tumemuua kimuziki!” alijibu Diamond.

“Kivipi” aliuliza Salam.

“Harmonize jitoe WCB!” alisema.

“Whaaaaaaaaat?” aliuliza Harmonize kwa mshtuko kupita kawaida, alionekana kutokuamini alichokisikia.

“This is our mission, ni lazima tufanye kitu kuhakikisha jamaa anakufa kimuziki. Unajua ninapendwa na watu wengi, na wengi wananichukia, hivyo ukijitoa WCB, wale maadui wangu wataanza kukuunga mkono wewe,” alisema Diamond.

“Mh!”

“Yaap! Wataachana na Alikiba, wataanza kunishindanisha mimi na wewe, yaani hawatokuwa na nguvu ya kumzungumzia Alikiba. Kuna media ambazo hazipigi ngoma zetu, najua watakuunga mkono, na inawezekana hata kwenye interview watakuita, ukifika niponde sana, nichakazechakaze lakini mwisho wa siku tunatengeneza kitu kimoja, kumuua Alikiba kimuziki!” alifafanua Diamond.

“Hapana! Mimi siwezi!” alisema Harmonize.

“Huwezi nini? Kujitoa?”

“Hilo naweza kujaribu, ila kukudiss, kukuponda, roho itaniuma sana, siwezi!”

“Basi poa! Wewe fanya vyovyote, hata kama kwenye interview hutoniponda lakini nataka mwisho wa siku watu wajue umejitoa WCB, sasa ianze vita upya, Diamond vs Harmonize na si Diamond vs Alikiba,” alisema Diamond.

“Ni wazo zuri sana,” alisema Salam.

“Hii ni siri, hatakiwi kufahamu mtu yeyote zaidi yetu sisi watatu. Linapotokea suala lolote, tuwasiliane kwa kupigiana simu na si kutumiana meseji. Yaani mbali na sisi watatu, hakuna mtu yeyote anayetakiwa kulifahamu hili. Hii vita inakuwa imetengenezwa kwa mlengo fulani lakini pia itakufanya ujitengenezee mashabiki wengi, yaani kwa kifupi hii vita itakuwa ni WCB vs WCB na si Diamond vs Harmonize, hii vita itakuwa imesukwa kijasusi zaidi,” alisema Diamond huku akimalizia kunywa Pepsi yake.

Mipango ikapangwa usiku huo, kila kitu kikakubaliwa na kilichotakiwa ni utekelezaji tu. Wakatawanyika na siku iliyofuata Diamond akampigia simu Harmonize na kumwambia kwa kuanza kabisa, atawatumia watu wake mitandaoni kuanza fununu za yeye (Harmonize) kutaka kujitoa WCB lakini pia ili kuonyesha hilo linaweza kutokea, anatakiwa hata kuhudhuria shughuli nyingine za wapinzani.

“Kwenye huu msiba wa boss Ruge, nenda, mimi nitakuja na sitokaa sana, kumbuka kila kitu kinaanza kutengenezwa hapo, jifanye kama unaanza kuomba suluhu kimyakimya, halafu watajichanganya tu, wataingia kichwakichwa, tutakuwa tumemaliza kazi,” alisema Diamond.

“Sawa bro!”

“Na fanya juu chini ule Wimbo wa Kwangaru ugeuze uwe wa kumsifia rais, tunafanya hivyo kwa sababu mwaka ujao ni uchaguzi, nitahitaji upate pesa kwanza, ujiongoze kwa muda huku hii vita ikiendelea na kuwachanganya maadui zetu, nakuahidi baada ya miezi mitatu ya wewe kujitoa WCB kizushi, hutomsikia Alikiba wala mwanamuziki yeyote atakayeshindanishwa nami zaidi yako!” alisema Diamond.....
 
japo stori umeitengeneza,. ila ukweli alikiba ajiandae kufulia sana asipokuwa mjanja... hater wa diamond ndio walikuwa wanamfanya awe juu.. hao hater watahamia kwa harmonize..

hapo alikiba anatakiwa akaze sana ili asipotee
 
japo stori umeitengeneza,. ila ukweli alikiba ajiandae kufulia sana asipokuwa mjanja... hater wa diamond ndio walikuwa wanamfanya awe juu.. hao hater watahamia kwa harmonize..

hapo alikiba anatakiwa akaze sana ili asipotee
yah kweli Mkuu wapo kumpoteza
 
"E="in ha, post: 33287731, member: 460246"]
Upo talented sana
Hii ni kama story ila inaweza ikawa na ukweli ndani yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOTE]"kweli mkuu inawezekana.
 
"E="in ha, post: 33287731, member: 460246"]
Upo talented sana
Hii ni kama story ila inaweza ikawa na ukweli ndani yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOTE]"yah 80% inawezekana.
 
"E="The Great Emanuel, post: 33287769, member: 282687"]
Umefikiria mbali sana jamaa whatever the case Ali ameisha iwe ni kweli au si kweli.
[/QUOTE]"kweli mkuu
 
"E="troublemaker, post: 33287799, member: 294185"]
Ni fikra lakini zinakaribiana na uhalisia. Huenda ikawa mbinu pia.
Hii ishu ina madhara makubwa sana kwa Alikiba kiukweli.
[/QUOTE]"na mpaka saizi kashachelewa.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom